Interview with Mwita Maro in Maji Moto

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.
Photograph of Mwita Maro
Photograph of Mwita Maro
00:00
00:00

Title

Interview with Mwita Maro in Maji Moto

Creator

Mwita Maro, Jan Bender Shetler, David Maganya, Kinanda Sigara, Ibrahimu Mtatiro Kemuhe

Contributor

Nyamusi Magatti (transcriber)

Description

In this interview with Mwita Maro, he discusses his personal history, Abamare and Ngoreme origins, and Bumare sacred sites and ritual (emisambwa). He also discusses the Baragumu of the Rikora, a trumpet which is blown if something significant happens such as a meeting, war, or theft of livestock. He talks about historical and economic topics like the division of meat, the Maasai wars and settlements, famines, as well as Arabs and Germans.

Language
Ngoreme
Swahili
Ethnicity
Ngoreme
Sex

M

Birthdate

1924

Date Original

29 September 1995

City

Maji Moto

District
Serengeti
Region
Mara
Country

Tanzania

Theme
Cultural Memory
Subject
Famine
Origins
Relations with others
Ritual
Territory
Original Format
Interview
Digital Format

audio/mp3

Source

Jan Bender Shetler Collection, Goshen College

Publisher

Goshen College

Rights Management

Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International (CC BY-NC-SA 4.0)

Contributing Institution

Jan Bender Shetler; Goshen College; Matrix: Center for Digital Humanities and Social Sciences at Michigan State University

Biography

Mwita Maro was born in 1924 in Bumare, Bitakonga and did work in the Geita mine from 1939-46. He was helpful in writing the Ngoreme history with Phillipo and others. He did his Asaro in 1942. He worked at the Maadui mine from 1946-50 and became a driver at Maadui after a course in 1948. In 1950, he returned home to marry. In 1952, he was a messenger for Mtemi Simeyu. He went to Musoma as a driver in 1954 and returned home in 1960. He was the chair of the village from 1973 to 1976 and was Mzee wa Mahakamu. He holds the Baragumu for his Rikora, given to him in 1957.

