Interview with Ginanani Chokora and Gejera Ginanani in Kyandege

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.
Photograph of Ginanani Chokora, Gejera Ginanani, and Mnada Joseph Mayonga at interview
Photograph of Ginanani Chokora, Gejera Ginanani, and Mnada Joseph Mayonga at interview
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00

Title

Interview with Ginanani Chokora and Gejera Ginanani in Kyandege

Creator

Ginanani Chokora, Gejera Ginanani, Jan Bender Shetler, Mnada Joseph Mayonga, Nyawagamba Magotto

Contributor

Nyangere Esther Faini Magoto (transcriber), Rose Wang'ombe Mtoka (transcriber), Nyamusi Magatti (transcriber)

Description

In this interview, Ginanani Chokora and his son Gejera Ginanani talk about Dadog origins and the livelihoods of the Dadog people in the Mara region. They also mention colonization, farming, and migration. They discuss cultural topics such as leaders, age sets, and generations.

Language
Datooga
Ethnicity
Tatoga
Sex

M

Date Original

26 July 1995

City

Kyandege

District
Bunda
Region
Mara
Country

Tanzania

Theme
Gender and Livelihoods
Linguistic and Cultural Patterns
Subject
Age and Generation
Group names
Leaders
Livelihoods
Migration
Neighbors
Origins
Territory
Original Format
Interview
Digital Format

audio/mp3

Source

Jan Bender Shetler Collection, Goshen College

Publisher

Goshen College

Rights Management

Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International (CC BY-NC-SA 4.0)

Contributing Institution

Jan Bender Shetler; Goshen College; Matrix: Center for Digital Humanities and Social Sciences at Michigan State University

Biography

Ginanani Chokora was born around 1918 in Natta, at Nyanduge. He then moved to Moreri during the time of war between the Germans and the English. He was still nursing at the end of the war. His father died when he was still young and unmarried. He went to live with his in-laws and later moved to Iriahika in Ikizu -- Heyera Gunyigeka where he was circumcised. Then, he moved to Sarakwa, where he married his first wife. He then went to Sasira, where he began to work for his father-in-law to marry his second wife. He left first with Shemeji. He went to Ikoma with his father in law (Baba mkwe), the Issenye, Ragana. Then he went to Raho. Then, his father-in-law said he had worked enough, 10 years, but wanted him to stay. They cut another gate in the fence of the cattle kraal. He went to Riharaha before villagization and moving to Kyandege. He took a third wife in Raho. He is a livestock herder and a prophet (for the Relimajega). Gejera Ginanani was born in 1944 in Raho. He has always been a herder and did not go outside to work. He still keeps his father's herd.

