Interview with Mariko Romara Kisigiro in Burunga

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.
Photograph of Mariko Romara Kisigiro
Photograph of Mariko Romara Kisigiro
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00
00:00

Title

Interview with Mariko Romara Kisigiro in Burunga

Creator

Mariko Romara Kisigiro, Mayani Magotto, Jan Bender Shetler

Contributor

Nyangere Esther Faini Magoto (transcriber), Rose Wang'ombe Mtoka (transcriber)

Description

Mariko Romara Kisigiro is a knowledgeable elder who served in various political roles in his youth. His interview was especially memorable for its description of the famine when people went to Sukuma to find food and the war of Ndabaka at Hantachega with the Maasai. Trade relations with Sukuma were strengthened when Nata went there during the famine. Other subjects include his own personal history, Nata origins and relations to Sonjo, ethnic group boundaries and prophets, age and generation sets, clans and the rituals of those groups. He also narrates the famines, outbreak of disease and chiefs of the colonial period.

Language
Nata
Swahili
Ethnicity
Nata
Sex

Male

Birthdate

1922

Date Original

31 March 1995

City

Burunga

District
Serengeti
Region
Mara
Country

Tanzania

Theme
Democracy and Diversity
Environment and Climate Change
Gender and Livelihoods
Linguistic and Cultural Patterns
Subject
Age and Generation
Disease
Famine
Leaders
Livelihoods
Neighbors
Origins
Place Names
Relations with others
Ritual
Territory
Original Format
Interview
Digital Format

audio/mp3

Source

Jan Bender Shetler Collection, Goshen College

Publisher

Goshen College

Rights Management

Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International (CC BY-NC-SA 4.0)

Contributing Institution

Jan Bender Shetler; Goshen College; Matrix: Center for Digital Humanities and Social Sciences at Michigan State University

Biography

Mariko Romara Kisigiro is from the Momoriho clan. He is an Msaye, from the lineage (ekihita) Bene Omugabo. He was born at Bigo in 1922 and went to school at Mwisenge in 1935. He finished grade 5 and then in 1942 joined the King's African Rifles. He fought in Kenya and in East Africa during WWII. In 1946, he left the army and came back home to Bigo, while his father was still alive. In 1959, his father died. He had already married but was later divorced. In 1963 or 1964 he moved to Nyichoka because there was good soil there, good harvests, and water nearby. He had other relatives that he moved nearby, and his mother died there. In 1974, with villagization, he moved to Burunga, but he did not want to and still regrets leaving those great fields in Nyichoka during Operation Vijijini. In 1952, he began involvement in politics. He was the first Diwani on the Chief's Council. In 1958, he joined TANU as Chairman of the local branch, which was then the Chiefdom of Nata. In 1963, when he moved to Nyichoka, he left all his political posts. He served on various committees in Nyichoka and Burunga. He did not complete the eldership titles (nyangi) except some of the first. Most of the history he knows he learned from his father and other elders. They would get together and sit and chat under the tree outside and discuss all manner of things and he would sit and listen.