Transcript

I108 Mwita Maro, Maji Moto, 29 September 1995, (Ngoreme). In Swahili and Ngoreme. Interviewed by Jan Bender Shetler, David Maganya, Kinanda Sigara, and Ibrahimu Mtatiro Kemuhe. Transcribed by Nyamusi Magatti. Mwita: {kilugha} A: hiyo ilikuwa ni summary tu, jina anaitwa Mwita Jan: anaitwa Mwita A: Maro Jan: Mosi, Mosi nani? Mwita: Mosi Sasi Jan: Sasi nani? Mwita: Sasi Wesinge Jan: Wesinge haha Wesinge? Mwita: Wesinge Machage Jan: Machage? Mwita: Machage Nyarutare Jan: Nyarutare? Mwita: Sarigoko Jan: Sarigoko Mwita: Sarigoko Rutorora Jan: Rutorora Mwita: Rutorora Mumbia Jan: Mumbia haha Mwita: Mumbia Mmare Jan: haha sawa aah kumbe hatujampata huyu mtu Mmare sawa hamati yako? Mwita: hamati yangu ni Mmare, ndio tumetoka kwa Mmare huyu Jan: haha nimesikia kuna wamare ambao ni wasweta wamare waeregi wamare wa aina nyingi? Mwita: Mmare, lakini ni mwiregi Mumbia Jan: Mumbia ni huyu motto wa Mmare Mwita: eeh (laughing) Jan: haha sawasawa zinaingiliana Mwita: zinalingiana Jan: sawa rikora yako? Mwita: Maina.. Jan: aah wewe ni upande wa chuma? Mwita: hapana wasai Jan: wasai aah hawa ni watoto wa hawa wagamunyeri haha Mwita: wamasaai Jan: haha na sega yako ? Mwita: Maina Jan: aah samahani saro yako? Mwita: umuruka Jan: umuruka haha Mwita: saro ya kina baba Jan: hii ni yako? Mwita: eeh ndio hiyo ni yangu Jan: na ilikuwa mwaka gani mlifanya? Mwita: arubaini na mbili ndio saro yangu Jan: haha ni hii saro yako ni katika upande gani wa sega wa burumaranja, bungererati? Mwita: busahi Jan: busahi haha sawa Mwita: {kilugha} omusai Jan: omusai sawa.. unaweza kujua mwaka wa kuzaliwa? Mwita: 1924 Jan: ulizaliwa wapi? Mwita: hapa hapa Bumare Jan: Bumare sehemu gani? Mwita: Bitakonga Jan: Bitakonga haha halafu ukahama sehemu nyingine au ni? Mwita: sijabadilisha kwenda mahali pengine ni hapahapa Jan: au ulienda nje kwa kazi au? Mwita: kwa kazi nilikwenda nje? Jan: ulienda wapi? Mwita: Geita Jan: haha ukafanya kazi gani? Mwita: aah nilikuwa nachukua mchanga ndani ya mine Jan: haha ilikuwa mwaka gani? Mwita: 1939 Jan: haha mpaka mwaka gani? Mwita: mpaka arubani na sita nikatoka Jan: mmh ulikaa sana? Mwita: ndio Jan: ulienda sememu nyingine? Mwita: Mwadui Jan: mpaka Mwita: hamsini noti Jan: haha ulikuwa na kazi ileile Mwita: hapana hapo nilijifunza udereva, mwaka arubaini na nane Jan: kwahiyo ulipoenda Mwadui ulikuwa dereva? Mwita: aah nimeanzia huko Jan: haha halafu ukafanya nini? Mwita: nikarudi hapa nyumbani Jan: mwaka? Mwita: mwaka nilisema hamsini Jan: aah ndio ulirudi kwasababu baba alikuomba urudi au uliona tu? Mwita: niliona nije nikapumzike nikaoe Jan: haha ulikuwa bado kuoa Mwita: nilikuwa bado kuoa Jan: haha baba alikuwa bado yupo? Mwita: eeh baba alikuwa yupo Jan: na mama wote? Mwita: wote Jan: sawa kwahiyo baada ya kurudi nyumbani ulishika kazi nyingine hapa? Mwita: niliendelea kukaa nyumbani hapa, kuwa mtemi Simeo Jan: messenger? Mwaka hamsini na? Mwita: na mbili Jan: na mbili Mwita: mpaka hamsini na tatu, hamsini na nne nikarudi tena Musoma Jan: haha Mwita: {kilugha} Jan: aah sawa halafu Mwita: sasa nikakaa pale Musoma kwenye mwaka hamsini na nne mpaka mwaka sitini ndio nimeacha kazi pale Musoma nikaja nyumbani hapa Jan: ukaona hapa nyumbani? Mwita: eeh nikaoa, sasa mzee akafariki Jan: haha sawa na uliporudi nyumbani ukashika cheo Fulani? Mwita: nikaendelea kuwa mwenyekiti wa muda kama miaka mitatu Jan: mwenyekiti wa? Mwita: wa kijiji Jan: kijiji..mpaka mwaka gani? Mwita: sabini na tatu#sabini na sita Jan: na baada ya kuacha uenyekiti? Mwita: nikakaa hapa nyumbani, mahakama nimefanya kama miaka mitatu Jan: haha sawa na upande wa mila na desturi ulikuwa na unafanya ulipata cheo chochote labda kwenye nyangi au mambo mengine Mwita: sijapata cheo A: amekabidhiwa# Mwita: hiyo nayo ni cheo..kupiga baragumu Jan: haha kupiga baragumu A: amekabidhiwa baragumu ya rikora Mwita: {kilugha} Jan: hiyo ndiyo baragumu ya rikora? Mwita: eeh Jan: eeh kumbe inatengenezwa hii ni ya ng#ombe au ni nini? Mwita: ni mnyama gani? A: Mngirisi {kilughaa}angalia Jan: aah nitapiga picha kabisa Mwita: haha hii ndio tandara mpaka hapa, ndio ile mpaka pale ndani lakini hii ni nyati.. Jan: nyati haha#kwahiyo ulisema inapigwa wakati gani? Mwita: wakati kama ng#ombe zimeibiwa, wakati wa vita au wakati wa hatari Jan: ukitaka kuita mkutano unaweza? Mwita: ndio, inapigwa saa kumi na mbili ya jioni na saa kumi na mbili asubuhi Jan: haha na bado unaitumia au hapana Mwita: si ndio naitumia Jan: lakini unaipiga Mwita: nalipuliza Jan: kama ngome zinaibiwa hata leo ungeipiga? Mwita: naipiga hata sasa wakisema kama nimesikia A: kama ile tarumbeta Mwita: tarumbeta kama ya jeshi Jan: sasa ulikabidhiwa mwaka gani? Mwita: hii nimekabidhiwa mwaka# hamsini na saba Jan: hamsini na saba..na asaro yako ilikuwa mwaka? Mwita: arubaini na mbili Jan: arubaini na mbili, hiyo haikuwa kwenye saro yako? Mwita: sikukabidhiwa kwenye saro yangu, ilikuwa bado Jan: kwahiyo ilikuwa kwenye saro ya akina nani ulikabidhiwa? Mwita: wa baba zangu Jan: lakini ni? A:{kilugha} Mwita: ilikuwa sio nyangi, siku hiyo ilikuwa ni mkutano wao wanakwenda kumsaidia Manangokowalisema leo tumechoka leo vijana wetu, tulikuwa wasare wote Jan: haha Mwita: kwahiyo ilikuwa ni kama