Transcript

I59-60 Ginanani Chokora and Gejera Ginanani, Kyandege, 26 July 1995, (Tatoga). In Swahili and Datooga. Interviewed by Jan Bender Shetler, Mnada Joseph Mayonga, and Nyawagamba Magotto. Transcribed by Nyangere Esther Faini Magoto, Rose Wang'ombe Mtoka, and Nyamusi Magatti. G: [KITATURU] J: Unaweza kutafsiri jinsi anavyo ... M: Anasema, anavyofahamu yeye anasema Wataturu wametokea Kaskazini. Sasa, wametokea Kaskazini likiwa kundi kubwa la watu, sasa walipofika maeneo haya walikuwa na punda. Wale punda wakawa wamepotea, sasa hawa waliobaki hapa wakabaki kwa sababu #### Wakabaki kutafuta punda; na walipo wapata sasa wengine wakaendelea Kusini, walipofika sehemu nyingine wakawa wengine wakasema wamechoka. Sasa kuchoka kwa Kitaturu wanasema Gereriga, kwa maana ya kwamba walichoka. J: Bureriga. M: Bureriga kwa maana ya kwamba walichoka wakaachwa pale ikawa ni #.. nyingine halafu wakaenda sehemu nyingine wakaachwa watu wengine ambao waliitwa Barabaiga. G: Wanasema tunataka kukata fiimbo. M: Yaani kwa ajili ya wao walibaki, wao wakasema sisi tunabaki hapa kukata fimbo yaani Barabaigi. J: Hii maana ya Barabaiga? M: Nao wakabaki pale wakaishi pale. G: Ni kitambo ############# J: Lakini, nani alitangulia? G: Sijui, ni sisi ##.. hii nchi ni yetu, sasa na sisi unaona sisi Watatiro, Watatiro walikuwa ni watu wa ngombe. Na sasa, siku ile mzungu aliingia hapa anasema, #jameni tunataka watu, kila watu watupe kila watu sehemu yao, kila watu sehemu yao.# Wataturu wakakataa wakasema, #sisi kama unafanya hivi tutafanya makazi mengi, na sisi ni wachungaji wa ngombe.# Wakakataa wakawa kama ni watu wa mpande wote Wisenye, Wikoma, Wanata wakawa wanachanganya changanya hawa ni kama hawa wakasema, #sisi hapana taka Mtemi, sisi ni hivi hivi# wakakataa. J: Kwa hiyo walikataa utemi? G: Walikataa. J: Si wakati wa Mjerumani au wa Mwingereza? G: Wa Ujerumani. J: Mjerumani. G: Wajerumani walitangulia kuja, Mjerumani alitangulia, sasa Mwingereza akaja Mjerumani akatoka. J: Hebu turudi kwenye ile mwanzoni. Ulesema wametoka Kaskazini lakini unajua Kaskazini ni wapi walitokea? G: Huku [KITATURU] M: Anasema haelewi ni sehemu gani lakini anasema ni Kaskazini wa Ethiopia na Somalia ndipo waliko tokea. J: Lakini kwenye historia ya zamani wanataja mahali tulipita hapa tumepita hapa, ipo au? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema, hana kumbukumbu ya mbali sana lakini anasema maeneo ya Kusini mwa mto Mara kuja sehemu za Ngoreme kuna milima; anasema kuna milima fulani ime, iko kwenye mkondo fulani ya milima imejitokeza tokeza kama ni mikondo ya milima ##.. sielewi ni maeneo gani , lakini nafikiri eneo la Maji Moto kuna kanda fulani ya milima tu, anasema unaitwa Robacheki. J: Rogwa. M: Rogwacheki. J: Labda uandike tu maeneo yote ambayo ametaja Rogwacheka ni huko sehemu za Ngoreme, halafu . M: Ni maeneo haya Rogacheka, J: Na hii ni kama mahali ambapo waliiingia kwanza? M: Anasema hapa ndipo nafikiri maeneo walipofanya makazi kwa mara ya kwanza. J: Halafu kuna walipotoka huko wakenda ni sehemu gani? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema kwa kweli hakuna mtu mwenye kumbu kumbu nzuri kwamba walikotokea kule Kaskazini ni sehemu walikoachwa hawa Watatoga ambao huwa, yaani sisi hawa tulioko humu tunaitwa Rotigenga. Rotigenga kwa maana ya kwamba tuliachwa baada ya punda kupotea waliokuwa tunasafiri nao, wale punda walipopotea tukasema kwamba tunabaki kuwatafuta punda; na huko nyuma Kaskazini tulipotoka kuna watu ambao ngombe wao walivunjika, walivyovunjika wakasema, #sisi hatuwezi kwenda, tutabaki kumuunga huyu ngombe, akipona tutakuja.# Wakaachwa kule wakaitwa Garach mweuda ngashi. J: Sema yote. M: Garach, mweudangashi, yaani wao waliachwa kwa ajili ya ngombe wao au ndama aliyevunjika. J: Na sehemu gani waliachwa? M: Haijulikani sasa ni Kaskazini. J: Huko Kaskazini? M: Lakini hapajulikani kwamba J: Na sikku hizi kuna kikundi ambacho M: Sijui wanasema kwamba wapo, wao waliwaacha ndugu zao lakini hawajulikani hawa watu ni wapi, siyo sawa na Barabaiga au Bureriga. Hawa ni wale wanaofahamika, hawa wote hawa ni kikosi kilicho ondoka kikaenda Kusini, Bajuta ni Kusini kwa hiyo hao waliachwa hapa, wengine wakaenda Bajuta ya Kusini. Kwa hiyo hawa ndiyo wakaenda wakaachwa Barabaiga, wakaachwa Beriga, lakini walioachwa kwanza Beriga halafu kwa mara ya mwisho kule ndiyo wakaachwa Barabaiga sasa toka hapo tena hakuna tena, msafara wa Kusini ukawa umeisha. Kwa hiyo inawezekana kwamba Bureriga ndiyo walioachwa mwisho, Barabaiga ndiyo waliachwa mwisho. J: Na nyinyi muliitwa Rotigenga, ni sawa na ile jina la huyu mtemi wa Wanatta? Ge: Na jina hilo limetokea kwa sababu ya upotevu wa punda, na kila kitu ikitokea tulitamka kwamba sisi hatutasafiri tena. M: Hatusafiri tena tumepozeta punda. Ge: Sasa tukaambiwa nyinyi kama mumepoteza punda sasa nyinyi mutakuwa Rotigenga, nyinyi hapa sasa mutakuwa Rotigennga ambao munasema muta J: Hili ni jina sawa na yule mtemi au? N : Ndipo bwana. M : Lakini huyu mtu hafahamiki, hili jina ujaribu uwaulize kwamba jina lao lina maana gani kwao, labda uwaulize jina lao lina maana gani kwao? J : Lakini unavyosikia jina lake ni sawa ? M: Ni sawa hata sisi huwa tunamuita Siro Rotigenga lakini haijuilikani yeye alilipata wapi jina hilo lakini kwa kwetu sisi lina maana. J: Kwa hiyo nyinyi pamoja Barabaigi, pamoja na Burega wote ni Rotigenga? M: Wote ni Watoga, wote ni Watatoga. N: Wa Mara ni Rotigenga. J: Kwa hiyo wao Burega? N: Bureriga wako sehemu gani? M: Wako kuanzia sehemu hizi za Meatu, kuanzia Meatu kwenda kwenda Kusini mpaka Igunga tunakwenda mpaka Manyoni. J: Huko sehemu za Singida, lakini wao kuwaacha nyinyi ni hapa hapa Mara. M: Hee wao walituwacha hapa sisi ndiyo kikundi cha wa kwanza kuaachwa Tanzania nafikiri. J: Na hata wa Barabaiga waliwaacha hapa hapa. G: Wote walikuwa pamoja. M: Walikuwa bado walikuwa ni kundi moja. J: Kwa hawa wanao sema nyinyi mumetoka Mbulu kwa wa Barabaiga. G: Hawa sasa unajua kusema hivi sasa si tuko hapa mwingine kutoka huko anakuja hapa kuamkia hapa anapenda hapa ana owa hapa, sisi ni watu wa hapa wa zamani na sisi mtu anatoka hapa kwenda huko anakwenda kwa watu wao kama anapenda huko anakaa anaowa. Ge: Mababu na mababu wamezaliwa hapa. J: Na kuna uhusiano bado na hawa vikundi vinginge? M: Wapo, uhusiano upo, uhusiano upo mkubwa tu ni kwamba watu wanaweza wanakwenda, mtu anaweza akatoka hapa akaenda akaishi kule, akatoka kule akaja akaishi hapa bado kuna watu wana ndugu zao kabisa. J: Kwa mfano, wewe umeisha fanya ugeni huko? G: Bado kwenda. J: Bado au huko Kusini umisha fanya ugeni? G: Bado. M: Tangu amezaliwa hajaenda huko. Ge: Nafikiri hata baba yake hakwenda huko. G: [KITATURU] Baba alikuwa anakwenda. J: Kuna historia jinsi, maana nilisikia kwamba nyinyi mkoa wa Mara Warutiginga nyinyi mumeisha gawana kwa sehemu sehemu; hii imetokeaje na ni sehemu gani wamegawanyika gawanyika? G: Kwa hapa sisi kugawanyika gawanyika kujenga. J: Au kwa maana wengine wameenda huko sehemu za Mara, wengine huko sehemu za Bunda, wengine sijui kwa, na sijui ni wapi lakini nilisikia kwamba kuna mugao kwa watu. M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema hakuna mgawanyiko, ila tu ni kwamba kulikuwa na baadhi ya koo, kuna ukoo mwingine ambao amewataja kwamba waliwahi kuishi sehemu za ziwani Majita Majita kunaitwa Marembo; lakini anasema hawa watu sasa hivi hawapo, nafikiri wengine walihamia huku kama wapo waliobakia huko lakini hawajulikani kama wapo. J: Hawakurudi tena hapa? M: Hawa walirudi lakini sasa kama kuna mtu mmoja labda alibaki. Lakini katika kumbu kumbu zake yeye anasema hamuna, anasema kuna baadhi ya wazee ambao anasema kwamba walikuwa wanaishi, wao waliishi kule alakini. J: Na wanaitwa Amarembo? M: Hapana ni Wataturu. J: Kwa ukoo lakini? M: Ni ukoo gani? G: ########. Huko ni Majita walikuwa wanajenga tu walikuwa wanaishi, na sasa wakarudi na. J: Walikuwa wanaita sehemu ile? M: Kulikuwa na sehemu. G: Sehemu zetu Wataturu tunaitwa Barembo. J: Ni nchi au watu? M : Nafikiri ni kaendio walikokuwa wanaishi. G : Kaeneo hako ni kama ? M: Nikafikiri kama kusema, labda Mogeta au G : Na jina hili ni kama Wataturu wanataja wenyewe? M : Lakini siyo ajabu yale makabila wa kule labda hawajui. N : Na pale malembo na ni ukoo gani wa Wataturu ulikuwa pale Marembo ? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema ni kwamba Kipeshiki kwamba ni ukoo mmoja walikwenda kuishi pale. J: Ni mchanganyiko? M: Ni mchanganyiko tu. J : Au kuna muongozi fulani ambao kuna kumbu kumbu kwamba wao, yeye alikuwa anawaongoza walipokuwa huko ? M : Hakuna. G : Zamani kabisa. J: Je, sehemu za Ukelewe walikuwa wanaishi? M: [KITATURU] G: [KITATURU] J: Hawakuishi Ukelewe. N: Wasizaki, Watatoga waliishi sehemu gani? G: Watatoga, Shizaki, hapo Shizaki walikuwa kama wanachanganya changanya [KITATURU] wanachanganya changaya hapa Mihare hata sasa wako. M: Anasema wamewahi kuishi kama sehemu hizi za Wasizaki wamekaa, walishawahi wameishi mpaka Sakira, wameishi mpaka sehemu fulani wao wanaita Girimeguda, Guta, anasema wale ambao waliwahi kuishi kule wale ambao baadaye walirudi. G: Walirudi ............ Majita kule wanajenga jenga Ikizo, Ushashi, wana changanya changanya Isenye, Ikoma na Natta wanachanganya changanya. J: Na Mashariki mlikuwa mnafika mpaka wapi? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema hana kumbukumbu vizuri ya majina ya sehemu walizowahi kuishi lakini anasema, kuna baadhi ya miji ambayo ilikuwa ngambo ya mto Gurumeti, maeneo yale ya Ikoma lakini anasema miji mingi ilikuwa ni ngambo ya huku sehemu za Gwalayu nafikiri hata kwenye ramani .................... J: Hii ilikuwa mahali pakubwa ambako walikaa? M: Anasema miji mingi ndiyo ilikaa huku, ile michache michache ndiyo iliweza kuvuka kwenda ngambo ya kule ambayo hana kumbukumbu ya majina kamili ya maeneo yale sababu. J: Nakuingia kwenye sehemu za Umasaaini mulikuwa munaingia pale? G: Hapana. J: Hapana. G: [KITATURU] M: [KITATURU] Anasema katika asilimia ya ukoo wao ambayo ni Rerimwajega, katika historia yao ya Rerimwajega anasema wameishi wameishi hata maeneo haya ya Mashariki, anasema kuna mbuga kubwa kupita sehemu za Ikoma, kuna mbuga fulani kubwa sana, mbuga ya kupita Soronera, wao wanaita Gumari. J: Wanaita Gumari ni huko Nabi au bado hujafika Nabi. M: Umeishafika Nabi ile mbuga kubwa, si kuna mbuga baada ya Nabi, kuna mbuga kubwa sana. N: Ile mbuga Gumari ukitoka Nabi umepita hivi si hapa ni Nabi, unapita unaingia kwenye hii mbuga hii, mbuga imekuja hivi. M: Mbuga imekata, kuna mbuga fulani pale imekata kona hivi kuelekea Magharibi ambayo tuseme karibu eneo ndiyo endo kubwa la hifadhi ya wanyama Serengeti. N: Seronera nzima ndiyo mbuga iliyokubwa kuliko mbuga zote. M: Anasema hii ukoo wao waliishi eneo hilo, anasema vizazi vya nyuma sana ambao hata yeye anawakumbuka tu baadhi ya wazee, anasema waliwahi kuishi kule, kwa mfano anaitwa Retaru, ambaye ni mzee wa zamani sana katika. J: Na yeye aliishi pale? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Getauri alimzaa mzee mmoja anaitwa Getamuri. G: [KITATURU] M: Getauri amemzaa Gembareku. J: Gambareku M: Halafu Gambareku amemzaa Gwereguda. J: Utanisaidia baadaye na spelling Gweruga. M: Gwerenguda akamzaa Chokora. J: Chokora. M: Chokora akamzaa Ginanani ambaye ndiye huyu. J: Amemzaa? M: Ginanani. G: Ndiye huyu sasa. M: Ndiye huyo, kwa hiyo sasa hawa sasa kwa umri wake huu fikiria sasa hawa watu huyu mtu alikuwa kipindi hiki ni wangapi? Ina maana ni wa sita, katika watu kwa umri huu watu wa kwanza kizazi sita yeye ni kizazi cha sita. J: Na Getamuri alikaahuko Gumari? M: Hee. J: Na Gambareka? M: Gambareku nafikiri [KITATURU] Ge: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Wanasema hawa wengine kwa mfano Gambereku amefia maeneo ya Meatu na Wilaya ya Miatu. J: Meatu. M: Meatu mkoa wa Shinyanga. J: Na Weruta. M: Mwererugada amefia maeneo haya ya Ikoma, sijui sehemu gani lakini ni maeneo ha Ikoma. J: Na Chokora? M: Amefia Ngurimi. Ge: Uliko kuwa siku hiyo. M: Kule uliko kwenda kufanya historia sasa kwa mbele yake. J: Haa sasa kwa huko. M: Haak. J: Bado. M: Mureryo. N: Huku Ikizu. M: Ukivuka Mugeta kuna ka mbuga fulani hivi ukwa Mogeta. Ge: Kuna siku ulikuja kuandika andika maneno kwenye kilio fulani ndiyo sehemu hiyo sasa. J: Chokora ndiyo baba yako wa kukuzaa? G: [KITATURU] J: Na wakati Retaruya alikuwa anakaa Ngumari Wamaasai walikuwemo pale au hawakuwepo? M: [KITATURU] G: Sijui sasa kwa hapo kwa kweli hapana jua unajua sisi mambo yetu kama twarikuwa kama nyinyi tunaandika maneno, maneno yatakuwa sawa; na sisi maneno yetu wanakwambia neno huyu anakwambia nyingine huyu anakwambia nyingine na sasa anasema, #hapo unapotea, hapa anasema haki, hapa unapotea.# J: Ndiyo ambayo imekumbukwa tunatoa sasa ni yupi? M: Sasa anasema kwamba, wao katika historia ya Wataturu ni kwamba hawawezi kuchanganyika na Wamaasai, ni kitu ambacho hakiwezekani ila mahala wanapohamia Wataturu; kwa sababu wao muda wote wanatembea na ngombe ni lazima Masai atasogea ili awaibe wale ngombe. Lakini, wanakuwa hawakai mahala fulani hawawezi kukaa jirani, wakikaa jirani ni vita. J: Mumewahi kuishi kwa mfano sehemu za Bagwesi pale? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema katika kumbukumbu yake hajui kwamba ni sehemu gani lakini anakumbuka kuna mahala wamewahi kuishi wakashambuliwa sana na Wamaasai. Wanasema wana kumbu kumbu kwamba kuna mahali wameishi kando kando ya mto Gurumeti. Ge: Hapa karibu na Sonora yaani wao wanaita Sonora kando kando ya Sonora. Usitumie Gurumeti kwasababu tunatumia kwa sababu mbalimbali lakini wao wanaita Sonora. J: Na kati ya hawa vizazi ambao alinitajia na ni akina nani walipigana sana vita kali na Wamaasai? G: Hawa Mureguda [KITATURU] J: Nani? M: Wereguda. G: Baba ya Baba. J: Huyu mtoto wa Gambareku? N: Wanata Gitamuri ni simba dume. J: Na hawa ambao walikuja kabla yake hawakupigana sana na Wamasaai? M: Kabla yake sasa, katika kabla yake si hitoria ni kwamba watu hawa wanapigana, lakini sasa hakuna mtu ambaye ana picha kamili kwa sababu yeye anasema huyu kwa sababu ana kumbukumbu ya kwamba wakubwa waliomtangulia wamemu hadithia sana. Kwasababu hadithi zilizokuwa karibu ndiyo maana amezikariri. Ge: Na kumbu kumbu hiyo maana ya kuishika, mpaka kuinukuru sana; wao wanazingatia walikuwa wanapigania fimbo, huyu Mwalota walikuwa wanapigania fimbo, hakuna upinde. M: Hawakuwana silaha? N: Wala mkuki. Ge: Silaha zao zilikuwa ni fimbo tu. Walikuwa na uwezo mkubwa sana hawa hata upande tu wa Mazingara. M: Sijui walikuwa na Mazingara gani. Ge: Wanasema hata fimbo ilikuwa inapiga Masaai halafu mtu anakata shingo kama anapigwa na panga. Na wakiimba wimbo wao wa ushujaa moshi unatokezea kwenye fimbo. M: Mtu anainua mfimbo, moshi unatoka. G: Unajua hawa Washashi hawa wanasema Walikoma na Wanandi wanasema maneno ya kuchekeza kama wazee wakiwa na kitu yao ya nini ya nini ni kama sasa. Sijui wale wakubwa walikuwa na kitu gani, kama wanafanya maneno yako kama wanaita mmbu wanakwenda kuita mmbu huko mbali huko wanafanya mambo makubwa. M: Walikuwa na uwezo fulani sijui wa nini? J: Lakini Wanabii tu au ni wote walikuwa na uwezo huo? G: Wapo wengine. J: Haaa wengine. M: Kuna Milango ya uwezo huu, siyo Wataturu wote Milango. J: Kwa hiyo Reramejaga wapo? M: Meramajega ndiyo hao kuna Reriginajega, kuna Gaoga. J: Ni mlango wa? M: Kuna Gaoga na Reramwajega sasa huyu mzee ni Reramwajega. G: Sasa mambo hiyo leo inakuwa wajinga wote. J: Mambo inapita. Kama ninyi mumekaa hapa mkoa wa Mara tangu zamani na zamani munaweza kusema kwamba kuna mipaka ya nchi ya Watatoga wa zamani au mlikuwa hamna mipaka. G: Sisi sasa nakwambia siku ile sasa wanakuja wanasema kila watu wafanye mipaka yao watu wote Wajerumani wanakuja wana tugawanya wa zamani tuna changanya hivi. M: Wao wanasema kwamba hawakutaka kuweka mpaka kwasababu walijua mipaka utawabana na wao ni wafugaji hawataki ingia sehemu nyingine, kwa hiyo hawakutaka kujengewa mpaka wao; walitaka wabakie hivyo hivyo tu kwamba leo wanahamia mahala fulani, kesho wanahamia mahala pengine ili wasionekane kwamba wao ni wa sehemu fulani maana wakihama kutoka ile sehemu nyingine wanaweza wakazua vita kwa kule watakapohamia. Lakini wao walisema, walitaka wakae huru ile waende popote pale wanapoona kwamba hapa sehemu fulani pamekuwa pazuri kwa ajili ya mifugo yao, basi wanahamia huko. J: Na zamani ilikuwa hivyo hakuna mipaka munatembea munapotaka? M: Na ndiyo maana utakuta kwamba walihama wakaenda mpaka Majita, wakarudi wakaenda mpaka Usukumani; kama huyu, unasikia kuna watu wamefia Meatu huko, wakaenda wakarudi wakenda mpaka huko Ikoma wanatembea tu mpaka huku sehemu za mto Mara. Wanasema, kuna mahala kuna shoka mzee mmoja wa zamani aliweka shoka yake kwenye mti mmoja, mti mmoja unaitwa Sabira, aliweka shoka yake mpaka wanasema hiyo shoka ipo mpaka leo lakini sasa watu shoka hiyo hawajui hata iko wapi. N: Nilikuwa nauliza kwamba walioingia Mara, makazi yao sana yalikuwa Kusini au Kaskazini? M: Kwa Mkoa wa Mara, wao wanasema walipoingia mkoa wa Mara, wao waliishi ndiyo maana wakawa wanaachwa lakini msafara ukiwa ni kwenda Kusini. Hawa walioachwa hapa ambao ni Rotigenga, ndiyo walioaachwa wa kwanza, lakini wengine wote walienda Kusini na ndiyo maana hata katika misafara yao ya kuhama kwenda na kurudi nyendo zao zilikuwa sana sana ni Kusini wanaweza wakaenda. J: Mpaka Barageta hata kuvuka? M: Maeneo ya Barageti watu waliishi tu, hiyo walikuwa wanaishi tu, na ndiyo maana unakuta sana sana wanaenda labda Kusini Mashariki kama hizi sehemu za Majita huku, na huku Ikoma huku, lakini Kaskazini huku hawa kuishi. J: Hawakuishi? M: Wamesema meisho ni mto Mara, hawakuishi tenga ngambo ya mto Mara. J: Na katika kuhama hama kwao ni aina gani ya nchi wanapenda, ni milima, ni mbuga, ni, maana wao wanaona ni nchi ya aina gani wanapenda. M: Wao wanapenda sehemu zinazoitwa Mehugunda. J: Inaitwa nini? M: Mehuguda. J: Mehuguda na kwa Kiswahili? M: Yaani maeneo ya tambarare mbuga tuseme. N: Sijui kama mzee atakuwa na kumbu kumbu, Ushashi Washashi wametuambia wakati wanaingia Wamewakuta Wataturu; je, ni kweli na ni kwamba mlipigana nao na kama milpigana nao baada ya vita ya Washashi na nyinyi mulielekea sehemu gani? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema kuna baadhi ya koo waliokuwa wanaishi sehemu za Magharibi, maana walikuwa wanaishi kwa ukoo, ukoo. Sasa kuna sehemu baadhiya koo ambazo zilizokuwa zinaishi sehemu za Magharibi wanaitwa Korodenga. J: Wanaitwa? M: Korodenga Korodenga, sasa wale ndiyo ndiyo waliokuwa na sana sana wanaishi kwa upande wa huku ambayo kihistoria nayo hawezi kujua vizuri kwa sababu, wao wanasema ukoo wao walikuwa wako Mashariki kwa hiyo kuelewa habari za huku inakuwa ni vigumu. J: Na hawa ambao waliishi Kyegata? M: Hawa nafikiri ni hawa hawa waliotoka huku walipotoka nafikiri ndiyo maeneo yao ya kwanza kuishi kwa hiyo walipotoka wakawa wanasogea. G: [KITATURU] N: Halfu, wakati wa Wikizu wanaingia sehemu hizi, walikuta Mbilikimu Wanata wakati wanaishi, Mbilikimu walikuwa Kusini mliweza kuwapata Mbilikimu bado wapo Kusini au mlikuta wamehama? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Kipindi cha utawala wa Mwingereza J: Ni zamani sana. G: Sasa, siku Mwingereza aliingia alikuta hapa Jerumani alikuja na askari, alikuja na kabila gani maaskari? M: Wabengiji. N: Wao walitoka huko Kongo ndiyo hao Wabeligiji. M: Sasa Wabeligiji hawakuwa na maaskari wafupi wa nanihii, hawakuwa na Mbilikimu? Ge: Na Wabeligiji hao walikuwa ni watu wa Kusini. M: Maana wao wanasema walikuja na maskari wafupi. N: Alakini, Mbilikimu waliokuwa hapa? M: Ni wale waliokuwa na nchi. N: Hee ni wale waliokuwa na nchi na ndiyo walio wafukuza, sasa wakati wakoloni wanakuja, Mbilikimu walikuwa wameisha fukuzwa na watu ambao waliingia haya maeneo ,wao wakaenda zaidi wakaenda kwenye misitu ya Kongo. Kwa hiyo wa Sizaki hawakupigana na Mbilikimu, walipigana na Wataturu wakati wanaingia maeneo ya Sizaki. Wa Ikizu wakati wanaingia humu, walipigana na Mbilikimu kwa sababu wakati Wanata wanaishi hli eneo, Mbilikimu walikuwa Kusini, na walikwenda Mashariki, Magharibi. Sasa, ndiyo wakaja kukutana na Waikizu, sasa ndiyo maana nasema kama wakati munaingia je, ndicho hicho kipindi kama mliwapata? M: Labda tumuulize Mzee kwamba wao na Waikizu nani waliowahi kuishi hapa [KITATURU] G: Waikizo walitoka wapi wakaja hapa? N: Waikizo. J: Wengine Kaskazini, wengine Kusini. N: Walitoka kwa Wakurya, wengine wametoka Usukumani, wengine niw wawindaji hawa unajua nini mnaowaita nyinyi Wandorobo. Wandorobo ni watu wa zamani katika pori la Serengeti, sasa wengine ni Wandorobo maana ni wa humu humu kama tulivyo sisi Wanata. M: [KITATURU] G: Hapo kwa kweli hapana jua sawa sawa. M: Anasema kwa kweli hana kumbukumbu. J: Sasa nipe kidigo zamani sana sasa najua siku hizi munajenga nyumba kama hizo lakini sidhani kama zamani kama munahama hama kuna nyumba inafanana na hii, kwa hiyo wakati wa mababu sasa nyumba zao zinafanana na nini? G: Tunafanya ngozi ya ngombe tuna J: Muna weka kwenye nini? G: Kwenye mti unaweka una kata miti unaweka nguzo, kama sas majani hapa kwa ngozi mnalala# J: Inafanana na ya Wamasai au hapana. G: Ya wa Masaai iko namna gani? J: Si ni kama iko hivyo. M: [KITATURU] N: Wanajenga kama Riburu, si unaona Riburu wanavyojenga, sasa na wao wanajenga hivyo lakini badala ya majani wanaweka ngozi sasa inatoka juu mpaka chini. M: ###.. wanajenga nyumba kama hii ya mzunguko, lakini ni ya duara, lakini ni ngozi, yaani full suite ngozi mpaka chini, juu na chini. J: Kwa hiyo zilemit mnalaza hivi. M: Hee inakuwa hivi inasimama wima hivi lakini sasa ukuta ni ngozi imetandikwa kwa ngozi na juu imetandikwa ngozi. J: Na hii mkijenga hivyo ni kwa muda gani mpaka mnahama tena? G: Hapa sasa kama mnapenda hapa munakaa kama munaona ngombe yako hapana pata majani sawa sawa, munakwenda. J: Na mnaacha mita mnapata nyingine mnapo kwenda? M: Unachukua ni ngozi. G: Ngozi yako. J: Unachukuwa ngozi tu. N: Mnachukua Mdagani kujenga nyumba, ilichukuwa Mdagani kujengwa nyumba ya namna hiyo. G: Ya namna hiyo nadhani ni kitambo sana ni kitambo kwa hapa. M: [KITATURU] G: Hakuna muda, ni kujenga jenga hapo. J: Ukifika leo usiku unalala. G: Unalala tu. Ge: Majengo ya nyumba hizo ilikuwani sawa sawa na hema ya hizi hema zenu, munaweza kutoa tu munajenga mara moja. M: Na kuita hema ## kwa hiyo ilikuwa kama hema, kwa sababu ngozi wanatembea nazo wakihama huo ndiyo ulikuwa mzigo mkubwa, wakati wa kuhama mzigo mkubwa ulikuwa ni ngozi. J: Na nani anabeba? M: Mwanaume. Ge: Nafikiri walikuwa wanbebesha punda. J: Punda walikuwepo? Ge: Halafu na watu wanaweza wakawa wana utaalamu, wanaweza wakakunja mpaka inakuwa kama mamba tu wakubeba shingoni. J: Ni ngozi ngapi mpaka unafikisha nyumba kama hiyo? M: Sasa inategemeanana ukubwa tu wa nanihii yenyewe, maana anatengeneza kulingana ngozi aliyonayo kama inaweza kutosha nyumba. J: Na ile aina ya nyumba hii ilikuwa inaitwa? G: Geranjiga. J: Geramujiga. M: Mujiga maana yake ni ngozi, yaani nyumba ya ngozi. J: Kwa hiyo wakati wa kuhama kuna vitu vingi vya kubeba. G: Vitu ni vingi vingi, ni ##.. kukamua. END OF GINANANI CHOKORA TAPE # 80, SIDE A : BEGINNING OF GINANANI CHOKORA SIDE B: TAPE # 80. G: ####.. na sasa na upinde pinde wenu nyinyi na ile sheki. J: Vyungu? G: Vyungu ya kupikia nyama. Ge: Walikuwa hawali chakula kingine ni nyama. M: Chakula kikuu kulikuwa ni nyama na maziwa. J: Kwahiyo mlikuwa na wafinyanzi kati yenu kati yenu kwa kufinyanga vyungu? M: [KITATURU] G: Akina nani? M: Lakini sasa. G: Lakini tware tusangerini itobose. N: Kare mokere kusangerani na Bharema. G: Amare bwiki hangu, ebhere mbakerene abhato bhari bwiki ###.. tokogora hayo nibho bhare bhatagwate #### ebhere ito tore tugwate Abhaturi mbale bharatuha ebhigero mawe ####.. N: Anasema vyungu walipata kutoka kwa watu wengine. M: Wao wlikuwa na wafua vyuma. J: Wanafua vyuma hawa kufinyanga? M: Wanasema hawana kumbu kumbu. J: Kwa hiyo ni watu wengine wakina nani walipata hiyo? M: Makabila mengine tunasema makabila hayoaambayo yalikuwa hayafugi wao wanaita Abharema wakulima, wanaita Wakulima ambao siyo wao, wao wanajiita wafugaji, kwa hiyo haya makabila mengine ya kibantu wanayaita Abharima yaani wakulima. J: Abharema ni kibantu lakini kwa kiruga munawaita jumla yao. M: Inaitwa Ngatinyeni yaani maana yake wakulima. J: Wakulima kumbe, kuna uhamiaji wa majira zamani. M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Katika kumbu kumbu yake kwamba baada ya yeye, baba zake enzi ya baba yake anasema, sasa kulikuwa kumekuwepo kuhama kwa kipindi cha majira hasa ya kiangazi kwa ajili ya kufuata malisho ya mifugo. Lakini baada ya hapo mvua zikisha nyesha, wanarudi kwahiyo inaonyesha hapo sasa walikuwa wameisha anza kuwa na mahala pamanenti (pa kudumu) pa kuishi. Siyo kama kipindi cha nyumba ambacho walikuwa wanahama, wanaenda kiangazi kikitokea wanakwenda kutafuta maji halafu baadaye hawarudi wanaishi tu huko huko ###. J: Lakini zamani hawakuwa na mahali, hawakuwa na mahali maalumu ambapo wanajua hii ni mahali pa kiangazi tunakwenda, ilikuwa inategemea. N: Si huyu anasema wakisogea kama wakitoka hapa wanakwenda Rubana zamani sasa, kiangazi kingine unakuta wanatoka Rubana tena wanakwenda. M: Inategemea mahala ambapo malisho yapo wanakwenda hawajali kwamba huku ndiko tulikotoka turudi kwa sababu mvua zimenyesha, kwa kipindi cha zamani haikuwepo hiyo lakini anasema, baada ya baba zake sasa kukawa ni kwamba, wakawa na sehemu kwamba wanaacha familia; wanaacha familia watu kama wazee na watoto wanakwenda vijana sasa na wanahama na mifugo wanaenda wanachunga kule mvua zikiishanyesha, malisho yameisha patikana na huko nyumbani wanarudi. J: Kwa hiyo, kwa kipindi cha Gambareku au baada ya ambacho unanieleza? G: Tuseme hapo Kitaturu M: [KITATURU] Anasema wakati wa kuanzia kama wakina Gambareku, Mereguda, hawa anasema tayari tumekuwa na miji. Kwa kina fulani wanaishi mahali fulani sasa hii hama ya kwenda moja kwa moja ilikuwa haipo walikuwa wameisha anza kujenga miji labda tu tuulize kwamba, hii miji waliokuwa wanajenga nyumba za namna gani kwa kipindi hicho, ampa # [KITATURU]. G: [KITATURU] M: Sasa anasema hana uhakika kwamba waliishi kutoka wapi lakini walijenga nyumba ya Tembera ni nyumba ambayo ukuta wake unajengwa kwa miti, wanaweka udongo Tembera, ila anasema hajui walirithi kutoka wapi, eitha kutoka wapi. J: Mfano walitoa wapi? M: Maana walirithi kutoka kwenye makabila jirani, lakini anasema#### J: Kwa hiyo katika ile kuhama hama nyinyi hakuna mahali ambapo mnaona ni maalumu labda ni mahali ambapo kuna kaburi ya wazazi wenu? Au kuna mahali ambapo tangu zamani ukoo wanafanya mitambiko yao pale pale, nyinyi munayo kitu kama hicho ambapo mahali fulani ni kama patakatifu au hayo haipo? M: [KITATURU] G: [KITATURU] M: Anasema, wao hawana sehemu maalumu kwa labda kwa sababu ya ibada au kwamba kuna sehemu fulani labda waliishi labda #### ila anasema katika koo hizi mbili ambazo ndizo zenye ###. Kuna ukoo mmoja ambao wao asili yao ni miwa wa kutoka ziwani. J: Wanaitwa nani? G: Gaoga. M: Sasa wao Gaoga ni wa kutoka ziwani halafu wao, halafu wao na huyu mzee anasema wao ni Rerimajega kuna mlima wanauita Gijarasemu huko Mashariki. J: Gijasemu. M: Gijeshemu yaani Gijerasemu, sasa wanasema kule ndiko ardhi yao. J: Mashariki? M: Anasema kuna mlima mrefu sana Mashariki. J: Anaweza kujua iko wapi kabla hajafika Gorogoro au kupita? M: Wanasema ni maeneo haya haya ya Mashariki, anasema wao kwa sababu wanasema ukoo wao uko sehemu hizi za Bureriga [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema kuna sehemu za Mbulu ndipo walipo wao wale wazee ambao bado wanafikiri wanafuata mila za zamani. Bado wanaishi katika maeneo haya ya Mbulu, kwa hiyo wao wanahisi kwamba pengine labda wao huwa wanaenda labda kwenda kuabudu pale kwenye huo mlima lakini kwa huku, ila tu labda itokee wao wanafahamu kwamba labda babu yetu alifia mahala fulani basi anaenda pale kwa ajili ya kama kukumbuka tu kwa ajili ya kumkumbuka au basi. J: Wanafanya hivyo? M: Heee huwa wanaenda. J: Kama watu Natta wanavyoita kusengera wanafanya hivyo? M: Heee. J: Wanaenda kwenye makaburi ya Babu kwa hiyo wana kumbu kumbu watu hao wamefia wapi na wapi. M: Kama inapotokea kwamba hawajulikani wako wapi, anaenda tu labda porini tu mahala popote basi anawataja kwa majina na anatambikia pale anaondoka kama hajui kwamba wako wapi, kama hawezi kuwa na kumbukumbu, au ni mbali hawezi kufika, anakwenda mahala fulani kwa sababu ameamua kufanyia mitambiko yake, anatambikia anawataja wote kwa majina anatambikia ana. Ge: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Huyu anasema kwamba kwa maana hiyo ndiyo maana utakuta kwamba kwa mfano koo kama huu wa kwao ni ukoo wa manabii. Kwa hiyo huwa wanakwenda kwa mfano, labda watu wa makabila wana weza wakaamua au vipi, au kitu kingine kinaweza kikatoka pale wakaja kwake yeye labda kuomba neema kwake unaona sasa wanatoka wanaenda mahali wanafanya mitambiko. J: Manabii. M: Hee yaani manabii hawa hawa aliye nabii aliyefatwa labda ni wale watu wake; inategemea kwamba ni jinsi gani alivyowaagiza kwamba wafanye, kwa hiyo wanamfata basi anawaelekeza wanafanya mitambiko huko porini baadaye wanarudi. J: Lakini huyu nabii lazima aende kwenye mahali mahali maalumu kufanya mtambiko yake au anaelekeza hawa watu wanaokuja kumuomba? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema, katika utaratibu wa kwa mfano amemfata yeye nabii sasa, wanatoka huwa hawakai hapa nyumbani kufanyia maongezi yao, wale watu wanaenda wanaweza wakatoka wakaenda kwenye mti juu kama pale ambapo ni mbali kidogo na nyumbani. Basi wanakwenda wanakaa chini, sasa wanaongea wana labda wanamuuliza maswali au labda wanamweleza shida yao na nini, sasa katika yale maongezi kutafuta yale maongezi yao sasa wao wanaongea pale halafu baadaye ndiyo wanaomba pale pale wote wakiwa wote pamoja baadaye wanarudi nyumbani basi wanachukuwa vitu vyao wanaondoka. J: Ameisha waelekeza? M: Heee. G: Wanaomba na Mungu wanakuja kama bado wakauja kwambu kwasababu wenda sawa sawa wapate kile wanataka, wapate hapa kwangu wewe wanafanya mitambiko yao kama ya kuni ya zamani basi tunaomba omba na Mungu. J: Sawa sawa, unaweza kunipa orodha ya saa nabii wa kwanza ambaye na anayemfata, na anayemfata na naye mfata mpaka unafika sasa, nabii wa kwanza katika Reramajega alikuwa nani? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema mtu wa kwanza katika Rerimajega anaitwa Gumbanyenye. J: Gumbanyenye. M: Gumbanyenye ndiye wa kwanza J: Anayemfata? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema anafahamu kwamba huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza sasa baada ya hapo hafahamu kwamba ni nani baadaye aliyefuata, aliyefuata kwa sababu kadri alivyotokea huyu wa kwanza sasa alipozaa tu watu wakaanza kugawanyika, kukawepo na nyumba fulani na milango sasa mpaka imekuwa na milango tofauti lakini koo ni hii moja, lakini milango inaenda inaachana. J: Lakini kwa kawaida, kuna nabii mmoja kwa Reramajenga wote au wanabii ni wengi? M: Ni wengi yaaniwote tuseme, wote ni wanabii. J: Wote ni manabii. M: Wote ni manabii katika Reramajega. J: Wanawake na wanaume? M: Wanawake wanaweza wakatokea huwa nimara chache kwa wanawake, lakini huwa wanatokea lakini kwa wanaume huwa wanajulikana kwamba ni wote ila sasa huwa inatokea fulani anakuwa na mtabiri au ni mtu ambaye anayeona mengi au matukio mengi kwa hiyo anakuwa anafahamika sana lakini wote wanakuwa manabii. J: Maana nilitaka ile mfululizo nilifikiri labda mutanisahihisha, nilifikiri maana katika kumbukumbu za wazee hakuna miaka ambaye imesema kwenye mwaka fulani nilifikiri watu wanasema kwenye nabii huyu fulani hiki kimetokea au kwenye nabii hiki kimetokea au amehesabu wakati kwa kufatana na nabii. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema hana kumbukumbu nzuri ya kuweza kukumbuka kwamba labda ya fulani akaja fulani, akaja fulani au akaja fulani, na kwa utaratibu ni kwamba wote wanakuwa ni manabii sasa wanaweza mmoja yuko labda kwa mfano kama mmoja yuko Isenye, mwingine yuko hapa, unaona sasa si rahisi kuelewa kwa kipindi hicho ni nani alikuwa nabii wote, kwa sababu ni nahihii, anasema ila kipindi ambacho ##### hata kwa siku za karibuni kunammona alikuwa anaitwa Kichagucha, ambaye ni wa karibuni tu hapa. Sasa, anasema mmoja huyo, unajua hawa kwasababu hao ni watu wa Mashariki, anasema kuna Mashariki kule kuna mkubwa wao [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Kitangida, Kitangida anasema yeye yuko ####.. wakati huo yeye ndiye alikuwa nabii mkubwa###### J: Au labda nyinyi ni kama hao Wanata ambao wanahesabu wakati kwa kufatana na Sega. Wanasema Sega fulani walikuwa wanatawala wakati hii imetokea, au sega fulani walikuwepo wakati hii imetokea, nyinyi munahesabu wakati hivyo? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. N: Tatiro Inywebose monyi na Sega. G: Sega #### J: Kwa mfano Sega yao. G: Sega yangu mimi Mwalisuhura. J: Mwali. M: Mwalilisuhura. J: Na sega ya Baba ambao walikuzaa? G: Nyanzega. J: Na nani aliwazaa Nyazaga? G: Babu yangu, [KITATURU]. M: [KITATURU]. Ge: [KITATURU]. M: Inaitwa Meranyega, hawa ndiyo waliopigana sana kwa mafimbo. J: Na nani aliwazaa Maranyita? G: [KITATURU], kwa kweli siwezi kukumbuka. M: Ila ukitoka Nyanzega kuna nanihii moja, kuna Sega moja iko hapa kati kati, ni rika moja ambayo iko kati kati hapo kabla haujafika ##.. wanaita Gerinda. J: Gerinda. G: Ni kama sisi tunafata sisi Garinda. J: Wanafata nyinyi. N: Ambao hawa wanafata. J: Na kwa mfano watoto wako ambao ni Sega. M: Sasa kuna wengine ambao wanafata hawa J: Ambao ni? M: Unajua ni kwamba Chambani. N: Ambao ni saizi moja na mzee ##### Chambani. M: Halafu baada ya Chambani ndiyo wanakuja Gerirenda, sasa ndiyo hawa. Ge: Sasa ni sisi. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Halafu baada ya hapo wanakuja Mesawita, baada ya Mesawita ndiyo wanakuja hawa ambao wako kwenye nanihii sasa hivi ambao Rurendura. J: Rurendura. M: Ndiyo vijana wa sasa hivi ndiyo walioko kwe Sega. Ge: Ndiyo sasa wameshikilia ukanda sasa hivi. M: Ambao ni vijana wa hawa wazee. G: Tumeishakuwa wazee sasa hivi. J: Mmeisha staafu. G: [KITATURU]###.. J: Kidogo tu sasa mzee kuna swali nyingine ambayo ungenijibu vizuri ili ni siandike uwongo kwenye kitabu changu. Sasa hawa wenzenu wa hapa hawa Abharema wanasema G: Abharema J: Wao wanasema Waikizu, Wanatta, Waikoma wanasema, wakati Wajerumani wanaingia nyinyi mlikuwa hampo, mulikuwa mumeenda huko sijui wapi na mulikuja mulipokuja kuingia tena, mulikuja pole pole lakini mlikuwa mumeenda sijui wapi na hii kuna kipindi karibu wote mlikuwa mumekwenda Kusin,i wakati ulisema nani alikuwa amefia huko? M: Alikuwa amefia Meatu. G: Gambaraku. J: Sasa ilikuwaje kwamba wengi wameenda huko, nipe historia ile ya kwenda Kusini. M: Kusini ni. J: Hamkwenda huko Kusini? M: [KITATURU]. Ge: [KITATURU]. M: Sasa anasema hivi, kwa kweli anavyofahamu yeye anasema na nabii mmoja alikuwa anaitwa Kichabo, anasema Kichapo alikuwa ni mtu aliye wahamisha watu kuwapeleka Kusini. Sasa anasema kwamba, aliwaondoa watu hapa kila walipokuwa wanafika watu wanakataa kwenda, wakigoma anakwenda anawazushia eitha vita, makabila na kabila jingine; maadaui hata Wamaasai anawazulia vita wanapigana watu wanapigana, watu wanakufa, basi watu wanakubali kuondoka. Kwa hiyo akawahamisha katika nanihii na anasema ukiangalia inawezekana kwamba ni kweli kwa sababu anasema, ukiangalia katika hii vita ya Gerinda, katika rika ya Gerinda, wengi wamezaliwa Kusini kwa Wasukuma, anasema Gerinda wengi wamezaliwa Kusini kwa Wasukuma; baada ya hapo sasa ndiyo watu tena wameamua tena kurudi, anasema hawa walizaliwa wakati wamefikia maeneo hayo, hawa Gerinda karibu rika hiyo walizaliwa Usukumani baada ya hapo ndiyo sasa wakaamua tena kurudi. J: Kwa hiyo walikaa huko kwa miaka mingi? M: Nafikiri walikaa kwa muda mrefu. J: Hata watoto wanaweza wakazaliwa wanakufa pale. M: Hapana, hapana, kwa mfano mimi nafikiri kuwa mfano ukoo wa kwetu wao wanasema hawakuenda kwa mfano Tabora, nafikiri juzi Merekwa alisema wao hawakwenda mpaka kule Tabora, waliokwenda huko wao walikwamia hapa Usukumani, kwa mfano Baba yangu mimi alizaliwa tu maeneo hayo pamoja na Shangazi yangu lakini sasa huku walihamia wakiwa vijana walizaliwa maeneo hayo. Ndiyo maana mimi Baba ana jina la Kisukuma, anaitwa Mayonga. J: Ni sehemu gani ya Usukuma? M: Sasa sijui, siwezi kuelewa kwa kweli kwa mimi binafsi siwezi kujua, sijui kama labda #### J: Sawa na ambao walikwenda ilikuwa ukoo mmoja tu? M: Hapana, walihama wote. J: Wote, hawakubaki hata wengine hawakubaki hapa? M: Hapana. J: Sasa, kuna kipindi ambacho Wataturu waliipata maradhi ya ngombe au njaa ambyo iliwafanya wawe masikini kabisa, kipindi kilikuwepo au hapana? M: [KITATURU]. G: [KITATURU] Sasa hapana jua ilikuwa kama Sega gani. M: Anasema hiyo hakumbuki. J: Inaweza kuwa wakati wa Baba yako? G: Baba yangu? J: Kabla ya wewe lakini. M: Anasema, ni kwamba yake yeye, ila anasema sasa hajui ni rika aliyofuata ambayo Gerinda au Nyanzega hakumbuki, lakini anasema hiyo lakini, anasema tatizo kubwa lililokuwa linawafanya hawa watu wanakosa mali ni vita vya Wamaasai tu. Vita vya Wamaasai ndivyo vilikuwa vinaweza kuwafanya maana walikuwa wa kupigana wakishindwa wananyanganywa tena. J: Kwa hiyo si maradhi wala njaa ambayo iliwafanya M: Hapana, sasa njaa inatokea kwa sababu hawa watu hawalimi, hawakuwa wanalima wao walikuwa na vingombe. Sasa inapotokea ngombe karibu wote wameisha chukuliwa, basi inabidi waishi kama masikini, sasa wana tanga tanga. G: Sasa kwenda hapo kufanya nini, sasa wazee wengi mmoja anakwenda kwa wale##### Wasukuma, wengine wanaishia huko na sasa unakuta Watatiro kwa hapo Wikizo na hapa ninihii Wasukuma wengi wanasema, #mimi niko na Mashetani ya Wataturu, Mashetani #. Sijui anataka Mkuki wa Watatiro,# sasa kumbe ni watu wale walikuwa siku ile. M: Kinachofanya hawa watu wanasema mimi labda ninataka mitambiko ya Kitaturu labda wameniambia Mganga ameniambia kwamba, #nataka mitambiko ya Kitaturu# anasema hiyo ilikuwa inatokana na kwamba hawa watu inaonekana haa watu inaonekana baada ya vita hizo kuna baadhi ya watu walikuwa wanakimbia, wanaingia kwenye makabila mengine wanaenda wanaishi huko kwa hiyo wanatokomea huko na mila zao zote zinaishia huko huko. Kwa hiyo, wanakuwa hawafahamiki tena maana wale watoto kwa mfano ni mtu mmoja na mke wake, sasa wale watoto wakikuwa, baba yao akisha fariki hawawezi kujua tena kwamba walitokea wapi. Je, sasa ndiy hawa wanazaa hawa ambao wanasema mimi ni Mashetani yangu au wananiambia kwamba nina asili ya Wataturu, nataka hiki, nataka munitengenezee J: Na ni kipindi gani ambacho hii imetokea, kwamba hii imetokea kwamba wameishi kwenye makabila mengine? G: Sasa kwa hapa unajua Wamaasai hawa kila Sega wanakuja wa zamani, kila Sega hapana kusema na Sega fulani alikuwa zamani kule. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema kabla ya labda kabla ya utawala huu wa watu weupe kuingia, wanasema zamani ilikuwa ni kwamba kila rika lazima ipigane vita kuuwa Wamaasai. J: Kwa hiyo hakuna kipindi kimoja tu ambacho umasikini umeingia kwa wengi. M: Hamna yaani anasema. J: Ni baadhi ya watu? M: Ni baadhi ya watu. J: Maana Waikoma wanasema kuna kipindi Watatiro wengi walikuwa kama wanakuja kuchunga ili wao wapate mifugo michache waende maana walikuwa wamefirisika kabisa, kwa hiyo inawezekana inawezekana kwa sababu maana vita vilikuwa vinapiganwa, sasa inawezekana labda kwa kipindi wanachosema hawa Waikoma inawezekana labda kwamba watu kweli walifirisiwa, yaani walipigana ile vita wakanyanganywa ile mali waliyokuwa nayo yote. Kwa hiyo ili waishi labda ndiyo maana wakaenda kuhemea kwenye miji kama hawa Waikoma walikuwa nayo inawezekana. J: Lakini si wote, hakuna kipindi ambyo ni karibu ni wote wame, M: Hamuna, kwa sababu wanasema walikuwa wamegawanyika kwa hiyo inawezekana labda ni hawa wa Mashariki ndiyo walio firisika, lakini hawa waliokuwa Magharibi wakawa wana mifugo yao wenyewe. J: Na mulipo rudi kutoka Usukumani mlikuja na mifugo wengi sana, mmetajirika huko? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema hiyo hana kumbu kumbu, kama walikuja #####. Sasa na hiyo nafikiri inategemea sasana kukoo labda ukoo mmoja ulikuja na mali nyingi sana labda ulikuwa hamna. J: Lakini kipindi mulipokwenda Sukuma hii sehemu ambazo mumeenda, hapakuwa mahali penu pa asili, palikuwa mahali papya kwa Wataturu au hata zamani walikuwa wanaenda huko? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema huko hana kumbu kumbu nzukri kwamba labda ilikuwa ni makazi ya asili au n kwa sababu ya vita tu ndiyo wakahamia kule. Lakini anachojua yeye ni kwamba anasema hawa watu Watatoga walikuwa ni wengi sana, ila kitu kilichokuwa kinawamaliza ni vita, maana walikuwa wanapigana vita na kila kwa sababu vita ilikuwa ni ya kila rika, sasa kila rika lazima ipigane, na ni lazima wafe. Na wanao kufa huwa ni vijana, kwa hiyo wanaobaki ndiyo wanaendelea lakini wao huwa wanakufa, anasema maeneo haya anasema yalikuwa maeneo ya kuishi kwa mfano hiyo mbuga ya Kusini ya Serengeti wanaita Orofulayi ni eneo lile la Ndabaka. Anasema Orufulayi, anasema ni mbuga ambazo walikuwa wanaishi tu. J: Na hawa Wanata na Waikoma wengine wananielezea vita ha Hantachega na nyinyi mulikuwepo kwenye ile vita au? G: Hakuwa wako. M: [KITATURU], inawezekana wakawa walikuwepo kwa sababu Hendajega ni mahali ambapo wao waliishi wanaita Hendajega, na hii. J: Hendajega. M: Hendajega ni jina la Kitaturu. J: Kwa hiyo hawa Wabantu wanapotamka wanatumia jina la Kitaturu. M: Ndiyo maana wao wanatumia Handa jega, lakini ni sisi Hendajega ni jina la Kitaturu. J: Sasa ulisema kwamba Rerimajega ni wanabii karibu wote, lakini ni nabii wa aina gani upande wa usalama upande gani? G: Unajua hii tunaomba yote hata mvua wanakuja tunaomba Mungu. J: Kwa hiyo hakuna utaalamu? Ge: Unajua shida za watu ukosefu wa mvua au kwenda kwa hawa Manabii wanashida ya njaa, wanakwenda kwa Manabii kuomba, unakuja ugonjwa fulani labda mbaya kama Surua hii, wanakwenda kwa huyu tena kwenda kusema, zuia,ni mambo mabaya yote yasiyotakiwa kuingia kwa Wanabii. J: Kila kitu, na ile ukoo mwingine ambyo ulisema wana unabii unaitwa nani? Ge: Wanaitwa Gaoga. J: Gaoga, na wao pia hawana utaalamu fulani? M: Wote unabii wa Kitaturu, unabii wa Kitaturu wote ni wa aina moja, wote unabii ni wao wanabii wenyewe wanasema wanaomba Mungu, wao wanaomba Mungu, labda ana waonyesha au anawaambia anawaonyesha kwamba, #epukeni hivi, au fanyeni hivi ili wa ajili ya usalama wa watu, au labda kwa usalama wa mifugo,# au kwa kuepuka baya lolote lile ambalo kama maradhi mabaya ili yasiikumbe ile jamii. J: Lakini, ile kujua kuzungumza na Mungu tuseme ni wakati wa usiku wa kuota ndoto, au ni hata mchana? G: Ndoto. J: Ni kwenye ndoto. G: Ndoto. J: Kwa hiyo ukoo ambao au milango tuseme ambayo wako hapo Mkoa wa Mara kwa Watatoga ni nani, na nani tumeisha pata kwa Reramajega, kwa hiyo na nani tena? M: Kuna Gaoga. J: Gaoga, halafu kuna nani? M: Kuna Jojojega. J: Ambao ni wewe au hapana, na mwingine au ni wote? M: [KITATURU]. G: Iko wengine, sasa unajua Jojojega, na Garyega, na Gaoga ni kama ### kidogo sasa wengine ni wadogo. M: Wengine niukoo zile ndogo ndogo sasa hawa ###.. J: Na hawa Waturi ni wakina nani? M: Hawa Waturi wako mbali #####. G: Unajua hawa kama sisi ni kama, unajua watu Ikizo wako Waturi, wapo Waturi wao, Watatiro wako Waturi wao wako, Wasukuma wako na Waturi wao. Sasa sijui, Mugwate Abhaturi wori na Wikoma hakuna kunaWaturi, na Wisenye hakuna Waturi, sasa hawa sasa kuna Waturi na sisi Watatiro tuna Waturi wetu hawa nanihii [KITATURU] Wasukuma kuna Waturi wao, Waturi wako sehemu; sijui Wazanaki iko iko Waturi, sasa wengine wanakuja kupata ninihii mkuki na nini hawa #####. J: Kwa hiyo wako ndani ya kila ukoo au hapana? G: Hawa. J: Kwa nyinyi Utatoga? M: Wao ni sehemu ni ukoo haijulikani kwamba ni wa ukoo gani ila wanafahamika kwamba ni Waturi wao ni Wahunzi wa vyuma. J: Kwa mfano, Rerimajega Waturi wapo? M: Nafikiri kabila zima ni hawa wananihii, ni hawa tu wa aina moja. G: Sasa tuseme hivi kama Watatiro. M: Ila tuseme ni kama ukoo mmoja. G: Sasa ukafata huu. M: Kazi hii ya. J: Na wao unawaita nananii? G: Giraguru. J: Na hawa wanaoitwa Isamajega ni akina nani? G: Isamajega ni hawa ni kama wanatoka kabila yetu ####. M: Ni jamii. J: Jamii ya nani? G: Ya Watatiro. M: Sasa sawa acha Kitaturu. G: [KITATURU]. END OF GINANANI CHOKORA SIDE B: TAPE # 80. MANENO: Ginanani Chokora Tape # 80, Side A. - North donkeys lost, those who were tired Bureriga. - Fimbo Barabaig - Refused Chiefdom move around, German time. - South of Mara River Ngoreme Mts- Maji Moto. - Robachek, Rogwacherk came here first. - Peoples whose cattle broke legs left North calves. - Bachuta, Bajuta, Machaba Ngorongoro, Gumari. BEGINNING OF GINANANI CHOKORA TAPE # 81: SIDE A. M: Anasema Isimijega inaonekana kwamba ni asili moja na Rotigenga, ni asili moja Rotigenga ila wao ilikuwa ni ####. Ambayo ilikuwa inapenda sana mambo ya porini ya uwindaji kiasi kwamba hata kuna kipindi fulani Nabii alisema kwamba tengenezeni kusanyeni mifupa muweke mujenga mazizi ya kama ya ngombe muweka mifupa; baadaye ngombe wakapatikana wakakusanya mifupa wakaweka, kwenye mazizi zikapatikana sasa lakini wao wakakataa wakasema sisi tunaenda kuwinda, sasa wakaenda kuwinda, wakati waliporudi wakakuta wenzao tayari wana ngombe. Sasa ndiyo wakawaambia sasa, ndiyo wakaawaambia sasa, #nyinyi munataka nani atawasaidia, sasa nyinyi si mulisema munakwenda kuwinda?# Lakini sasa wana ngombe sasa, kuanzia hapo ndiyo wakabadili sasa hata matamushi lugha na nini, wakawa hawawezi kuongea sasa na wao. J: Haa kweli. M: Heee. J: Wako wapi sasa, wako hapa mara. M: Wako humu humu, Mara hata Isenye hapa wengine wamemezwa hata Ushashi. J: Na munawahesabu kama ndugu. M: Heee G: Ni jamii yetu. J: Na siku hizi wana ngombe. M: Hapana, kwao asili yao kwao ngombe hamuna. Ge: Hata utamkuta mmoja ana ngombe tano lakini hawezi kuwa nyingi###. N: Na wao kazi yao ni kuvua tu. M: Wao kazi yao ni kuwinda tu, na kuvua samaki. N: Ndiyo maana wameishia Ushashi kwa ajili ya uvuvi. M: Heee kwa ajili ya uvuvi. J: Hasa wako sehemu ile ya Ushashi, wana asili yeyote na wa Ndorobo au hapana? M: Hapana [KITATURU]. G: [KITATURU]. J: Hata nyinyi hamna uhusiano na Wandorobo? G: Hamuna. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. J: Kwa hiyo unasema hata kwa lugha Isamajega wako mbali? M: Anaongea unasikia ila kuna baadhi ya mambo mengine kwa kweli anaongea yanakushinda kuelewa. J: Na mila na desturi inafanana? M: Baadhi inafanana, lakini kuna mambo mengine wao wameisha acha. J: Na nyinyi muna asili ya uvuvi au ni hawa tu lakini kuwinda munawinda au hapana? M: Kuwinda tunawinda. J: Sana au? M: Kuwinda tunawinda tu kwa sababu chakula chetu kilikuwa ni nyama, damu na maziwa ndicho chakula #### ugali tumekuja kula kwa miaka ya karibuni. J: Kwa hiyo zamani mlikuwa mnafuga pamoja na kuwinda, hata kuwinda wanyama wakubwa kama tembo, mlikuwa mnawinda? M: Tembo walikuwa wana winda kwa ajili ya ushujaa, lakini hawali tembo. J: Au kwa ajili ya kuuza pembe? M: Hapana hawakufanya biashara. M: Wao ilikuwa ni sifa tu kwamba ameua, anatamba. G: ####. Kikubwa, wanasema huyu mwanaume. M: Shujaa. J: Au kifaru walikuwa wanaimba, wanawinda. G: Kifaru kama wanaiona, wanasema ngoja niuwe hii wajue mimi ni mwanaume sana, lakini sisi hapana kula. J: Ni kama sawa na simba, au chui kuua kwa ajili ya ushujaa? M: Ushujaa tu. J: Sawa. G: Tunakula mbogo tu, mbogo hiyo ni kama ngombe. J: Na muna winda kwa upinde? M: Heee. J: Mlikuwa manatumia mikuki au? G: ############# J: Na katika vita mlikuwa namtumia mkuki? M: Katika vita. G: Kwa sasa M: Vita kwa zamani ilikuwa ni kwamba kwa mfano, ile vita ambavyo vilipigana vya zamani sana walikuwa hawatumii silaha nyingine yoyote ilikuwa ni fimbo, ila silaha ya sasa hivi ambayo ipo upinde ni kuanzia ndiyo upinde umeanza kutumika hapo. J: Hata kwa uwindaji? M: Heee hata kwa uwindaji. J: Au Ngao walikuwa wanatumia zamani. M: [KITATURU] G: Ngao ni wale. M : Wale wenye fimbo, waliopigana na Wamaasai, wale waliokuwa wanatumia fimbo ndiyo waliokuwa wanatumia ngao kwa ajili ya kujikinga na mkuki. J : Walikuwa nayo. M : Hee walikuwa nayo. J : Kwa hiyo koo zote ambazo uliniambia ninaweza nikafika huko Mbulu kwa Barabaiga nitapata Rerimajega au siwapati ? G : Utapata. J : Nitapata na Gaoga ? G: Utapata. J: Jojajega? G: Utapata. J: Wote? G: Wako. J: Na huko sehemu za Singida? G: Wako huko. J: Nitawapata wote. G: Utawapata sasa kama ukifika Mbulu huko sasa makabaila ya Wataturu utapata wengine wapo. M: Na kule ndiko wanasema kwamba, wa kule inaonekana kwamba bado kuna wazee wakubwa wenye umri mkubwa ambao wana kumbu kumbu nzuri , wanasema hawa wa huku wameshapoteza, hawa wanasema huko, lakini wa kule bado wameshikilia zile mila. J: Na wale ambao waliokuwa wanaishi Ngorongoro ni nyinyi au ni hawa ambao walikuwa wamesogea mpaka Ngorongoro. G: Hata wale wako wa kwetu hawa huigwa. M: Unajua hawa wengine si baada ya kutoka hapa walihama, sasa katika kuhama kusogea inawezekana labda waliweka makazi hapa kabla hawajaingia kwa hiyo hayo maeneo wengine walijenga wakaamua kurudi huko wengine wakaenda. J: Maana hakuna mipaka kwa hiyo. M: Hakuna mipaka. J: Wanaenda. M: Hao wanaenda tu. J: Kwa mfano Waikoma wana Machaba yao wamepata kwa huyu Mtaturu ambaye nafikiri anaitwa Machaba, sijui kwa nini. G: Heee Machaba. J: Na huyu alikuwa kutoka sehemu gani? G: Huyu, huyu sasa huyu Machaba huyu M: Ni wa Rerimwajega. G: Sasa ni wa kwetu huyu, na sasa Machaba huyu ### walikuwa wanafanyiwa na ##.. J: Rerimajega wa hapa Mara au wa huko Mbulu. G: Walikuwa wote walikuwa bado wako wote hali moja ###.. tunamwambia karibu na Wamaasai wa Ngorongoro. J: Walikuwa Ngorongoro huyu. N: Ngorongoro au hapa kwenye mbuga ya nanihii Gumari. J: Ilikuwa Gumari. M: Wanasema wote walikuwa bado wako ######. J: Na ilikuwa katika enzi ya akina nani? Ni Sega gani kwa huyu Machaba? N: Au kizazi gan kati ya vizazi #### M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. Ge: [KITATURU]. G: Kama unakwenda Mbulu huko utapata, sisi tutakudanganya ............... M: Wanasema wamepoteza, na wanasema na ukienda kule ndiyo ukienda kule ndiyo utapata. J: Lakini huyu Majaba alikuwa kabal ya Gambareku? G: Majaba nadhani Gambareku ni mdogo kwa Majaba. J: Kama Getamuri. G: Kwa Getamuri hapo kama sasa hapo. J: Getamuri? G: [KITATURU]. M: [KITATURU], anasema katika ukoo inawezekana kwamba wanasema hawa waliachania wakati wa Retauri, waliachania wakati wa Retauri na inawezekana wakati huo wa Mwajebwa., ni wakati huo wa Retauri; ila sasa anasema katika kumbu kumbu, ni kwamba miji nyumba kuna kuwa na nyumba nyumba ndogo, na nyumba kubwa. Sasa anasema, hii ya huku hawa wa Remarajega wa huku ni nyumba ndogo lakini wale wa kule ni nyumba kubwa kwa hiyo wale inawezekana wakawa labda na wamepiga hatua nyingi. Kuna vizazi vingi vilivyo ambavyo tayari vimeisha kuwepo kuliko wao walioko hapa kwa sababu wao ni nyumba ndogo ni ............. J: Kwa hiyo Rerimajega waligawana wakati wa Retauri. M: Retaruhi ndiko waliko achania wale wengine wakaenda Mashariki ambao wako sasa hivi maeneo ya Mbulu na hawa waliobakia huku. J: Na nyinyi mna historia jinsi walivyo kuja mnajua kwamba ni wakina nani walikuja kwa Majaba, ikatokea nini, maana nina historia ambayo wao wanasema labda na nyinyi mna historia nione kama ninaweza nikalinganisha. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema ni kwamba kumbu kumbu hajui kwamba ni nani alienda kwa majina lakini anasema kwamba walikuwa ni mchanganyiko walikwenda Waikoma, pamoja na Waisenye ila waligawanyika kwa mfano waliingia ule mji ulikuwa ni mkubwa nyumba fulani walikuwa Waikoma peke yao, na nyumba nyingine kulikuwa na Waishenye peke yao na siku ya kuondoka tena watu wakapewa baraka zao wakaondoka na kila watu waliondokea mbali mbali hawakuchanganyika. M: Mulisikia kwamba na Wanata walipewa pia pembe za aina fulani? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. Ge: [KITATURU]. M: Anasema ni kwamba hajui kwamba ni kabila gani walichukuwa, kulikuwa na pembe ya tembo pamoja na pembe za nyati. Lakini hajui ni nani waliochukua ile pembe ya nyati, lakini kuna watu wengine wanasema Waikoma wlichukua pembe zote lakini hizo ni mambo ya kuambiwa tu lakini siyo kuwa wana uhakika. J: Na wakati wa ukoloni kuna kipindi kuna nafikiri ni nabii wa Watatoga alikuwa mtemi wa Waikoma, hii ni kweli au haikutokea? M: Ni labda nisaidie ni kipindi cha Wajerumani, au Waingereza, au ukoloni nani? J : Nafikiri ni Wajerumani lakini sina uhakika. M : [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema alikuwepo. J: Alikuwa nani? M: Alikuwa anaitwa Kijagucha. J: Ilikuwa ni kipindi gani alisema? M: Anasema hajui ni kipindi [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema utawala wa Wajerumani. J: Na ni Waikoma wenyewe walimchagua, au ni Mjerumani alimpa au? M: [KITATURU]. G: Sasa hapo unajua hapo hapana alikuwa mtemi wa kama wa kitawala yeye wale walikuja wakakuta yeye yuko kwa utemi kama wa asili wa Unabii. J: Wakina nani? M: Wakati hawa wageni wanakuja hawa Wajerumani. J: Lakini alikuwa kama muongozi wa akina nani? M: [KITATURU]. G: Ni wote. J: Hata Waikoma, Watatoga, ni wote wanamuona kwamba yeye ni mkubwa wao? N: Mnasema alikuwa anaitwa nani? M: Kichaguja. N: Waikoma wakaita Kichagucha. J: Kwa hiyo Wajerumani walipoingia wanauliza, nani mkubwa wenu? Wakasema huyu kwa hiyo akawa ni Sultani wa Wajerumani. G: Sasa kuja kutawanya watu sasa kutawanya watu sasa yeye akakataa kuwa mtemi kama wa Serikali. J: Akakataa? G: Hee aingia kwa utemi ule [KITATURU]. M: [KITATURU]. N: Alikuwa ilikuwa ni kizazi kipi kati ya vizazi vile ulivyotutajia? J: Ambayo ulitutajia kama ilikuwa Chokura alikuwepo au akina nani? N: Ilikuwa enzi za Chokora au? G: Chokora alikuwa yuko na yule ni mkubwa. J: Mweduta. G: Gichagucha ni mkubwa yeye sasa. N: Ni mkubwa kwa Chokora? G: Kwa Chokora ni mkubwa, yeye ni kama hali moja [KITATURU]. J: Kwa hiyo ilikuwa enzi ya Mweliduta au Gambareku alikuwa ameisha fariki? Ge: Yeye tuseme ##. Yule ni mkubwa nafikiri vizazi vya kwanza vya akina#### N : Alikuwa mkubwa kwa baba yake huyu, kwa sababu Kichaguchi ukitizama Ikoma wanaweza wakawa wadogo kwa huyu wanao mfuatia huyu ndiyo wengi wakina Kichagucha. J : Wanaoitwa jina hilo ? N : Kwa hiyo waliwaita wakati yule amekufa, nafikiri alikuwa na umaarufu wake. Ndiyo maana Waikoma wakamuita hilo jina. Ge : Waliozaliwa sasa kwa huyu ni mdogo huyu. N : Haak, ni wa hapana huyu ni mkubwa kwa hawa wanaoitwa Kichagucha. J : Lakini aliwezaje kuwa mkubwa wa Ikoma na ni Mtaturu ? G : Sasa, ni kama sasa maneno hii ya kwenda kuomba maneno, tunataka kitu namna gani wanakwenda kuomba Mungu watu wanapata ndiyo hiyo tu. J : Na ni Rerimajega huyu. Ge: Unajua hawa Manabii hawa Wakitaturu katika makabila ambao tunao hawa kuja kuchanganyika nao kulikuwa na ##### ili wakipata shida waweze###### Hawa watu, kila kabila wakipata shida #### na wao hawana ubaguzi wa kusema kwamba kabila fulani amekuja kuomba kadhaa hivi ###.. hawa walikuwa na kila kabila tu. J: Lakini ilikuwaje Mungu alipogwa vipawa vya kwa# watu kwa nini kwa nini Wataturu wana kipawa kikubwa cha Unabii. G: Unasemaje? J: Maana watu wote wako hapa na wote ni watu wa Mungu sawa kwa hiyo kwa nini unabii kubwa sana uko kwa Wataturu? G: Sasa sisi ni watu wadogo wengine wanatuzaa, wale wanatuzaa sisi, huko mbele huko ni kitambo sana sasa kutokea kitambo yile ya mbele ni hii vitu inakuja hivi, huyu anakuja anafatiwa wewe ni mtu mwingine unaanza kuomba Mungu anapata tu######. Ge: Akichaguliwa huyu kila hapa Mtemi wa hawa ndugu zetu, [KITATURU] kati ya Mwingereza na Mjerumani katika uwezo wako huo alilazimika kumuuwa, sijui Wajerumani sijui Waingereza, kwa uwezo wake huyo. J: Kumuuwa huyu Kichangucha, walimuuwa? M: Aliuwawa kwa risasi na wakoloni. J: Ni Wajerumani? M: Nafikiri kati ya Wajerumani au Waingereza nafikiri ni Wajerumani. Ge: Nasikia alikuwa na uwezo hata mpaka wale watawala walikuja kutawala nchi sijui waliona ana uwezo gani wakamuuwa. G: Unajua yeye, unajua watu sisi tuko hapa sisi wote hapa fulani kama huyu, kama huyu, kama nani anasema, kawaambie wale wazungu munajua mtu huyu hata hapana weza nyinyi, ni kitu kingine huyu, huyu hapana weza huyu huyu ni kitu kingine hakuna nini yeye sisi tuna muona ni mtu tu, kama mnajaribu kumuuwa hapana weza, sasa wanafanya hivi, mgeni ule anakuja anasema ngoja nijaribu nione wakakuta hakuna kitu wanauwa, unajua tuko sisi ngozi nyeusi hawa hapana maneno ##### M: Lakini inasemekana kwamba, alikuwa anataka walimkamata, sasa katika kumkamata mwingine akajitokeza akamwambia kwamba huyo mna mkamata hata mkimpeleka hawezi kulala huko mnako mpeleka, atatoka tu mtashitukia asubuhi hayupo maana huyu ana mambo ya ajabu sana, kwa hiyo wakaona kwamba ili kumaliza tatizo lake ni kumuuwa, wakaamua kumuuwa. J: Labda ni huyu ambaye Waikoma waliniambia waliwaambia wakoloni kwamba hamuwezi kutawala kama huyu bado yupo. M: Nafikiri ndiye huyo. J: Labda ni huyu. M: Heee sasa si walimkamata ili nafikiri walimkamata ili waende kumpeleka eitha kizuizini, lakini sasa watu wakatokeza wakasema msemo wa huyu mzee, #huyu mnampekeleka mnafikiri mutamuweza huyu? Hamu muwezi.