Transcript

I11 Mariko Romara Kisigiro, Burunga, 31 March 1995, (Nata). In Swahili and Nata. Interviewed by Jan Bender Shetler and Mayani Magotto. Transcribed by Nyangere Esther Faini Magoto and Rose Wang'ombe Mtoka. [tape # 15, side A] [The first part of the tape is his life history and is summarized above.] Jan: Mwanzo wa Wanatta ulikuwaje? Romara: Abanatta asimoko yabho.... baba Nyamunywa aikuwa mwindaji... huyu mwindaji katika pitapita kwake porini kule akampiga mnyama mshare, basi, baada ya kumpiga mnyama yule mshare akawa anafuatilie nafuata nyayo... nafuata nyayo... nafuata nyayo... akamkuta yule mnyama ameanguka kwenye jiwe mwamba, ambao kwenye mwamba huo kuna maji. Na sasa bado hawajafanya chochote alimwona mtu mwingine anamwijie pale, yaani ni mwanamke. Huyu mwanamke alikuwa anabeba furusi mgongoni. Sasa alimkaribisha pale wakazungumza, sasa hatujui kwamba walizungumzaje, ikaonekana sasa wakafanya maskani pale kwenye mwamba yule. Bwana akachuna mnyama, wakaona maji yapo pale, baada ya kumchuna mnyama pale, alimwambia mwanamke, "ebu nipe nafasi kwanza ninywe moto." Bas, mwanamke akaenda, yule akatumia njia ya kupechecha moto, yaani ni kupekecha, moto ukatoka. Mayani: Ule mti inaitwaje? Romara: Ekingaita, na Rurendi. Baada ya kutoka moto akamwita, akaja. Sasa wakawa wanaendelea kuchoma zile nyama, wanakula. Ndipo kilikuwa chakula chao kikuu. Sasa yule mama, kumbe katika furusi zake zile alikuwa na mbegu za nafaka. Wakachukua miti wakachimbua chimbua pale jirani yao pale akapanda zile mbegu zikaota. Sasa zilipokwisha kuota mwisho zikaiva. Pale imekuwa kama maskani yao. Jan: Kwenye mwamba? Romara: Ehh, kwenye mwamba ule. Mbegu ziliota, zikaiva, wakavuna, Sasa ndio wakaanza kutengeneza chakula cha nafaka badala ya kuwa na nyama tu. Mayani: Mbegu gani hizo? Romara: Ulikuwa ulezi. Kwa Wanatta ulikuwa mbegu yao kuu, ulezi. Sasa ndiyo hivi. Na huyu Mwanamke jina lake alikuwa anaita Nyasigonko. Lakini Wanatta walikuwa wanasema uchunguzi uliojulikana sana ni kwamba ni Msonjo, kutoka nanihi Sonjo huko Loliondo. Sasa hawa ndio waliishi, walijiungana pamoja, wakazaa watoto, ndio hawa sasa ni Wanatta. Sisi tunapofanya mambo mengine mengi tunajiita, "sisi ni wa Nyamunywa na Nyasigonko." Kwa sababu wazazi wetu ni Nyamunywa na nani? na Nyasigonko. Jan: Na watoto wa Nyamunywa na Nyasigonko ni Wanatta tu au kuna makabila wengine.... Romara: Wanatta tu. Ila kwa makabila mengine ukichunguza utakuta wanao wakuu wao waliowazaa. Ndiyo. Jan: Na kuna kumbukumbu wapi walijenga na wapi walikuwa wawehama hama? Romara: Wao, mahali walipoungania kwa kihistoria ni Bwanda. Ehh... Bwanda. Tena ni jirani hapa ni nanihi Namogu. Ili mimi sikuwaji kufika kwenye jiwe hilo, ni hapa, kabla ya kufika Mugumu katika eneo, ukipita kilimo, upande huu kidogo, kuna Bwana hapo. Jan: Bado ile mwamba unaonekana? Romara: Ndiyo Jan: Sasa ni nani anaweza kujua kabisa iko wapi? Romara: Kuna mzee, mimi siwahi kufika pale, lakini tulikuwa na mzee anaouendea vizuri sana, siku hizi ni mgonjwa kitandani. Mayani: Nani? Romara: Hassani. Jan: Bwanda ni kati ya hapa na Mugumu? Romara: Ehh. Karibu hapo, shule ya sekondari, upande huu wa kilimo. Ndiyo Bwanda. Kyambalya yenyewe tu. Sasa maisha ya Wanatta kutoka hapo, hawakutoka kwenda mbali. Yalikuwa ni katika eneo hili tu, na wanahama hama humo humo tu. Kutoka hapa hii ni Natta ilikuwa mpaka kwenda kuungana na Wamaasai. Kabla ya Wazungu hawajaweka mipaka na nini. Sisi eneo yote ilikuwa ni Natta, tunaungana na Wamaasai tu. Jan: Haikuwa na mipaka maalum? Romara: Mipaka maalum, kwa mfano sisi na Waikoma ilikuwa ni Mto Grumeti. Halafu.... hasa walikuwa upande wa Mashariki tu ndio kulikuwa hakuna mipaka maalum, ila tunajua majirani zetu kulikuwa ni Wamaasai. Issenye hawakuwepo hapo wakati huo. Jan: Walikuwa wapi? Romara: Walikuwa huko... mashariki, jirani na Maasai. Jan: Na mahali pao iliitwa? Romara: Iliitwa Nyberekera. Ehh. Sehemu wanooishi sasa Waissenye ni Natta. Walishamulia kule na Wamaasai halafu wakashindwa wakakimbilia Natta, sasa walipokuja Wanatta waliwakaribisha katika eneo lao. Wakajenga. Jan: Unajua ile historia jinsi Waissenye walivyokaribishwa? Romara: Nafahamu kidogo. Waissenye asili yao walikuwa wanaishi Nyeberekera, jirani na Maasai. Na walikuwa na mganga wao ambaye ndiyo alikuwa ni kiongozi wao kwa mambo yote. Wamaasai walikuwa wanajaribu kuwapiga vita lakini hawawawezi. Basi Wamaasai waliwatafutia hira siyo wakawaibia ule uganga wake. Sasa badaye wakakata akili ya kuwanyima mvua kwa muda wa miaka mingi. Mvua haikunyesha Nyberekeraaaaa... muda. Bas, watu walikosa chakula, ikawa wanakwenda kupiga bao kwa waganga wengine wa nchi zingine. Wakipiga bao wanaambiwa, "mchawi ni yule mganga wenu yule, ndiyo mchawi, msipomwua, hamwezi mkapata vyakula." Bas, mwisho waliamua kumwua. Kamchukua, wakaenda kamweka kwenye shina la marangari, marangari ile mkubwa ile pori wa porini. Halafu wakakata yale marangari ikamwangukia. Bas, ilipomwanukia akafa. Sasa Wamaasai ndiyo wakapata nafasi kuwaingilia Waissenye sasa, wakapiga vita kweli. Sasa Waissenye ndiyo wakakimbilia katika maeneo hayo ya Natta. Jan: Lakini walikuwa adui yenu wakai ule? Au rafiki? Romara: Hapana... Walikuwa ni majirani tu... Bas, hatukuwa nao ubaya, kama ni adui tusingewakaribisha! Jan: Kwa hiyo mlikuwa na uhusiano? Romara: Uhusiano ulikuwepo tu wa ujirani. Sasa walipobanwa kule ndio kukimbilia hapo Wanatta wao ni watu wenye huruma wakawapokea. Jan: Walipowapokea wakawapa mahali wapi? Romara: Wakawapa maeneo kutokana na Saiga zenywe. Ehh. Waissenye wakajenga ile sehemu ile ya Nyagoti. Jan: Na Saiga gani walijenga pale? Romara: Saiga? Saiga wakati huu ulikuwa ni Abakihocha. Ehh Asaiga ya Abakihocha. Ya manyira hano. Nyagoti walijenga karibu wote. Kwanza baada ya kutoka Nyaberekera. Halafu walipotulia walianza kugawanyika tena katika Saiga za Wanatta sasa. Warumarancha wakafuata Warumarancha wa Natta. Halafu Wangirate wakafuata Wangirate wa Natta. Halafu Wasaye wakafuata Wasaye wa Natta. Jan: Wakajenga nao? Romaro: Wanajenga jirani, jirani sasa. Kama Wasaye wa Natta ni hawa, hawa ni Wasaye wa Issenye. Kwa mfano, ile Nagusi, ile Nyeberekera wanaoiita sasa. Hio walipewa Wasaye. Kwa sababu eneo lile la Wanatta lilikuwa la Wasaye. Halafu wakaja Wangureti kwa sababu Wangureti wakikuwa Makundusi wa Wanatta. Wakapewa ng'ambo wa Mto Rubana ile Sasakwa, .... mpaka Ng'otera. Halafu Warumarancha nao walikuwa hapa Rubana hapo karibu kwenye ili kivuko cha zamani. Bas nao walijenga Mumaruuga. Bas walijenga hivo. Ndiyo hivyo sasa imekuja imekwisha kuwa mchanganyiko, si sasa hakuna kusema Asaiga wala nini, kumechanganyikana. Jan: Na wao wanaanza kujiita Wanatta? Romara: Ah, bado ni Waissenye tu, ila wenywe hata kujenga kwao hawajengi kiSaiga, karibu wamechangyikana tu. Na hata sisi Wanatta hatujengi sasa kile kiSaiga kwa sababu ya maendeleo haya. Sasa ni kama tumechanganyikana tu. Ehh. Jan: Lakini zamani ilikuwa kama mnejenga kwa Saiga? Romara: Ehh, kwa Saiga. Eh tulikuwa na vita sisi wenyewe tunapigana pigana. Jan: Saiga ilikuwa inapigana na Saiga? Romara: Ehhh. Ilipigana na Saiga. Jan: Kuna kumbukumbu fulani kama vita fulani ambayo Saiga fulani ilipigana na Saiga nyingine? Ipo? Romara: Ipo ila mwaka sikumbuki. Bamwisho Batata aba Kinaho na Abasanduka. Abasaye na Abangirate. Kumbukumu ya mwisho ni Basaye walipigana na Bangirate. Jan: Na mapigano yao ilikuwa kweli kuua? Romara: Hapana. Walikuwa wanatandikana kwa fimbo tu. Jan: Kwa hiyo walikuwa wanapigana nini? Swahili gani iliwaleta mpaka kupigana? Romara: Wanapigana kwa sababu ya utawala. Maana ile Saiga, wale walio na uwezo zaidi ndiyo wana kuwa na utawala wa nchi. Jan: Ah, nilifikiri wanafanya kwa zamu? Kama zamu yako ipo bas, unaingia. Romara: Kwa zamu ipo, lakini sasa ukitaka kuingia, zamu yako imefika na wale waliokuwa nayo wanaikatalia, mpaka mpigane, mwashinde wale waliokuwa kwenye zamu, waondoke na nyie mtawale na nyie. Hapo walikuwa na muungano. Jan: Na kila Saiga ilijenga mahali pake? Romara: Mahali pake. Jan: Na hii ni tangu zamani au siku za karibuni wameanza kujenga kwa Saiga. Romara: Tena ninavyoelewa ni siku za karibuni. Zamani ilikuwa sipo. Walikuwa wote walijenga pamoja. Jan: Au ilikuwa kwa Hamati? Romara: AhAh. Kwa Hamati walijenga kwa Hamati zamani lakini Saiga haikuwepo kujenga kwa Saiga. Kwa Saiga yenyewe ya zamani ilikuwa ni hivi: Labda mimi ninyo vijana hawa, watatu, sasa huyo kijana wa kwanza mkubwa, ndiyo Asaiga. Pamoja na wenzake woooote katika Natta nzima ndiyo Saiga. Halafu anakuja huyu wa pili, sasa akipevuka na naye anaona, kwamba mimi nimekomaa sasa kuwa Saiga anaanza kupigana na huyu. Na wote wakiwa katika eneo moja tu. Bas, wanapigana, kama wanashindwa wanarudi na wanatulia, mpaka waweze kupata ushindi wawashinde wale wakubwa, halafu wanatawala. Sasa huyu mdogo tena naye anawafuata. Bas, hivo hivo ndiyo inakwenda. Lakini ilifikia kipindi ikawa wale wanaoshindwa kuwanyang'anya Saiga kwa sababu Saiga ile wao ni watu waliokomaa na hawa bado ni vijana wa machipukizi sasa wanabanwa katika nchi yao ile, mwisho wanakimbia. Hata wanakimbia Ngoreme kwenye Asaiga yao hiyo ya Ngoreme vile vile wanakwenda wanakaa kule kwa muda fulani kwa sababu kujimarishe ili wapate nguvu waje kupigana tena. Sasa pirika pirika hiyo iliwafanya kutengana. Sasa hii kufukuzwa ikaonekana kwamba wale waliofukuzwa wanakwenda wanajenga mahala pao. Unaona sasa. Kufukuzwa kwa kulianzia kwenye Saiga ya Wanatta.... [end of side A, tape 1, #15] Ndio ulianza kutengana sasa kujitenga. Bangirate unaowasikia ni kwa sababu wale Wangureti Asaiga ndili ikaanza kujenga pake yake. Halafu na Asaiga ya Warumarancha naye ikajenga peke yao. Na Asaiga ya Wasaye ndiye ikajenga peke yao. Sasa huyo ndiyo mwanzo wa kutengana kiSaiga hilo. Kwanza zamani walikuwa ni watoto wa mtu mmoja tu. Jan: Na zamani inawezekana kama wewe umezaliwa Msaye unaweza ukiona, mbona nienda kwao, Warumarancha, nianze Asaiga kwao, unaweza? Romara: Ilikuwa wazi. Kwa sababu ilikuwa ile Asaiga huo ni watu makundi mengi wamefuatana kwenye Saiga yenyewe, kwa kipindi kilichopita. Kuna wakubwa, na kuna wanaofuata na kuna wanaofuata sasa. Wakitinda mimba hawa -- chasiriti. Hawa wakitinda mimba wakati Saiga yao, wakati Saiga unavunjika, wanasema wameshakomaa, sasa wamevunjika, inatawala Saiga nyingine. Na hawa bado vijana wadogo, bado wanahitaji raha vilevile waendelee na michezo, maana wale Saiga hua wana michezo sana. Sasa kijana akiona mwenyewe, mwingine bado hajaoa, anaona mimi nianze kuitwa mzee na bado ni kijana na sijaoa. Acha anatoka pale anarudi huko kwenye Saiga nyingine. Jan: Sasa zile daraja, ulitaja daraja tatu, unaweza kusema majina yao. Romara: Daraja tatu, cha Siriti? Ehh. Siriti ya kwanza ilikuwa Amanyema (Abakinaho hata kwa Abasanduku, nao bakuru, ansiriti ankuru). Halafu Siriti ya pili Abaganda. Siriti ya tatu... Abakiira. Yamwisho. Jan: Hakuna daraja la nne? Romara: Hamna, ni madaraja matatu tu. Jan: Kwa hiyo ni hasa hawa wadogo wanaokimbia kwa Saiga nyingine? Hata baada ya kutahiriwa wanaweza wakaenda? Romara: Inawezekana, mtu sasa ni uamuzi wake tu. Anaweza aka... Jan: Na wale, wanaoita wengi kutahiriwa pamoja inaitwa...? Mayani: Ekigori. Jan: Kwa hiyo kila daraja ina Kigori yake au ... Kigori ni ... Romari: Kigori sasa zile daraja tatu zote zinatahiriwa, hasa utahiri hizo darja hizo mbili, Amanyema, Abaganda. Hawa ndiyo wameshakomaa watatahiriwa ekigori. Wote pamoja. Sasa ile daraja la pili uje kutahiriwa baadaye. Kwa sababu wakati ule hawa wanatahiriwa wenyewe bado wadogo. Bas wanatahiriwa nyuma sasa. Ndiyo darja ya mwisho inatahiriwa sasa ya mwisho inafunga na Saiga kabisa. Jan: Hata katika tohara wanatambua kwamba hawa ni Amanyema na hawa ni Agaganda, wanawatenga hivyo? Romara: Wanawajua... hawawatengi... ila wakiwatahiriwa wanatahirisha wote pamoja ni Kigori tu. Ila sisi wanatambua kwamba huyo kwa rika ni Manyema huyu ni Mganda. Ehhh. Jan: Kwa hiyo inaweza kuwa miaka mengi kati ya huyu Amanyema na huyu Abakina? Romara: Ehh. Ni mwaka tofauti na inakuja, nafikiri haipunguzi kwenye