sherehe, yeyé alipewa na wamare tu Jan: na wamare, wagamunyeri na wamare Mwita: eeh maana hii ni yakwetu tu wamare na kila kabila, kila koo hapa ina yao Jan: mmh haitegemi kwamba ni wamare wa abairegi au wamare wa nini na nini, ni wamare wote? Mwita: haha hii ilikuwa ni wamare, tuseme zilikuwa ni kabila hii mbili na ile ya mnyama ilikuwa ya tatu kwahiyo sasa hii moja ilikuwa kwa huyu na nyingine tena ndogo yake ilikuwa kwa Werege Jan: hakuna nyingine? Mwita: ziko tatu Jan: kwa wamare? Mwita: eeh kila kabila kwetu hapa au kila mlango unataka uwe nazi hivi..vitatu A: huwa ziko nne, huwa na ile tarumbeta, kadogo kale vijana wadogo wadogo wanapewa Mwita: tarumbeta Jan: mmh kwahiyo wanazigawanaje? Mwita: kwenye nyumba Weregi Jan: Weregi wanayo moja Mwita: moja, Weregi ya ukoo wa huyu walikuwa nayo moja na sisi Weregi tulikuwa nazo mbili Jan: kuna Waeregi wa aina mbili? Mwita: Weregi wa aina mbili Jan: kwahiyo Waeregi wa kwenu wanaitwa Waeregi nani? Mwita: Waeregi wa abahiri Mumbia Jan: abahiri Mumbia haha na waeregi hawa wengine wanaitwa? Mwita: {kilugha} Jan: barimande haha kwahiyo watatu kwa.. Mwita: wa kisero wapo {kilugha} Jan: kwahiyo abakisero wana moja? Mwita: eeh Jan: ya wamare haha na ya wane? Mwita: wanne wasweta Jan: wasweta haha lakini hii ilikabidhiwa tofauti na hizi zingine? Mwita: wao vilevile wanakabidhi kulingana na siku ile inakbidhiwa ni wote tulipewa, sasa wakatoka akina baba wakatuachia sasa {kilugha} Jan: haha Mwita: {kilugha} Jan: na ulikabidhiwa mambo mengine siku ile? Mwita: aah hapana Jan: ile nyama? Mwita: nyama hii ya kuchukua juzi, tulikuwa tunakula wakati tunakabidhiwa A: huku kwenye makabidhiano sasa vijana wanakula nundu Jan: sawa Mwita: wanakula nundu ya ng#ombe Jan: mmh Mwita: na wazee wanakula mgongo, sasa tuendelee hapo nyama za mgongo halafu wazee wakubwa wazee wakora nyangi wanakula sarara Jan: sarara ni wapi? Mwita: sarara ndio nyama hizi laini, hizi za humu Jan: aah na kichwa nani anakula? Mwita: aah hiyo thamani Jan: haina haha Mwita: sarara nyama laini sawa sasa hapa uje uandike vizuri hawa ni wakora nyangi halafu hawa ni wazee wa makamu Jan: sawa Mwita: eeh sasa hawa ni vijana, sasa yeye wakati amepewa hii alikuwa yuko hapa bado hapa kwasababu huyu nimekuambia ndio mtangi wa wagamnyeri Jan: mmh na mtangi wa? Mwita: wagamnyeri Jan: wa Maina? Mwita: wa wagamnyeri Jan: aah mtangi wa Mwita: mtangi si ni motto wa kwanza, ndio Maina sasa huyu ndio mkubwa wetu wote Jan: haha sawa kwahiyo kazi yako kama wewe ni mtangi ni nini? Mwita: sasa mimi ni mtangi kwakuwa mimi ni mtu mkubwa kwa sasa hivi mwaka juzi ndio tumekabidhiwa sasa mgongo tunaanza sasa kwenda polepole tunakuja kung#atuka sasa ila hii bado hatujakabidhi vijana wetu ila sasa tumeshakula mgongo tumehama kwa hiyo A: kung#atuka kutoka kwenye nundu tunakuja kwenye mgongo, uking#atuka kwenye mgongo unakuja kwenye sarara Jan: kwahiyo wakati wazee wanang#atuka wao wanaenda kula mgongo wanaachia nyinyi Mwita: eeh wanawaachia vijana sukubi Jan: haha A: hapo labda tueleze kuwa unapokuwa kijana unakula sukubi Mwita: basi angalia mfano mzuri hapa unapokuwa mzee wa makamu unakula mgongo, unapotoka kwenye uzee sasa unaenda kwenye uzee kabisa unakula sarara Jan: sawa Mwita: na wanalia watu, huwa kuna sehemu ya kulia, si ovyo ovyo A: kuna vyombo vyake Jan: haha sawa Mwita: sukubi inaliwa ndani ya zizi {kilugha} nje ya zizi kwenye ekehita, halafu mgongo inaliwa ndani katikati ya zizi, sarara inaliwa kwenye ghala Jan: kwenye ghala Mwita: kama pale wanakaa pale halafu sinia yao ni orohongo Jan: haha Mwita: lakini hapo palikuwa pazuri Jan: haha sawa kwahiyo ulikuwa unasema wewe kama mtangi wa wagamnyeri shughuli yako ni nini? Akipiga yeyé ni kosa? Mwita: anaweza yeye baragumu kwa haraka kama kuna hatari, wanauliza kulikuwa na hatari gani? Jan: lakini mtu mwingine hawezi kupiga au ni wewe tu? Mwita: kama siku tuna kikao au mkutano mkuu anajifunza tu Jan: haha sio mbaya Mwita: sio mbaya, lakini huwezi ukaipiga hivihivi mpaka siku ya matukio Jan: mmh kitu ambacho nilitaka kujua ni kama huyu mtangi ana wajibu wowote katika ulinzi wan chi kwa jumla au? Mwita: kwa ukoo wao ni mtu kama anaheshimiwa au kama kuna shughuli Fulani unaweza kusema wewe pamoja na huyu nani mkubwa Fulani nenda wewe utuitie mtu Fulani pale eeh sasa akikataa wanasema yani unatumwa na mtu mkubwa unakataa eeh Jan: na wakati wazee waling#atuka walikufundisha mambo mengine ambayo ni wewe ambao unakabidhiwa una..? Mwita: ipo nyangi ambayo tunaifanya kama hawa hawajaifanya yani kuporona, ndio nilishakuonyesha namna ya mila kuporana Jan: ulifanya eborana? Mwita: eeh nilifanya eborana Jan: na walikufundisha mambo ambayo bado unaitumia? Mwita: nayatumia kwa mazingara waliyonifundisha Jan: haha..na inahusu kazi yako ya mtangi au hapana? Mwita: hiyo inahusu mila na desturi kwa wangoremi waliotairi borana kama siku ikitokea mahali fulani wewe umefika ndio unaonyesha Jan: na kama wewe umeborana unaweza ukaborana motto wako au? Mwita: ndio Jan: unaweza ukafanya? Mwita: ninaweza nikafanya kwa mzee yeyote atakayefanya ananizidi analeta watoto , nachukua kama huyu wa kwangu nampereka anakwenda kuborana kabla mimi sijaifanya hapa Jan: mmh aah sawa na kuna mengine ambayo walikukabidhi