# Basi ndiyo wakaona kwamba huyu mtu inawezekana kweli ana miujiza, wakaamua kumuuwa ili waendelee kutawala. J: Kichaguja kumbe, lakini wewe unasema hawa manabii kama huyu nanapata kipawa chake kutoka kwa Mungu, lakini ni Mungu tu anamtegemea au ni kama ni labda ni Roho za watu ambao Waliisha kufa ambao wanakuja usiku kuzungumza naye? G: Sasa kwa hapo mimi na kwambia kwa hapo sasa sisi wazamani walikuwa hawa tuko na uwezo kwa nje sasa kinakuja hichi mambo yanakuwa yanabadilika yanabadilika sasa tunazaliwa sisi, na sisi leo kule. J: Hakuna nabiii ambaye anaweza kufanya mambo haya siku hizi. G: Kwa zamani kule walikuwa na uwezo. M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. Ge: [KITATURU]. G: Unajua sasa huyu ni mtoto, ndoto sasa itakuwa ina kuja sasa, ni kama wale wakubwa wake wanakuja kuwaambia maneno. J: Ni wakubwa wake? G: Ni wakubwa wake wale, unajua hiyo yalikuwa iko ya zamani. J: Hiyo ndiyo nilitaka kujua ni ya akina nani kwa hiyo ni wakubwa wake wanakuja kuzungumza naye. G: Sasa, anajua hiyo sasa hiyo ni maneno ya zamani ile hata inakuwa kitambo, na watu wa zamani unajua walikuwa wengine wa zamani kule kwa sisi kufikia walikuwa wengine kama unakuwa mgonjwa mwingine anatoroka sijui kwenda wapi, sijui mwingine anakwenda juu, sijui mwingine anafanya nini, wa zamani kwa kusikia maneno sijui ni haki sijui ni uwongo, lakini leo hakuna hilo mambo imekwisha. M: Kuna wengine ambao inasemekana kwamba hawakufa, hawakuonekana wamekufa imeonekana wametoweka tu [KITATURU]. G: [KITATURU]. J: Alikuwa anaelezea nini? M: Alikuwa anajaribu kueelezea historia ya huyu nabii anayeitwa Giriweshi, mtu mmoja anaitwa Giriweshi anasema yeye ni wa ukoo wa Gaoga, sasa anasema huyu mtu inasemekana hakufa, alitoweka tu. Anasema, alikuwa anaweka, alikuwa ameisha zaa kijana amekaliwa muda mrefu akawa amezaa kijana sasa yule kijana alipokuwa amekuwa, na yeye akawa siku hiyo anaweka ngombe alama, sas bahati mbaya akajichoma na ile nanihii ya kuwekea akasema,#haak Mungu# sasa aliposema haaa Mungu, hapo hapo sauti ikamwambia kwamba,#toka hapa duniani umeisha zaa mwingine# kwa hiyo akatoweka. Alikuwa mtu mmoja alikuwa na anangaa sana kazi ya kungaa sana. J: Na huyo alimuona? M: Hapana hakumuona, hizo ni historia tu halafu anasema katika ukoo wao kuna, au katika historia alikuwa anaelezea watu ambao hawakufa. Anasema katika ukoo wao wa Rerimwajega, anasema kuna vijana wawili sasa hawa vijana kulikuwa na mzee mmoja ambaye jina hakuniambia [KITATURU]. G: Gadirega. M: Gadirega, kuna mzee mmoja alikuwa nabii anaitwa Gadirega. Sasa alikuwa anakaa kwenye mti fulani unaitwa Sabira. Sasa pale wazee walikuwa wanakuja wanakusanyika pale wanacheza bao, lakini alikuwa anaachwa pale karibu kila siku wengine wakitoka yeye anakuwa anabaki pale lakini walikuwa na wakagundua kwamba alikuwa anawanyonyesha vijana wawili. Sasa ili siku ile wamugundue akawa alikuwa na mke wake sasa, siku hiyo wazee wakaondoka, mmoja akajiwekea madawa fulani machoni akajifanya anaumwa macho sasa wale wazee wakawa wako pale wenye kikao chao wanacheza bao, wale wengine wakaondoka sasa yeye wakati wamekaribia kuna nihii si walikuwa amefanya makusudi kwamba anataka kuwaona hawa wanao kuja kunyonya huyu mzee wakoje. Sasa akawa amejifanya tu kwamba amelala kwa hiyo wale wazee wanaondoka yeye akawa amebaki pala akajifanya amelala; wakataka kumuamusha, wakasema tumuache tu sasa na wale wale wazee wengine si walikuwa wanajua sababu yake, kwamba amekaa pale ili ajue hao wazee wana muwacha mzee huyu kila siku hapa huwa anafanya nini? Basi wale nanihii wakaondoka, wazee wakaondoka yeye akawa amebaki; sasa akawa anaangalia kwenye matundu akaona vijana wawili wanateremka wakaja yule mzee baadaye wakaondoka, basi ndiyo huyo mzee akaenda kusema sasa hiyo siri kwamba huyu mzee huwa ananyonyesha watoto wawili vijana wa kiume. Sasa inakuwaje sasa wakajaribu kumshauri yule mzee wakamwambia huyo mzee, #sasa wewe una watoto wa kiume hapa duniani, sasa hawa wanaokuja kukunyonya na hawana ujombani, sasa itakuwaje kwa sababu umewazaa wewe mwenyewe sasa watakuwaje watakuwa wanaishi je, maana hawana mama ni wewe mwenyewe?# Sasa wakasema, #tuchukuwe# akasema,#basi kama ni hivyo wachinje ngombe# wakachinja ngombe, sasa yule mke wake ndiye akachukua nyama. Ila sasa bahati mbaya akawa yule nanihii dada yake na yule mwanamke naye yuko jirani, akachukua mkono wa ngombe kwenda kama kitoweo pale nyumbani; sasa wale wanawake hawakujua sababu ya kuchinjiwa ngombe sasa. G: [KITATURU]. M: Sasa wao waliambiwa hiyo nyama ni ya kuliwa tu hapa nyumbani, lakini yule mwanamke akaona mpaka nimpe dada yangu nyama. G: [KITATURU]. M: Anasema siyo kwamba yule mama ndiye aligawa, anasema yule mama mwingine aliye kuja alikuja aka, mama yake, dada yake alikuwepo sasa akakuta kuna azunguka zunguka humo ndani akakuta kuna nyama, kwa hiyo akachukua mkono akaenda nao. Sasa kumbe ile niya ile nyama ni kwamba ile nyama iliwe halafu yule mwanamke apate mimba ya kuzaa hao watu, hao watoto mapacha. Unaona sasa siku ya kuzaliwa ikafika yule mama akapata mimba siku ya kuzaa ikafika, akauliza, akazaliwa mtoto lakini akazaliwa mmoja. Sasa, wakauliza mtoto mwingine amekwenda wapi? Sasa ndiyo yule mama akasema si alisema hii nyama siku ile dada alikuja akakuta sipo akachukuwa nyama, akachukuwa mkono, wakamwambia nenda umuite aje hapa. Ndiyo wakaenda wakamfata wakamleta akaja akakaa pale, alipozaliwa yule mtoto wale vijana wakaondoka wakaenda kuwinda. Sasa wakawa wote wameisha zaliwa kwa kipindi hicho hicho wakawa .............. G: Hapa namunangani, unaona hapo ndiyo kubwa hapo. J: Sasa naona nyinyi munajiita Waratoga, kwanini wengine wanawaita Wataturu, Watatiro, hiyo jina imetoka wapi? Ge: Unajua hii ni mbinu za makabila, mbinu za makabila kabila fulani inaonyesha vizuri kabila fulani inapinda kidogo lakini mwelekeo wao ni jina moja tu. Zingine zinapungua. J: Ni hiyo tu? M: Matamshi, kwa mfano Wasukuma wanaita Anaturi. J: Kweli? M: Abanaturu. J: Na lugha yenu munaita lugha gani, Kitatoga? G: Na wewe unasema kwa wazungu ni kabila gani? M: Yaani Muamerika. G: Amerika sasa nyinyi, na nyinyi wengine mnazuknguza kimoja? J: Amerika, tusema Amerika ni mchanganyiko wa watu wengi sana, nafikiri ni ulimwengu mzima wako huko Amerika, hakuna nchi ambayo hawajaleta watu kukaa Amerika. M: Hata wa Afrika wapo? J: Waafrika wapo wengi sana wa huko, China, Japan wako wengi sana, wa Ulaya, kila nchi ya Ulaya wako wengi sana. Kwa hiyo sote tunazungumza Kiingereza, lakini kwa asili maana watu wengi wa asili wametoka sehemu ya Swirtzerland ambao kama Kijerumani na nini. G: Kula kwanza................. N: Nasikia kuna kipindi Wasukuma walikuja kuchungia Wataturu na kipindi hicho wazee wengi wenye miji wa Kitaturu waliuwawa, hawa Wataturu walitumia lakiniwake zao walikuwa wanauwa Wataturu halafu baadaye Wataturu nao wakaanza kuuwa wale wachungaji wa wanaochunga kwenye miji yao sasa usemi hiyo kama ni ya kweli je ni kipindi kipi ambacho Wataturu na Wasukuma walikuwa. M: Sijui mimi mwenyewe, binafsi sijui lakini kwa historia na mila ya Kitaturu kuwa na mtu mchungaji mbali na kijana mwenye mji au mbali na mwenye mali mwenyewe, sijui kama ilikuwa ni kitu ambacho inawezekana, ila kuajiri kwa wafugaji inatokana ............. labda tu, na watu na watu waliokuwa wana wanalowea kwenye miji kama kuna, kwa mfano hawa manabii kulikuwa kuna watu ambao wanaweza wakaenda kwenye ule mji wakakaa tu kwa sababu hakuna kazi watu wamekaa wanakula wanaishi tu, hawaulizi kwamba ni nini, wanahesabu ni mtu anakuwa ni mwenyeji [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Sasa mzee anasema, yeye katika kumbu kumbu zake ni kwamba hakuna kitu cha namna hiyo, ila anachojua ni kwamba ilitokea kipindi cha vijana wa rika ya Chambani, Chambani ndiyo walio anza hii tabia ya kuuwa uwa watu, hata ambao wanakaa nao lakini anasema asili yake haikutokana na labda na kabila hii anasema kulikuwa na kazi ya vijana ambao walitokea katika Wataturu walioko Mashariki walikuja sasa walipokuja wakaja na hii tabia ya kuuwa uwa watu. Wanauwa halafu wanakata mkono wanakwenda kutamba kwa mabinti, #tume uwa# kama jambo la sifa. Sasa kwa sababu ni ujana, ikaenea katika rika hiyo, kwamba wengi wanafanya kitendo cha namna hiyo lakini hakuna asili yoyote labda ya kutokuelewana kati ya kabila moja na nyingine. J: Na ni hawa hawa ambao walio uwa sana wake wa Wasukuma? M: [KITATURU]. G: [KITATURU]. M: Anasema kuoa kwa makabila hasa Wasukuma ilikuwa inatokana na kuwa na idadi ya watu hata mabinti katika kabila la Wataturu, Watatoga kuwa wachache. Anasema walikuwa wanaweza kumbisha binti mmoja hata watu wengi hata ishirini wa

Show Full Transcript Download Transcript PDF

Related Items (Vitu vinavyohusiana)