miaka minne au mitano. Tofauti yao. Kati ya daraja. Jan: Ulisema kuna kumbukumba wakati ambapo Saiga haikuwepo na ilikuwa ni Hamati tu? Au ulisemaje? Romara: Saiga ilikuwepo ila uliniuliza kutengana. Saiga ilikuwepo. Ilikuwepo ile Saiga kigori halafu walioondolewa. Sasa walioondolewa kwenye Saiga sasa wanaitwa Abateeniku. Walikuwa bado marika hayo matatu yapo tu. Saiga yenywe, Ekirogi na Abateeniku. Ehhh. Walioondolewa ndiyo Abateeniku. Sasa hawa ni wazee. Watoto wao bado hawajatahiriwa kwa hiyo hawatambuliwa kwamba ni vijana tena. Wakishateneka, wanao vijana watoto wao wakubwa lakini hawajatahiriwa Kigori kwa hiyo hawatambuliwi. Sasa wanatambua wale wazee waliovunjika na wanaita Abateeniku. Ehh. Unanielewa hapo? Jan: Kuna Chasaiga na kuna Amakora au Rikora. Unaweza kunitofautisha kazi ya Rikora ilikuwaje na kazi ya Saiga ... maana mtu mmoja anaweza kuwa na Rikora yake na Saiga yake. Ilikuwaje kama yote ilikuwepo? Romara: Mambo ya Rikora mimi kuisimulia huwa natatanika sana. Jan: Kwa hiyo Rikora haikuwa na nguvu sana? Romara: Rikora ilikuwa na nguvu nyakati zile lakini sasa kitu kinacho nikorofisha wakati nimeanze kuwa mimi nimekuwa kama mtu kushugulika na shughuli za kikazi kikazi. Mambo ya Rikora sikuyashiriki. Mayani: Lakini nyumba gani wewe? Romara: Mwanyachuuma. Sasa majina nayafahamu lakini shughuli zao kama ulivyoniuliza ndiyo si... Jan: Majina yao yalikuwaje? Romara: Majina yao yalikuwa yako makura mawili. Ehh. Jan: Na katika Mwanyachuuma kuna daraja nyingine? Au wote ni wanachuuma tu? Romara: Kuna Mwanyachuuma, na daraja nyingine kuna Mwanyasaye. Jan: Ndani yake hakuna... Romara: Kuna, ndiyo sijui wapi juzijuzi niliweka kumbukumu kwa ajili ya... Sasa hapo kuna majina, vile vile kuna Saiga zinazofuatana ndani ya Rikora hiyo. Mwanyachuuma hiyo. Sasa hapo ninachanganyikiwa. Sina kumbukumbu kichwani. Nilijaribu kuandika mwenye daftari kujaribu kunisaidia kwa sababu sikuwa na mazoea sana juu ya jambo hilo wala sikushiriki. Eh kwa hiyo ni vigumu sana lakini jaribu kuona kumbukumbu kwa sababu nimesahau. Sijui nimeweka wapi. Jan: Lakini wakati ulipokuwa kijana Rikora ilikuwa bado inafanya kazi? Romara: Ilifanya kazi. Jan: Hasa uliwaona wako kwenye kazi gani? Romara: Yakerera. Kazi ya kerera. Mwaka fulani wakaita dekerera mwakake? Kuna shughuli ya Rikora, Rikora ikishika madaraka, maana Makora haya yanabishana vile vile kama Saiga. Rikora linaloshika madaraka sasa ufanya sherehe ya kutembea ndani ya nchi. Wanaimba nyimbo, ndiyo (Mosi -- kutangaza sasa wenyewe wamepata utawala). Maana vyama viwili vilikuwa vina.... Jan: Na sherehe yao ya kutembea ilitwa? Romara: Kuterera. Mayani: Ebere nikono kobori Natta chasaiga ni irenge? Romara: Chasaiga? Esatu. Mayani: Bahe na bahe na bahe? Romara: Abangirete, Abarumarancha, Abasaye. Mayani: Na Chahamate ni renge? Romara: Chahamate chekwika inywe au isano? Nebugha Abamoriho, Abagikwe, Abamwancha, Abagetiga. Inywe. Jan: Unayo kumbukumbu kuhusu mwanzo wa Hamati yako? Romara: Hiyo sifahamu ilianzaje. Jan: Au wametoka wapi? Romara: Au walitoka wapi? Hiyo kumbukumbu siojui. Mayani: Ebere, mubayo bayo, muchahamate chiyo, Abamoriho neke bahita bere? Au neke bahatoora kama kigero kya korake, eh.... ikahogua bando ..... Romara: ......kifupi.... Nicho Bairegi, Abiregi abacha ng'ombe ............... Oburwe na ang'ombe... Ulezi na ng'ombe.. [this is rough translation/transcription of Mayani for the Ekinata here: Mbahirgoresero Ang'ombe: Haya ni Maneno kuhusu ng'ombe. Sisi ni Abigirege wa ng'ombe banyara yi chawi watu waliokwenda kulima, Alimenga alama ndama wanana maadume ya kondoo yakalalamika sisi Wairege yaani, Wamorihi (bitaberi). Ulezi na ng'ombe. Hwe ABiregi cha ng'ombe, baragara gi twaryo, Abano bagire amogondo, Bakaturang'ane akaso, bakabasa mori kendo, Chamaguruki chikiberi. Huwe Abirege ntohitaberi ng'ombe no oburwe.] Jan: Na ile kusema Abairegi maana yake ni nini? Romara: Ndiyo hawa Abamoriho. Jan: Maana wametoka pale au ni uhusiano tu? Romara: Ni walewale tu. Sijui ni kwa sababu eh... jina Abamoriho ni sawa na nini... unajua sisi katika mila yetu jina langu Romara lilikuwa halitumiki. Kila kipindi cha ujana kuna jingine. Nafikiri hilo nalo katika Hamati hiyo labda ni jina jingine. Kama anataka kujitambulisha mbele ya Wanatta hawezi kusema mimi ni Mmoriho. Ahah anasema mimi Mwiregi. Inaeleweka huyu ni Momoriho. Ehh. Lakujisifu lile. Jan: Anasema nini tena kujisifu? Romara: Aragamba... Batunda bayro, banyeka gagachigawe, batutu agiramo mogondo, batura makubaso ......... Mayani: Ebere, ndiyo tumare... Nawe Abagikwe nuheche kila... Romara: Niheche, babomba na Basi bahibirikere Abasi banchege ..................... Mayani: Nawe abagera Abamwancha? Romara: Abamwancha? Eh... Bare na Abagosi,..... nasubatira........... Mayani: .... Omugetiga? Romara: Omugetiga nteheche. ......... Mayani: Nasi Bagikwe? Romara: ............ Jan: Sasa nieleze kidogo jinsi watu walivyojenga zamani. Ulisema ilikuwa Saiga kwa sehemu kubwa, lakini ile Oruberi, ilikuwa akina nani walikuwa wanakaa kwenye Oruberi? Romara: Kwenye Oruberi... ilikuwa inafuata watu wanaofahamiana au wanaopendana wao wenyewe wanaishi Oroberi. Jan: Ni Hamati moja tu? Romara: Hamati moja inaweza kuwa na Roberi tofauti. Inaweza kuwa na Roberi moja au hata mbili. Jan: Lakini ndani ya Roberi moja... huwezi kupata Hamati mbili wanakaa? Romara: Haiwezikani. Jan: Au labda ni Ekehita moja inakaa ndani. Au unaweza kupata Ebehita zaidi wanakaa ndani. Romara: Ebehita wao wanakaa ndani, ebehita zaidi. Ebehita ndani inaweza kuwa Ebehita bitatu binne. Vimo ndani ya Oroberi moja tu. Jan: Sasa walivyojenga walijenga karibu sana kwa pamoja? Romara: Ilikuwa wanajenga karibu kama tunavyoishi sasa vijijini humu. Kwa sababu nyakati hizo kulikuwa nyakati za hatari za vita za makabila. Sasa kama kabila inakuja kutushambulia unakuta tuko pamoja tunashirikiana. Eh. Jan: Na mlikuwa mnafanya nini kujikinga? Romara: Kujikinga? Kama kwetu hapa niliona kwanza mkitaka kujilinda wanajenga kuna sehemu nyingine zina vichaka