siku ile? Mwita: hapana Jan: ni hii, na ulisema siku nyingine ulipata nyama kukabidhiwa? Mwita: eeh Jan: si siku ile? Mwita: si siku ile Jan: haha na wanachagua siku yoyote ambao wamekusanyika? Mwita: ni siku wanaokusanyika wanaona hiyo kitu, hao wanafuatwa Jan: hawakuita sherehe? Mwita: hawakuita Jan: maalum? Mwita: eeh hawana sherehe maalum, kama hiyo waliona Jan: na hii inaitwa kuteneka au hapana? Mwita: hapana Jan: ni tendo gani? Mwita: ni kitu wanaona tumefika umri tumekuwa idadi Fulani tumekomaa, hata mimi leo naweza kusema tuchukue vijana wa huyu na huyu jamani ng#oma yenu ni hii tunang#atuka kama sasa tumefika ila ni watoto wanaogopa ogopa kila siku tunawaambia jamani ng#oma yenu ni hii lakini wanaogopa Jan: aah wanaogopa? Mwita: aah mimi sijui, mwingine anasema haha tunasema basi Jan: na mtangi wao mmeshajua ni nani? Mwita: mtangi tunaujua tu, yupo mkubwa Jan: haha na yeye anakataa? Mwita: anaogopa (laughing) sasa anarudi tena kusema wapo wa kwangu anamzidi huyu kidogo anajua kutandika, jamaa huyu aendelee kukaa nayo maana yeye ameshaifahamu Jan: eti ina hatari yake kwanini anaogopa? Mwita: anaogopa shauri ya kulitimisha Jan: aah ni ngumu? Mwita: ni ngumu aah A: hiyo ni sawasawa na kamanda wa jeshi, yeye anakuwa na sauti kubwa Jan: hii ambayo nilitaka kujua kwahiyo anaogopa kuna dawa au kuna nini? Mwita: maana humu ikipigwa tumbo yako inafanya nini {kilugha}, kuna ngozi ya simba humu ya ng#ombe, katikati kuna ya simba Jan: na kuna madawa madawa ndani yake Mwita: eeh ndio nakwambia.. Jan: na ni juu yako kuifanya iwe upya tena au unaiacha iwe hivyo? Mwita: haha mimi ni kupenda kutaka kuwa upya labda ikitokea mila na desturi ya huyu amefanya túseme sherehe ninaweza nikaenda nikawaambia wanatoa mkono wa kulia halafu naleta nachunika humu inatolewa hivi halafu inawekwa humu, kama hapa unaona wadudu wamekula Jan: kwahiyo ulipokabidhiwa ukapata siri za dawa yake? Mwita: eeh waliniambia Jan: kwahiyo ukikabidhi kwa mwingine na yeyé anapata siri hizo? Mwita: eeh namwambia siri hizo eeh Jan: na kuna mitambiko fulani unahitaji ufanye wakati huo Mwita: aah haitaji siku hiyo wakikukaliza wamekukaliza hamna mitambiko yoyote Jan: haha na huna mitambiko ambayo lazima ufanye unapoitunza? Mwita: hata Jan: haha Mwita: hapa ni kukabidhiwa unakwenda nayo, hata mimi nikimkabidhi kijana hao wote tumekubali leo kijana fulani ngoma yenu ni hii umeng#atuka basi wanakwenda nayo Jan: na kwa bahati mbaya ikiharibika kuna madhara yoyote inatokea? Mwita: ni kuripotiana siku hiyo hii tunasema ni tandara A: {kilugha} Mwita: ile tandara inatolewa ile ya kulia basi inachongwa sihitaji tena utafute hii kama hii ilikuwa ni ngumu unatafuta nyingine safi tena unakuja unaunga tofauti na hii Jan: lakini ni wewe unahitaji kutengeneza? Mwita: mimi mwenyewe Jan: haha labda hii ni maana kijana anaogopa? Mwita: (laughing) Jan: aah kumbe sawa Jan: basi tuendelee na historia ya Wamare Jan: sawa Mwita: kwenye mto Bumeti akabaki Mwikoma kule ng#ambo walikuwa vijana wawili, mngoremi akaja huku ng#ambo yani huku kwetu pamoja na manjia sasa akateremka nayo Jan: nani? Mwita: Mungeremi Jan: mungeremi ni nani? Mwita: Mkoma alibaki huko Ikoma kule na Mungoremi akaja huku Jan: sawa samahani sasa endelea kuhusu Ngurime akafanya nini? Mwita: mngoremi sasa akazaa hapo akapata nyingi nyingi hizo wamare, kitale ikawa Ngoremi nzima sasa ikapatikana humu milango milango mwiregi eeh wakateremka kuja kwenye milima milima zaidi ya hapo sasa sijaendelea kufahamu vizuri Jan: hujui labda majina ya wengine ambao walikuwa wametoka huko wakaja Mwita: mmh mimi najua walipotoka sasa kuwatanyika tena wengine wakatoka sehemu hizi sasa hapo siwezi kufahamu Jan: mmh hawa ambao wanataja huyu Sabayaya ni nani? Mwita: Sabayaya ndio sisi hawahawa tuliotoka, tulipotoka huku Mangweso tukaja sehemu ya Sabayaya wangoremi wa Sabayaya Jan: haha hii Sabayaya ilikuwa baada ya mngorime au kabla ya Ngorime? Mwita: Sabayaya alikuwa ameshatoka sasa A: {kilugha} kwa maana hiyo la kwanza ilikuwepo Mwita: {kilugha} A: nafikiri huyu Sabayaya ndio amemzaa Wandira Jan: haha Mwita: sio ndi ni Warira Jan: Warira haha A: tukirudi hapa tunaweza tukapata.. Mwita: {kilugha} A: nilichokuwa nakitafuta kimepotea maana nilitaka kujua kwamba wangoremi wametoka wapi nimeshapata kwa msingi huo huyu Sabayaya ni kijana, Wandira, Sabayaya Wandira kwa maana huyu ni baba, huyu ni mtoto wake Jan: sawa lakini hatujui kwamba.. {END OF SIDE A} {START SIDE B} A: ile ya kwao nafikiria huyu Sabayaya amezaa Wandira, Wandira huyu maana sisi wangoremi ndio tunajiita hivyo kwa msingi ni kwamba huyu Wandira ndiyo amemzaa Wangoremi, nina wasiwasi kitu kama hicho Jan: na kuna mlima hapa ambayo inaitwa Isabayaya ambayo huyu mzee alitaja? Mwita: si alisema pale au mimi ndio sikuelewa Jan: aah ndio alisema kuna mlima A: hii sabayaya sijaisikia Mwita: {kilugha} hiyo lakini sijui kama kuna mlima hapa A: {kilugha} Jan: sawa sasa ulisema kwamba mlikuwa pamoja na wa Ikoma sasa hata wa Ikizu wana historia kwamba na huyu mtu wao wa kwanza akaenda huko Mangwesi akampata sijui nani Sabayaya halafu akarudi tena Ikizu sasa na ninyi mna historia hiyo? Mwita: huyu Sabayaya ndiyo huyu huyu ametokea hukuhuku Sabayaya ndio akaja kuzaa sisi hapa inaitwa Sabayaya Jan: haha sawa na kwa wamare ni hawa tu ambao wametoka Sonjo au kuna wengine walikuja kuingia baadaye? Mwita: walipookuja hapa wamare wakawa wanagawanyika sasa, eeh kukawa na vijana watatu mwingine ana mji wake na kujiita mimi.. A: {kilugha} Mwita: {kilugha} Jan: abasweta na? Mwita: abasweta na abahiri magita Jan: magita? Hawa wametoka wapi? A: abasweta wametoka nafikiri ni Tarime, ni eneo la Kenya Mwita: wametokea Kenya {kilugha} A: halafu hawa nafikiri wametokea Uganda hawa Mwita: [kilugha] A: hii imetokea Uganda Jan: kwahiyo hawa wote wamare wote ambao asili ya ni kutoka Soncho wanaitwa waeregi? Mwita: [kilugha] Jan: lakini wote ni wamare? Mwita: wote ni wamare Jan: haha na ni wamare kwasababu wanakaa eneo hilo? Mwita: eneo hilo Jan: la Bumare? Mwita: la Bumare Jan: haha Mwita: ni sehemu imetoka huko juu mpaka Rusinga, wamepakana Jan: kwahiyo Bumare inaenda mpaka inafika Nguko? Mwita: aah hapana, mwisho ni hapa kwenye kamlima hapa, inapakana na wanguko halafu inakwenda huku na huku tunapakana na Kitale A: ila utakapokwenda sehemu ya White brothers utakuta kuna Bumare 1 na Bumare 2, sasa ile ramani mariwani la Bumare 2 itakuja kukufikisha kwakuwa wewe umetembelea itakuja kukufikisha karibu na Bantamome eneo la mwisho kwasababu walikuwa eneo hilo kama ni ni mrambaro wanne Jan: haha Mwita: maana hiyo milima ya Mrambano 1 hiyo ilikuwa inamilikiwa kihimaya sasa kiutawala ilikuwa chini ya Bumare Jan: ya Bumare? Mwita: ee kiutawala Jan: sawa na ukichunguza ndani zaidi ni kama Bumare ni nchi lakini kitu kama waeregi au nini ni ukoo lakini unaweza kusema wamare ni ukoo au si ukoo maana wana ujamaa au ni watu mchanfganyiko tu ambao wanakaa pamoja? Mwita: Wamare tunasikia ni wakitale lakini wako vinyumba vinyumba vinyumba, milango sasa na sisi Wamare wote ni Wamare Jan: haha sawa Mwita: sasa kwenye kugawanyikana utakuta wamo Waeregi, wasweta hapohapo tena utakuta ni Mwiregi eeh Jan: haha kwa mfano wamare wanaenda wapi kuseng#era? Mwita: wote tunakwenda huko juu milima yetu Jan: haha kwahiyo wote mnaenda kwa pamoja? Mwita: wote pamoja Jan: hata kama ni mlango gani? Mwita: Bumare hii ya kwetu ni wasai na bungerati ukitaka kwenda kusengera huku tunakwenda siku hii, moja tunapiga baragumu hapa na huku wanapiga tunakuja tunakutana hukuhuku juu Jan: na inaitwa wapi wanaenda? Mwita: Sengere Jan: Sengere A: kuna sehemu mbili, kuna Sengere kuna Nyakigumo Mwita: Nyeremande Jan: Nyakigumo A: sasa hapo umeandika Jan: Nyakisengere, Nyakigumo A: halafu kuna Remande A: mmh sasa weka dash hapo sasa hii Sengere {kilugha} Mwita: {kilugha} kwanza tunajikusanya tunaenda wapi, tunaenda Sengere tukitoka Sengere Nyaute, Nyagekenge tukishatoka Nyagekenge Jan: haha kwahiyo mnaanza Sengere halafu Mwita: Sengere Jan: halafu mnaenda? Mwita: Nyeute Jan: Nyeute halafu mnaenda? Mwita: Nyegekenge Jan: Nyegekenge halafu? Mwita: tunagawanyikana sasa Warimande wanakwenda Remande Jan: warimande Mwita: wanakwenda Remande Jan: wanaenda Remande haha Mwita: wakisero wanakwenda Romo pamoja na Wasweta Jan: haha sawa Mwita: Walimagure wanakwenda Kitachi na Nyahute {kilugha} Jan: wanaenda Kitachi na? A: Nyahute Mwita: {kilugha} Jan: Rematomano Mwita: sawasawa tunagawanyikana sasa Jan: mmh Mwita: {kilugha} tunakuja kukutana tunateremka huku Jan: mnakutana wapi tena? Mwita: tena tunateremka sasa kuja hapa kama kuja Bumare hapa kwenye kijiji Jan: na yote inafanyika siku moja? Mwita: ni siku hiyo hiyo tu Jan: aah A: anyway baada ya kumaliza sehemu kuu hizi Sengere halafu tunatoka wote Sengere tunakwenda Nyahute tunatoka wote Nyahute tunakuja Nyegekenge sasa tukishafika hapa hii nyumba kubwa, unajua hapa sasa kuna nyumba mbili, nyumba kubwa ambayo ni abahiri mombia hawaendi sehemu yoyote ile Jan: abahiri mombia ambayo ni nyumba kubwa haha A: hawa wanakaa sasa hivi nyumba ndogo zinatawanyika sasa kwenda kuiji maana hii ni kuiji wanakwenda sasa kuiji kwenye vyumba vidogo vidogo yao Jan: kuhiji? A: kuhiji sasa ni kuabudu Jan: aah sawasawa na mnafanya nini hii sehemu zote mnafanya mitambiko gani? Mwita: mitambio hapo utakuta wengine wana tumbaku wana maunga wanatambikia pale kuna maji yanchotwa mle, sasa ndio wanakuja Jan: lakini kuchinja mnachinja huko? Mwita: tunachinja mbuzi hapohapo Sengera Jan: Sengera? Mwita: Nyagikenge Jan: haha Mwita: {kilugha} Jan: kwahiyo abahiri mombia wanabaki palepale mahali ambapo mnachinja? Mwita: eeh tunangoja hawa waende kutambika huku halafu wanakuja sasa tunateremka sasa kuja chini A: halafu wanakuwaga na mbuzi wawili, wanatoa huku mbuzi moja na kule wanatoa mbuzi moja Jan: haha sawa na mnapofanya hii kitendo hii ambacho Wamare mnaenda, mnaenda kuomba nini? Mwita: kuona kama miaka imepita mingi hawajaenda unaona kama kuna ugonjwa unakuja hatari hatari wanakwenda pale na kuchukua mitambiko tambiko wanakuja kufanyia Jan: haha au mvua mnaweza kuomba? Mwita: eeh hata siku hiyo wakiomba inakuja tu Jan: ooh inakuja tu Mwita: eeh inakuja, wakati wa kiagazi tena inanyesha Jan: sasa mlifanya hii mara ya mwisho ni mwaka gani? Mwita: sikumbuki hapo, ilikuwa mimi ungali vado mdogo sana Jan: ooh kweli na hawajafanya tena? Mwita: hata ndio miaka yetu tunaterejea hawa twende A: {kilugha} Mwita: {kilugha} Jan: mnasema? A: mitambiko ya nyumbani ndio abahiri tuliyofanya pale wanafuatwa tu Jan: haha hii ya mojamoja Mwita: eeh hii ya mojamoja Jan: lakini hii ya wote? A: inafanyika mara moja tu, kwa karne tuliyo nayo sasa hivi Jan: ian jina maalum kama wote wanaenda Mwita: jina maalum tunakwenda kusengera kwetu sasa Jan: haha haina kwa kilugha haina jina kwamba wote wanaenda? Mwita: ni wote wanakwenda hakuna kilugha Jan: aah sawa Mwita: kusengera A; lugha ni kusengera Jan: aah sawa lakini nilifikiri labda ni tofauti na ile nyumba ndogo ndogo kufanya kwenda A: aah ile nyumba ndogo haiendi kusengera inafuata korosho Mwita: au mwingine anaenda kufanya mitambiko ya nyumbani Jan: ianfuataje hiyo korosho? Mwita: inafuata pale majani, kufuata maji, kufuata nini Jan: aah sawa haha sawa na ukisema hizi nyumba ambazo zinagawanyika huko si maana ya nyumba ni wake wa watu kila mke ana nyumba yake? Mwita: hapo tumeshataja umeona hii majina hayo yote kama ni kisima kikubwa chetu cha Sengere ni wote halafu inawezekana kuwa kuna jiwe lingine linakuwa la wa kisero wenyewe wanakwenda kwa niwe lao Jan: hizi ambazo umetaja ni jiwe? Mwita: eeh ni majiwe sasa inafuata milango milango Jan: hiyo remande roma? Mwita: remande ni jiwe Jan: ni jiwe na roma? Mwita: roma ni lijiwe, lina maji Jan: aah ina maji Mwita: madimbwi madimbwi, vidimbwi vya kuweza kuchotea maji Jan: na tena rematomano? Mwita: rematomano vilevile ni lijiwe limetambaa sasa lina kashimo Jan: haha na tena ina maji Mwita: eeh na maji yamo Jan: na sengere? Mwita: sengere ni mto sasa, kisima, nyaute ni jiwe lina maji Jan: haha Mwita: nyagikenge ni jiwe lina bwawa kule ndani A: lina bwawa Mwita: {Kilugha} Jan: na yote ipo karibu karibu? Mwita: eeh ipo karibu Jan: kwahiyo ni kwenye milima hiyo? Mwita: kwenye milima hizi Jan: ooh nyuma yake? Mwita: eeh nyuma yake huko juu, imesimama juu, niliona taa inawaka Jan: ooh ulimwona Mwita: niliona taa inawaka nikasema koroboi nini kumbe ilikuwa gari {kilugha} kama kuna taa unaona kule A: {kilugha} Mwita: unapotea kama hujui Jan: aaah Mwita: kama hujui unaweza ukapotea kabisa Jan: ukienda huko? Mwita: sasa mimi mwenyeji nitapoteaje na najua misimu iko hapo, watu wanapaogopa sana, sio mchezo Jan: ooh hawaendi huko ovyo Mwita: ooh kama hujui unaweza ukaangukia humo Jan: ooh kwahiyo zamani watu walikuwa wamejenga huko? Mwita: walikuwa wanakaa hukohuko mlimani Jan: aah karibu na zile visima? Mwita: vyote visima hivyo, watu walikuwa mlemle tu, akina baba wamezaliwa ni hukohuko akina mama sasa ndio wakaja kuhama wakati huu Jan: haha walikuwa wanakaa juu ya milima Mwita: juu ya milima, kama mnafanya ngome ni ngome hapo Jan: vado zinaonekana Mwita: eeh Jan: aah Mwita: {kilugha} Jan: ni kama ngapi huko? Mwita: {kilugha} Jan: aina mbili Mwita: eeh Jan: ya nini? Mwita: tatu {kilugha} A: mlima moja una bugo mbili halafu mwingine ndio una mmoja Jan: mmh#aah kumbe na ni enzi za akina nani walikuwa wamekaa huko? Mwita: walikuwa ni enzi za akina babu zangu waliozaa baba Jan: abasahi? Mwita: abasahi Jan: abanyambureti walikaa? Mwita: ndio wanyambureti sasa ndio wamekaa sasa wanahamia kuja huku chini Jan: aah na hawa abamaina ambao? Mwita: wagamnyeri sasa ndio tuli.. Jan: hawa baba wa abasahi? Mwita: walikuwa wanaishi sasa humuhumu Jan: walikuwa wanaishi? Mwita: mwenye mlima Jan: aah kwahiyo ni akina nani walijenga ubugo? Mwita: sitatambua Jan: lakini unajua kwamba wamaina walikaa pale? Mwita: wamaina walikaa humu, wasai walikaa humu sasa sijui ni akina nani waliona hiyo vita wakaanza kutengeneza lile ngome siwezi kufahamu, A: lakini kwenye zile nani zangu kuna sehemu inayosema wanaanza kutengeneza kuzuia maana ubugo unaanza kujengwa kwenye mwaka elfu moja mia nane na, kipindi cha kuzuia wamaasai Jan: mmh ndio haha A: ukiangalia humo utapata hizo Mwita: yeah ndiyo A: kipindi hicho wanaanza kutumia ugwe Jan: haha ugwe Mwita: eeh ugwe Jan: ni nini A: ugwe ndio ubugo Jan: aah ni moja? A: eeh kiswahili ndio inaitwa ugwe Jan: haha Mwita: hiyo ngome Jan: ugwe haha A: eeh kiswahili sasa ndio walianza kuitumia na pamoja na wakaja kutumia tena haya, sijui inaitwaje Mwita: {kilugha} A: ni yale mamiti ambayo yanaota kwenye#{kilugha} Jan: mmh cactus A: inaitwa huwa inazaa watoto wakiiva ndani yake ni matunda mazuri sana Jan: aah ni cactus Mwita: ndiyo Jan: walianza kufanya nini nayo? Mwita: kufanya tena kama zizi kuzuia wasiingile na wamasaai na wanyama wakali Jan: na ebotogwo ni nini? Mwita: ebotogwo sijui Jan: sijapata ile jina vizuri, hizi inaitwa nini? Mwita: chingoto Jan: abitoha Mwita: aah hiyo hapana, kiswahili hii inaitwa marangali A: unaona majani yake yapo hivi makubwa namna hii halfu yana miba miba Jan: yeah Mwita: yapo kwenye ukienda mediterrenean utaipata A: inazaa watoto halafu yenyewe Jan: yeah nimeipata kwahiyo walikuwa wanaitumia kwa kufanya Mwita: kuzuia kwenye vita Jan: kwenye ubugo? Mwita: haha wakati wa ubugo ni ubugo Jan: haha Mwita: halafu hiyo sasa ikatokea mamiba yakaja Jan: haha Mwita: {kilugha} Jan: nasikia kwa wazee wengine kwamba sijui ni wakati wa abasahi au abanyambureti walikuwa na njaa kubwa sana wengine wanaita njaa ya mogoro Mwita: eeh njaa ya mogoro eeh ilikuwepo ya abasahi hapa Jan: ya abasahi? Mwita: mmh njaa