vikubwa. Vita zenyewe zilikuwa zaidi ni za usiku. Kwa ajili, kama sisi maadui wetu alikuwa hawa Wamaasai, kuja kunyang'anya ng'ombe. Sasa wanatushambulia usiku, sasa walikuwa wanatafuta mahali ambapo kuna chaka ... kubwa, ndio wanajenga kando yaaaaake, bas, halafu wanaweka ua, wanazingira ruberi roooote. Eh ua. Jan: Ua ya nini sasa? Romara: Ua ya miti. Jan: Inayopandwa au hiyo ya kukatakata? Romara: Inawezekana ya kupandwa au ya kukatwa wanakuja na wanaegesha. Ehh. Ilikuwa nzito sana na kubwa, ehh. Halafu wanafanya na mlango mmoja. Sasa kama kutatokea hatari vijana wanapigana pale kwenye lango. Halafu watu wengine wote,wazee na watoto na akina mama, wanaingia ndani ya hiyo chaka. Bas, wanakuwa pale pale na vijana wanawalinda, wasijawakuingilia tena. Ilikuwa hiyo namna moja wa kujilinda. Jan: Na ng'ombe waliweka wapi? Romara: Ng'ombe si waliweka humu humu ndani ya ua. Jan: Kwa hiyo ni akina nani waliangalia ua imejengwa safi? Romara: Hiyo ilikuwa ni kazi ya vijana sasa. Vijana wa Oruberi. Sasa viongozi wao, si walikuwa wazee. Kama wazee wanaona hapo bado hapajawa tayari wanawashauri kwamba, hapa hapajawa imara. Hiyo ilikuwa ushirikiano wa vijana na wazee. Jan: Lakini hukusikia kwamba walikuwa na ngome au mahali walijenga kukimbia, ni chaka tu? Romara: Hapo kuna chaka. Halafu kulikuwa na mahali pengine kama hakuna chaka, wanajenga nyumba nyingine... tunaita tembera. Nyumba inayojengwa kwa miti mizito halafu inakandikwa, juu inafunikwa na udongo. Jan: Na hii inaweza kuwa moja kwa Oberi moja? Romara: Ehh. Kwa Oruberi moja. Jan: Na ni ndani? Romara: Eh ndani ya Oruberi. Kama adui wanakuja wooote wasio na uwezo wa kupigana wanaingizwa mle. Sasa wanabaki ni vijana tu kupigana nje. Kama watashindwa na maadui wanaingia, basi wanakuta watu wote wengine wamefanya nini? ... wameingia ndani ya ile nyumba. Jan: Na kulima walilima wapi? Romara: Kulima walilima katika eneo lililo jirani nao tu. Jan: Ilikuwa inaitwaje? ...ile sehemu ya kulima. Romara: Sehemu ya kulima ilikuwa inaitwa Ahumbu. Kwa mfano sisi tumejenga hapa sasa tunaondoka tunaenda pale ng'ambo kulima. Tena tunaenda kulima pamoja. Wote mashamba yetu yalikuwa karibu karibu. Kwa ajili ya hifadhi kwa ajili ya wanyama waharibifu. Bas, sasa hapo panaitwa Ahumbu. Jan: Na hii pia ilikuwa na ua wake? Romara: Ehh.. ilikuwa na ua wake. Bado mjenge ua wa kuunganisha wote mashamba yote yatakuwa ndani. Ehh. Jan: Na Oruberi moja wana Ahumbu moja? Romara: Na Ahumbu ni moja. Jan: Ni mbali au ni karibu. Romara: Sasa inategemea na mahali mlipochagua. Eh. Iwe mbali au iwe karibu. Lakini walikuwa wanaenda mbali hata ... unaona mlima huu? ... walikuwa wanaenda kulima. Jan: Na wanalala pale? Romara: Ikifika wakati wa vyakula vimechanua, wanafanya nyumba pale wanalala. Jan: Hii nyumba ilikuwa inaitwaje? Romara: Ekiburu. Jan: Na sehemu ya kulisha ng'ombe ilikuwa wapi? Romara: Sehemu ya kulisha ng'ombe naye ilikuwa mahala pake. Jan: Na hii ilikuwa inaitwa? Romara: Ekerisho. Jan: Lakini kama ahumbo ni pale, ekerisho inaweza kuwa katikati hapo? Romara: Eh.. Ekirisho wakati ule hatuweki mbali, ili tunatafuta nafasi ambayo haina mashamba tu. Ndiyo ekerisho. Eh. Jan: Inawezekana mwaka moja ni huku na mwaka mwingine inahama? Romara: Eh. Maana kilimo tulikuwa tunahama hama. Wakati huo. Jan: Na Oruberi walikuwa wanaweza kuhamisha Oruberi? Romara: Oruberi kuhama labda ni matatizo fulani imepatikana sasa ndiyo wanahama pale kwenda mahali pengine. Jan: Kwa mfano nini inaweza kutokea, ambacho inawasababisha wahame? Romara: Kwa mfano tumesema kuna maadui wanaowashambulia au kuna maradhi yameingia katika sehemu ile yameua watu, watu wanaona labda hapa ni pabaya wanaona tuhamie mahali fulani. Au njaa inasababisha nao vile vile kuhama. Hatupati chakula labda tuenda sehemu fulani inawezekana itatusaidia tukapata chakula. Jan: Na hii walifanya mara nyingi kuhama hama? Romara: Tuseme mara nyingi kama kwa kihistoria ya Wanatta walikuwa wanahama hama sana. Sababu nikichukua kutoka eneo hilo hapo tulipo mpaka Ikizu, eneo hilo lote walikuwa wanahama... wanasikia tumejenga hapa akina fulani, wengine wamejenga hapo.. bas... nafikiri hapo sasa nijua kwamba kumbe wakati huu ilikuwa ni ya kuhamahama tu. Watu wenywe, kama sisi kikudi fulani tunaamua haizuru kutoka hapo Burungu tunaamua tuhamie kule. Tunahama. Tunaacha na Burunga wamejenga. Tunahamia sehemu ile tunakwenda tunajenga. Jan: Na watu wanajenga kwa kikundi au wanahama moja moja? Romara: Ah.. kwa kikundi ulikuwa wakati ule. Mwana mmoja uende ujenge porini utaishi? Ehhh. Jan: Kwa hiyo wanaweza kuchagua sehemu ya pori tu? Waanze upya? Romara: Ehh. Jan: Lakini Oruberi nzima wanaenda? Romara: Hiyo ilikuwa lazima. Jan: Wazee, vijana, wote? Romara: Ndiyo. Jan: Kama Oruberi moja wameamua kuhama wanahama wote. Vijana ndiyo wenye madaraka kuhamisha Oruberi kweli wataacha wazee? Ehh. Mayani: Mimi nina swali kidogo hapo. Swali kwenye Saiga. Eh wakati Asaiga inataka kutaacha, wanataka kutaacha Asaiga. Utuambia ni vitu gani vinavyotayarishwa au ni watu gani wanavyotayarishwa, ili Saiga hilo inakamilika inataacha? ... Hii nyingine inang'atuka nyingine inataka kushika madaraka. Ni mambo gani au vitu gani au watu gani wanaoweza kuchaguweka katika uongozi huo, ili Saiga inataacha? Romara: Nani... vitu vinavyohitajiwa pale au watu wanaohitajiwa pale hasa kwa vitu sina chochote nitakachosema. Labda kwenye sherehe hiyo wanahitaji ng'ombe wanachinja. Siku ya Saiga. Wanakula. Halafu katika uongozi wa Saiga wanachagua viongozi. Viongozi hawa wanaitwa Wachama. Mayani: Wangapi? Romara: Hu chagua wanane. Eh... kwa mfano kiongozi mkuu wao anaitwa Kaangati. Na wengineo. Mayani: Labda vitu vya kutayarisha ili Kaangati ili Saiga iwe na madaraka... kwa matayarisho... Romara: Mimi sielewi. .... Abachama bhose mbahabu ninihi.... Wachama wa siku hizi walikuwa wanapewa baada ya kuteuliwa kuwa Wachama wanapewa fimbo. Orutanya. Hiyo ndiyo fimbo la mchama. Hata kama ni kwenye vita la fimbo, hashiki fimbo nyingine. Yeye Orutanya wake ndiyo anakwenda nayo. Mayani: Ebere Mtoku.........................