ya mogoro Jan: walikuwa vado wanaishi pale? Mwita: kwenye milima huku Jan: haha lakini ilikuwa wajerumani bado au walikuwa wameshafika? Mwita: aah wajerumani aah sasa hapo sitambui ilikuwa wajerumani au waarabu, maana wakati huu haukuwa na mtu wa kuandika mambo kama hayo, wanasema wasai walikuwa na hiyo njaa ya mogoro Jan: haha wakaenda kuenea wapi? Mwita: wengine wanakwenda Ukerewe Jan: Ukerewe? Mwita: eeh Ukerewe ndio walikwenda kufanyia, Ukerewe wanaleta viazi hapa..watu wanatoroshwa hapa na wakerewe kuenda usimbiti wanaingia Musoma Jan: haha Mwita: sasa mtu anasema nimevuka baharí sijui mto kumbe yuko hapahapa Jan: na ugonjwa wa ile mogoro ilikuwa ndui? Mwita: nini? Jan: ambao walipata wakati wa ile njaa ya mogoro? A: chebundi Mwita: aah ndui A: ndui au ndui si ndio gorondo Mwita : eeh A : malale si imetokea hapa, hii imetokea hapahapa wameham wamekuja hata mimi nina macho nimeona Jan: yeah malale ni baadaye haha A: ugonjwa uliotokea baada ya njaa ni ndui.. Mwita: gorondo ni A: na kolera Mwita: na kuhara watu walihara A: nini si yellow fever ni kolera, hasahasa huu ugonjwa tunaouita sasa hivi ni kipindupindu Jan: mmh A: eeh maana watu walikuwa wanaharisha maji wanakufa Mwita: hiyo iliua watu sana kwenye njaa Jan: mmh ulisema kuna kipindi waarabu walikuwepo? Mwita: si waarabu walifukuzwa na mjerumani Jan: sawa waarabu walikuwa hapa wenyewe? Mwita: eeh sasa walikuwa hapa waarabu ndio wakaja wakatawala wajerumani wakaja wakamfukuza Jan: lakini utawala wao si ilikuwa si ni biashara tu au walikuja kufanya nini? Mwita: sasa walikuja kibiashara na utawala humu Jan: aah Mwita: wanasema hakikisha unakuwa muislamu halafu wanaanza kuchapa watu karanga na sumu Jan: mmh karanga, wanataka wapate karanga? Mwita: eeh biashara Jan: aah na walichukua watumwa? Mwita: eeh ndio walikwenda na watu Magorondo, walikuwa wanachukulia mizigo yao wanakimbia wanapitia Ikoma huko wanakwenda huko Jan: kwahiyo watu ambao walichukua ni hawa wa kubeba vitu vyao? Mwita: mizigo eeh Jan: aah Mwita: walikuwa wanachukua mizigo Jan: kwahiyo hawakuchukua kama watumwa watu wa kuwapeleka na kuwauza? Mwita: hata hapa ilikuwa ni mizigo tu, hawakufika hapa Jan: hawakufika? A: aah wajerumani..waarabu Mwita: waarabu? A: huku hawakufika..{kilugha} Mwita: {kilugha} Jan: abasumba? A: masumba si ni wajerumani Jan: amasumba ni wajerumani, aah kumbe kwahiyo wengine wanachanganya wanaona hawa ni waarabu lakini sio? Mwita: wote walikuwa ni rangi nyeupe..abasumba Jan: amasumba hii neno ina maana gani? Mwita: hii unajua hii wasumba imeteremka kipindi ambacho wasumba ni watu wanaopenda urafiki Jan: aah Mwita: na wale watu walikuwa wanakuja kiurafiki, wajerumani Jan: walikuja kirafiki? Mwita: eeh kwa mara ya kwanza walikuja kirafiki A: walikuwa wanawadanganya hawa wakubwa wakubwa wengi kwamba mtufanyie hivi tupate hivi tupae hivi, kama wewe ulivyokuja sasa si umekuja kiurafiki? Jan: mmh Mwita: huwa wanaleta ushanga na vitu tofauti, nadhani wakawateka, huyu anasema nani ana meno ya tembo mwingine pembe ya faru wanawadanganya danganya hivi wakawaletea chuma, unajua watu wa zamani walikuwa wanataka vyuma vya shamba wanafurahi tu kumbe wanakwenda nao Jan: hahana ninyi mlikuwa mnaua tembo kwahiyo mlikuwa na meno yao? Mwita: tembo walikuwa wanauwawa hapa kwa wandorobo na wapo wangoremi waliokuwa wanapiga tembo vilevile wanafuga meno sasa wakawa wanawauzia Jan: aah kumbe aah sawa kwahiyo wajerumani walipofika kutawala walifanyaje ili wapte huyu mtemi wa kwanza? Mwita: hapo sasa sijui nilikuwa bado sijazaliwa Jan: aah hukupata jinsi walivyo? Mwita: aah sikupeleleza walifanyaje hapo Jan: mmh sawa Mwita: mwalimu anaweza akafahamu A: eeh mjerumani hapa kwetu unajua hapa walipita Jan: walipita tu? A: mwaka 1916 Jan: haha A: walikuwa wanakimbia Mwita: {kilugha} A: huwa walikuwa wanapita wanakimbia Jan: haha lakini walipoweka watemi wao ndipo waliwatawala? A: hata hawakufika huku kwetu, walikuwa bado Mwita: ooh Jan: ilikuwa kwahiyo watemi walikuwa.. Mwita: nchi ilikuwa iko chini ya mjerumani lakini na mtu yoyote aliyekuwa kwa kipindi hicho anatawala alikuwa chini ya uongozi wa kijerumani, kiinchi Jan: sawa wenyewe Mwita: lakini wajerumani wenyewe kufika walikuwa hamna, walikuwa bado ila wamepita sasa kipindi wanakimbia walipita hata ukienda kule Mguteni utakuja kukuta walipita halafu fedha yao noti zilifika mwaka 1916 na watu walitairi wanaita hizi vinoti Jan: aah sawa eeh vizuri Mwita: halafu hata hawa wenye sandeko ndio wajerumani walipita wenye sandeko hawa wakawa wanabeba yale masanduku Jan: haha Mwita: mizigo yao hiyo A: {kilugha} Mwita: kama kuna mtu amekwambia kwamba kuna keha {kilugha} Jan: yeah Mwita: kumbuka hapo usidanganywe baba kwasababu hii tohara ya kampuni ni kipindi kile wajerumani wameanzisha utawala wao kimakampuni Jan: mmh Mwita: kutoka mpaka Afrika ya kusini Jan: sawa Mwita: ndio tukafomu jina abakabwe unaona, tukahama pale tukaja mwenye sandeko hicho kipindi ambacho wajerumani wakawa wanaondoka A: kampuni hiyo kama ulisikia akina mama yangu walikuwa na vinoti Mwita: vinoti ni kipindi wametoa nini, wametoa hizo noti zao za kwanza mwaka 1915# Jan: haha sawa kwahiyo naomba mzee.. {THE END OF TAPE # 16O, DONE BY NYAMUSI MAGATTI, AUGUST, 2009}

Show Full Transcript Download Transcript PDF

Field Notes

Baragumu of the Rikora -- Given to Abamaina in 1957. Pembe ya Tandara, leather of Nyati below for scoop. Is blown if cows are stolen or there is a war, or a meeting. There are four baragumu in Bumare according to clan: 1. Wairegi -- Abahiri Mombia 2. Wairegi -- Abahiri Barimande 3. Abikisero 4. Abasweta [RIKORA/RITUAL; GEN4] Division of meat 1. Vijana -- eat outside of the zizi, at the ekehita. eat the sukubi, nundu, 2. Wazee vijana -- eat inside of the zizi, ekesero, eat the mgongo. 3. Wazee wakubwa -- Wakora Nyangi -- eat by the ghala, out of an orohongo, ear sarara, laini meat. Mtangi of the Gamunyere -- respected, has done Eborano at least. The Baragumu has dawa in it, lion skin etc. Has to be kept and maintained properly. Origins -- Abamare from Soncho to Manyare to Mangwesi to Grumeti -- Ikoma on one side and Ngoreme on other. They gave birth to: 1. Mare 2. Kitare 3. Wiregi 4. Kisero. Isabayaya and Wandila. [ORIGINS/NGOREME; ORIGINS/MARE] Some came from Tarime and Kenya 1. Abasweta 2. Abahirir Magita -- from Uganda and the lake Those from Soncho 1. Iregi 2. Gisero [SONJO; GOSI] Emisambwa of Bumare If all of the Wamare go together they all go in this order: 1. Start at Sengere, a spring. --> 2. Then to Nyehuti, a spring in the rocks. --> 3. Then to Nyegekenye, a pool in the rocks. Here the Abahiri Mombia stay back, they are the first and the wakubwa of all Wamare, they wait till the others go on to their places. It is here where the white goat is killed for all. -- the Warimande go to Remande, a spring in the rocks -- the Kisero and Sweta go to Roma, a spring in the rocks -- the Warimaguri go to Kitache and Rematomano, a spring in the rocks. Then they all go back down the mountain together. They go to clean the spring or for sickness or rain. All Wamare go or just one household. [EMISAMBWA] Settlements -- Maasai wars Obugo -- still can be seen about three of them up on the mountain where the risambwa are. Built during the old Abamaina, Abasaye and Abanyambureti last to live in them. used cactuses around compound after moved out. [FORTS; GEN2] Anchera ya Magoro -- Abasaye. Ndui, Barondo. Kipindupindu. went to Ukerewe. potatoes. [FAMINE] Arabs -- bought peanuts, slaves as porters. Many died along the way as porters, never came back. Amasumba -- Germans, people who come as friends and then change to rulers. beads. ivory from Ndorobo. brought iron ornaments. 1916 pass through -- Monyasandeko had to carry their loads, forced. As Germans left. 1915 asaro group called Wanoti from introduction of German money. [GERMANS; ARABS; TRADE]

Show Full Field Notes Download Field Notes PDF