[Mayani's rough translation: "Byengera" -- the things that are brought from the 4 corners for this sherehe] Romari: Ah Ah. ............................................................. (205) [Mayani's rough translation: I don't know abou this because I did not do the business of the Saiga. When I went through "kutaacha" the wazee had prepared it all without our participation.] Isipokuwa kitu cha kuongeza pale Wachama wote hawavai nguo nyeupe wale nyekundu. Huo wanavaa nguo nyeusi. Nyamaganda: ...............................................(212) [Mayani's rough translation: Mbona pale samani nguo nyeusi haikuwepo, walipataje?] Romari: ....................................................... {Mayani's rough translation: Mtu anazungumza kitu ulichoona, zamani walivaa masagi... nguo ya nyamera, walitoa manyoya. Wakivaa nyeupe nchi (aase) itakuwa kavu, kama ikawa nyeupe sana. Kamaguka = nchi kuwa kavu. Nyamaganda: [Mayani's rough translation: nchi kuwa giza?] Romara: [Mayani's rough translation: hapana kuwa laaini.] Mosi: Kangati wabho huo abanasifake? [Mayani's rough translation: Kangati alikuwa na sifa gani?] [END OF TAPE #15, SIDE B, BEGIN TAPE #16 SIDE A] Romara: Awabho ............................................................ [Mayani's rough translation: Kwa wawe hawana mtoto amekufa. Baba yake yupo na Mama yupo. "Kutema Riburu" -- ndani ya Saro Kangati anapiga riburu, mahali wanapolala kutahiriwa kwenye kigori] Jan: Labda unaweza kuwa na kumbukumbu kuhusu njaa kuu ambazo zilikuwa kwenye nchi hii. Nilisikia kuna majina ya njaa nyingine, na kama historia kidogo ilikuwaje katika ile njaa? Romara: Njaa kubwa zilizopita, kwanza njaa kuu sana ilikuwa inaitwa Agechaa ya Magoro. Njaa ya Miguu. Jan: Nalitokea, Wajerumani walikuwepo? Romara: Walikuwa bado. Mmmm. Nafikiri baada ya hiyo kutokeo haichukua muda Wajerumani wakaja. Ehh. [AROUND 1882?] Jan: Sasa ilikuwaje katika ile njaa? Romara: Hiyo ndiyo ilishambulia watu sana, nchi hii karibu watu wooote walihamia Usukuma. Wakaenda kupona. Jan: Usukuma sehemu gani walienda? Romara: Sehemu yote kama Dutwa na .... jirani yake, Kanadi. Jan: Walikuwa na jamaa pale au walienda tu ku.... Romara: Ni kwenda tu. Jan: Hawakuwa na watu ambao wanawapokea vizuri? Romara: Hawakuwa nao lakini Wasukuma nao unajua wao walikuwa na ukarimu wao vilevile. Waliwapokea tu wageni wanapokuja. Kwa hiyo mimi nina imani waliwapokea maana yake watu wote kukimbilia kwa nchi ya watu halafu waende wapone na warudi salama... ilikuwa wana imani nzuri tu. Jan: Katika vizazi vyako kuna kumbukumbu ni nani ambaye alienda Usukuma na kurudi? Romara: Mama. Jan: Anaitwa nani? Romara: Mwinoki. Mama amekwenda msichana, nafikiri kama anayonihadithia haikosi sawa sawa na huyu tu [POINTS TO A CHILD OF ABOUT 10] au zaidi kwa sababu alitembea hapa mpaka Usukumani. Jan: Na alikuhadithia jinsi ilivyokuwa huko? Romara: Ehh, alinihadithia, walipofika pale walipata chakula wakala, sasa badaye wakasikia vyakula vimepatikana kwetu ndiyo wakaanze kurudi. Jan: Na walikaa huko kwa miaka? Au ilikuwa miezi tu? Romara: Nilifikiri .... kwa ... kama ni zaidi ni kwa mwaka moja. Jan: Na wengine wamebaki pale Usukumani? Romara: Wengi, walibaki wengi sana. Walibaki wengi sana. Wengine waliuzwa huko. Maana yake unakwenda watoto watatu, unafika kule sasa hakuna chakula unachukua mtoto mmoja unamwuza kwa wale wenye vyakula. Na wale wafanye biashara wanamnunua wanamsafirisha nchi nyingine nao wanakwenda kumwuza. Sasa wengi walipotelea huko kabisa. Jan: Na wao wakaingia kwenye ile biashara ya kwenda pwani na kuwa watumwa ambao wamefika mpaka Amerika? Romara: Hiyo historia ya kwamba walipelekwa huko... sidhani... Wanuza humo humo Usukumani tu. Mwl. Nyamaganda: Maana Usukuma ni nchi kubwa unaweza kutoka sehemu fulani kwa mfano Kwimba ukampeleka Maswa. Kwa ajili ya kumpoteza asije akarudi kwa jamaa zake. Jan: Lakini wakiuzwa pale wamekuwa kama watoto wa nyumbani au walikuwa kama watumwa ambao wana maisha mabaya. Romara: Hapana, watoto wa nyumbani. Wananunulia kwa ajili ya kumfanya kama mtoto wa nyumbani. Mwingine anaoa.... Jan: Hana maisha mabaya kama watumwa.... Romara: Hapana Jan: Kuna njaa nyingine ambayo ina jina lake? Romara: Njaa nyingine ilifuata wanasema ya Riranga. Agecha ya Riranga. ... Jan: Na maana ya Riranga? Romara: Jua kali. Jan: Ilifuata ile ya magoro? Romara: Ndiyo ilifuata ya magoro. Mwl. Nyamaganda: .............................. (203) [Mayani's rough translation: Is this when Mzee Wiranga was born? That is as he named after the hunger?] Romara: [Mayani's rough translation: Hapana ni jina tu, si sababu ya njaa, Wiranga ni jina la ukoo - ekehita.] Mayani: [Mayani's rough translation: Kweli mama yako Mwinoki na Baba Magotto wako mbali kwa umri?] Romara: [Mayani's rough translation: Sidhani kama ni tofauti labda wameachana kidogo, Mama anampita Magotto. Wakati walikwenda kupona Usukumani Mama Nyabikwabe, mama yake Mang'oha, Shangazi, alikwenda kutembea mpaka Usukuma, analingana na mama Mwinuki. Hawa wanaita "Wakienche" -- rika ya Akina Mama [WOMEN HAVE AGE-SET NAMES OF THEIR OWN!]] Mayani: [Mayani's rough translation: Mama Nyibikwabe alizaliwa mwaka gani?] Nyamaganda: [Mayani's rough translation: Wameweka utemi 1885, Megasa, Wakati baba alikuwa mdogo, anaachishwa titi. Mama Nyibikwade alikatika vidole vya miguu kwenge njaa. 1882 Baba Magotto alizaliwa. Nyawagamba alizaliwa kabla ya baba, Nyibikwabe labda mwaka 1878 kuzaliwa au kabla ya.] Romara: [Mayani's rough translation: Agecha ya Riranga, watu hawakuhama Usukuma, wakakwenda kununua chakula na kurudi. Hatu Usukuma walikuwa na njaa ule ule. Mama alisema walikuta nzige walikufa walipikwa na jua.] Augustine: ...................................... Romara: ............................................... Augustine: .......................................... Romara: Njaa ilichukua muda mreeefu sana, ila watu na jua kali, muda mrefu, maji yakakosa, majani yakakosa, hata ng'ombe wakaanza kula makonge hayo, ili wapate maji kidogo, kutafuna tafuna.... Jan: Na Megassa ameshaanza kuwa Mtemi au ilikuwa kabla yake? Romara: Hapo sina uhakika. Augustine: .................................. Romara: ................................ Mayani: ............................ Romara: ................................. Mayani: Kukisia ....... Romara: .... miaka 10 kutembea Usukuma ....... Jan: Kama hii ya magoro ilikuwa mama yako alikuwa msichana, hii ya Riranga, wewe ulikuwa.... Romara: Yeye alikuwa mtu mzima na mimi nilikuwa sijazaliwa mimi. Mayani: ............................................ Romara: ................................................ Mayani: .......................................................... Augustine:..................................................................... All: .........................................................................................(285) Mwl. Nyamaganda: ..........Megassa 1885..................... Mogoro 1882....................... Mayani: .................. Jan: Sasa mmekubaliana nini? Mayani: Si anatuambia anasema kwamba huko alikwenda hizi nzige.. unajua nzige? Alikuwa anakuta zimekauka, eh, hata hawataki kuzipika, wanasema, ah, hii imepikwa na jua. Jan: Ilikuwa wakati wa Riranga? Mayani: ehh Riranga. Jan: Lakini mmesema Wamaasai ni kabla ya... Augustine: Mama ameuliza mmekubaliana nini, makubaliana yetu ni kutafuta Megassa alitawala wakati gani. Tumekubaliana Megassa alitawala baada ya mwaka wa Njaa ya Miguu. Jan: Kwa hiyo ya Riranga Megassa alikuwa bado yupo? Augustine: Alikuwa mtawala. Ilihatukuwa na kumbukumbu la miaka. Mosi: Maana sasa walitoka kule wamekwenda wamerudi, sasa walikuwa wamemweka Mtemi. Romara: Maana wakati wamehama nafikiri, ye Tabaka, Rihe ya Tabaka......... Hantachega........... Jan: Rihe ya Tabaka? Romara: Ehh.................................... Mayani: [Mayani's rough translation: Rihe ya Tabaka, ni nani analo historia nacho?] Romara: .....bamenyere Hantachega............................ ..............................................................................................(436) [Mayani's rough translation: Rihe ya Tabaka ni pale walipokuwa wametoka kupona njaa Usukuma. Wamejenga Hantachega. Vita vya Tabaka imepigana wameshatoka Usukumani. Katika vita hiyo Wajerumani wameanza kuingia kwenye nchi hii. Wakipotoka kulikuwa na nafasi ya mlima njiani. Wamaasai wakajibanza pale kuua watu. Waliua Mjerumani. Mahali panaitwa Mchagata. Mzungu Mjerumani alikwenda pale kuwakmesha wasiwavizia watu. Watu wawili -- mmoja na banduki mmoja na risasi -- Maasai waliwaua wote. Baada ya njaa Wajerumani waliingia.] Jan: Kwa hiyo anasema Rihe ya Tabaka ni baada ya.... Mayani: Anasema wakati wametoka kwenye Agecha ya Magoro, ndiyo, wametoka tu, hawakuja moja kwa moja kuja huko, walijenga pale Hantacheega. Romara: Watu wengi walijenga Hantacheega. Jan: Baada ya kurudi kutoka Usukumani? Mayani: Ehh. Na hapo ndipo vita ilipoanza ya Maasai ya Tabaka. Jan: Na ilikuwa akina nani? Ni Wanatta tu au Waikoma, Waissenye? Romara: Hapo ilikuwa ni nani Wanatta walikuwemo, ilikuwa ni mchanganyiko wa makabila. Maana pale Hantachega walijenga Wanatta, Waikoma, tusema historia hii niliyo nayo ni Wanatta na Waikoma. Halafu na Wasukuma. Ndiyo walichangia vita hiyo. Wakauawa sana. Mayani: Ebu tueleze kama unaelewa kwa kirefu hiyo vita ya Hanatacheega. Romara: Vita ya Hantacheega, Wamaasai waliondoka huku, wao wanafuata ng'ombe kuuule kando la ziwa. ...Buringa... sasa walipofika pale Hantacheega waliona pale Hantacheega wamejenga kwenye njia yao. Basi, walikwenda mpaka kijiji cha nanani ... Hantachega... zaidi walikuwa ni Waikoma tu, ndiyo walikuwepo ... Sasa ilikuwa ni Saiga ya Akubura wakati huo... Saiga ya Abakuubura. .... Abaromure? Ehh. Abaromore na Abikoma? Bhose na Natta be............................................ (485).......................... [Mayani's rough translation: Saiga -- (Barumarancha) Wakabura Waromore -- wote Wanatta, Waikoma na Maasai waliitwa Saiga yao jina hilo. Wamaasai walifanya mazungumzo nao, sisi tunataka kwenda magaribi, nyancha, kupata ng'ombe, sisi ni Oromure, tukija msituzuie." Waikoma walikubali na wakala Ring'a nao. Baada ya kutoka walizungumza na wengine walikataa. Walipopita wamekwenda maneno yakapita kwa Natta na Sukuma, waliona haitawezekana. Waliona waenda kwa Mganga kuona kama tutaiweza. Walikwenda kwa Omugabo Gorigo, Mtaturu. Wazee walikataa wasipigane. Mganga alichukua mtoto wa kondoo, akachinja na kupika. Alipika ugali kidogo. Aliweka maziwa kwenye pembe. Aliwaambia vijana nane kula na kumaliza. Walishindwa kumaliza. Omugabo aliwaambia kula, wakashindwa. Muganga aliwaambie waache vita vyao, kama mlishindwa kumaliza chakula mtashindwa vita. Walikwenda nyumbani. Walipofika njiani wakashauriana wakasema, "kweli hatuwezi vita? Hapana. Amesema tupigane vita." Walipofika kwenye kijiji waliwaambia mganga anasema tupigane vita. Sasa walikuwa wanawangojea siku za kupigana zifike. Walipiga yowe sehemu zote, Sukuma na huko kwetu. Sukuma walitoka mbali. Siku ya kwanza na ya pili hawakuonekana. Siku ya tatu walisema kama hawaji turudi nyumbani. Siku hiyo waliangalia magaribi waliona vitu vingi vinakuja. Na Wamaasai pia waliona mashariki pameziba. Wamaasai walituma kijana kuja kuona. Walisema sisi hatuna maneno mengine sisi ni vita tu. Huyu alimpelekea majibu wanataka vita. Wamaaasai walijadili wapite. Wanakataa. Wamaasai walisema tuwakatie ng'ombe. Watu walikataa. Maasai walikusenya wakapuliza moto --- moshi ikaenda juu "korose" au dawa ni alama ya ushindi. "Abarema" [THE FARMERS, ANOTHER DIVISION, FARMERS AGAINST HERDERS] Wasukuma, Wanatta, Waikoma, Waissenye wote ni Abarema. Walijipanga -- mkono mmoja ukafika mpaka Mbalageti na mkono mwengine mpaka mbuga. Wamaasai walipojipanga mpaka wakavuka Mto Mbalageti , wakatokea nyuma yao. Mbugani walianza vita kali sana. Wamaasai waliwasukuma mahali pamoja, katikati. Waliuwawa sana. Walikwenda mpaka walichangyikana pamoja wote. Wamaasai na mkuki na Waikoma na upinde. Wakikupiga na mkuki na mwingine mshare. Watu wa Abarema walishindwa. ... Watu wengine walikuja kufanya matatizo wamekuja baadaye -- kikundi cha Wamaasai kuvizia watu. Waliua Mjerumani. Mwenyake alibeba sanduka la marisasi na banduki. Wamaasai waliwatokea nyuma. Jan: Kwa hiyo hii ilitokea baada ya njaa? Romara: Ehh baada ya njaa... Mayani: ....... [Mayani's rough translation: Mtu Wakikong'oti alikuwa wapi? Hakuenda kupona njaa Usukumani, akakaa hapa. Alisema watu wasiende bila kuwa mnyangi. Alipasua kondoo nusu kufanya Guho na nusu Ekise.] Romara: ......... [Mayani's rough translation -- sijui.] Mosi: ......... Jan: Waikoma walikuwa Hantacheega kwa ajili ya njaa pia? Romara: Si watu walihamia wengi wote Sukumani sasa ilikuwa njia ya kurudi... badala ya kurudi watu wenye miji wakatoka Usukuma wakaja wakajenga katika sehemu ile ya Hantachega, ni sehemu nzuri sana ya kilimo. Sasa wakaendesha maisha pale kwa kilimo kwa ajili ya kung'oja badaye wahame kuja.... Jan: Na wakati walipokuwa Usukumani waliiga mambo mengine kutoka Wasukuma au walirudi na wameanza kuwa na mambo ya Usukuma? Romara: Utamaduni ni ule ule. Mwl Nyamaganda: Labda ile maudodi labda walikuwa wanavaa. Romara: Ule udodi walikuwa wanavaa mkononi. Mayani: Ebere... Hayi kikong'oti bakutikari..... Romara: ............................... Jan: Au aina nyingi ya uganga unatoka Usukumani sivyo? Romara: Hawa waganga wengi ni Wasukuma. Jan: Lakini hii ni ya siku hizi au tangu zamani walianza kuwa na dawa kutoka Sukumani? Romara: Sukuma walikuwa na dawa toka wakati huo. Jan: Hata zamani waganga wa hapa Natta walikuwa na dawa kutoka Usukuma? Romara: Waganga..... ni jambo ambayo imeivwa tena nilikuwa mkubwa tu. Watu waliiga iga tabia na mila na desturi ya Kisukuma wakiwa hapahapa. Eh. Tulikuwa na Wasukuma wengi walikuja humu wanajifanya kama ni waganga basi vile Bagaru, niliona Wabagaru wanachanga changa mwili chale. Sasa wanapaka paka madawa yale ya rangi ya ambiro. Hawa ni... ilikuwa tabia iliivwa tu lakini watu walikuwa hapa sio kwa sababu walikuwa huko Usukumani. Jan: Na zamani waganga wa Natta na yao hawakuwa na yale kutoka Usukumani? Romara: Waganga walikuwa na yao. Jan: Na waganga wa mvua pia walikuwepo? Romara: Walikuwepo? Jan: Ya Wanatta? Si kutoka Usukumani? Romara: Ehh Jan: Kwa hiyo umemaliza katika njaa? Au bado zipo. Romara: Kwa njaa kama mtu ana sehemu ambayo hakuelewa nimsaidia mimi mwenyewe nimefirisika. Jan: Ya Riranga pia walienda Usukumani? Romara: Wa hapa? Hawa kwenda ila walikuwa wanaenda... kuenea na kurudi tu. Ya Riraga hawakuhama. Mosi: .......[Mayani's rough translation: Walihemea wapi?] Romara: ........[Usukumani wanashida pia. Bukuria -- Kurusana or Rosana mission] Jan: Walienda wapi? Romara: Huko Ukuriani. Jan: Wakati wa ule njaa wa Riranga? Romara: Maana wakati huo nao walikuwa na njaa hiyo. Jan: Lakini kaskazini hawakuwa nayo? Romara: Hawakuwa nayo. Jan: Na kabla ya ile njaa ya Mogoro kuna kumbukumbu wa njaa kabla ya hayo? Romara: Hapana .... Ila labda kumbukumbu niliyokuwa nikisikia ni maradhi ya kuharisha vyoo wanlikuwa wanaita Kyamunda. Ni maaradhi yaliyokuwa yaliingia hapo zamani kwa watu kwa kuharisha na kuharisha damu wanakufa. Hiyo ndiyo ninasikia historia ugonjwa huo unaitwa Kyamunda. [END OF TAPE #16, SIDE A, BEGIN SIDE B] Jan: Sasa, ulisikia jinsi Wajerumani walivyoweka huyu Megassa? Kuwa Mtemi wa kwanza... labda unayo historia kwa kirefu... Romara: Ninayo historia nilivyoelezwa ... Ilikuwa, Wajerumani walipofika hapa Natta ... Sasa kwa mfano sisi ...labda ni rudi nifanye kukukumbusha tu. Sisi Wanatta tulikuwa hatuna mtawala, mtawala ni ule Saiga. Saiga inapochukua madaraka ndiyo inakuwa mtawala wa nchi. Kwa utawala wetu ulikuwa ni wa demokrasia. (laugh) Sasa walipofika Wajerumani wao wakauliza Wanatta, je, Wanatta, tena wamewaita wote, wakauliza, "mkubwa wenu ni nani?" Sasa Wanatta katika mawazo yao wakatafuta ukubwa wa namna gani. Wakaenda kwenye nyangi zenywe. Wakamkuta Megassa ndiyo mkubwa kwa nyangi zote za kiNatta. Sasa wakawaambia mkubwa wetu ni huyu. Jan: Na kwa nyangi alikuwa amefika cheo gani. Romara: Nafikiri alikuwa amemaliza nyangi zote. Maana nyangi zooote mtu akizimaliza naye ni cheo kikubwa sana, wengi hawamalizi, unamaliza kiasi fulani, unakufa, unaacha, awe zingine unashindwa kuzimaliza kwa sababu hujafikia wakati wake wa kuimaliza. Eh. Jan: Megassa ameshakuwa mzee? Romara: Ndiyo wakati ule amekwisha kuwa mzee. Aliwekwa mzee tu. Sasa wakamchukua wakamweka kuwa mtemi. Ametawala muda mfupi tu halafu kabla ya hapo wakamshauri, kwa sababu aliona umri wake ni mdogo amebaki tu, hana uwezo wa kuongoza, sasa wakamshauri kwamba, "tunakuomba utupatie kijana wako ambaye twende tunamfundishe kazi." Bas yeye akawaita Wanatta tena, wale washauri wake. Akawauliza, "unaonaje, nasikia Wazungu wanavyosema?" Sasa Megassa alikuwa na vijana hawa, wawili, kijana wake wa kuzaa anaitwa Kisamo. Na halafu kuna kijana huyu Mtemi Rutuginga alikuwa ni kijana wake wa kununua. Sasa wakamwambia, 'kama wanahitaji hivi, hawa watu, inawezekana wana hira wanataka kwenda kumchinja mtoto wako, kwa hiyo usiwape Kisamo, wape huyo ulionunuliwa, hata kama wakienda kilio, basi." (laugh) Ndiyo akawapa Rutuginga, wakampeleka Shirati, twenda .... Shirati ilikuwa ni kama ...Wilaya... walikwenda kumfundisha jinsi ya kutawala. Sasa ndipo walipotoka kule wakaja ameshaelimishwa. Badaye Baba yake akapofuka macho, yeye akashika kama uwakili wa Mtemi. Jan: Hata kabla ya Megassa kufa? Romara: Eh. Kabla ya Megassa kufa. Ameshikilia madaraka hayo mpaka.... Megassa kufa si aliuawa na Maasai? Bas, baada ya kufa alienda akawa Mtemi moja kwa moja. Jan: Na kuhusu Utemi wake ulionaje? Romara: Rutiginga? Utemi uliendelea vizuri sana. Isipokuwa ilifikia sehemu fulani alikorofishana na Wanatta, Wanatta wakamkataa. Wakati huo Wadachi wamesha, wamohumo, bas, wakakorofishana Wanatta wakamkataa. Akaenda, akahama, akahamia Ngoreme. Jan: Na ilikuwa mambo gani? Romara: Sasa sielewi walikorofishana kwa vipi. Nafikiri labda sana sana sikuchunguza hapo, kulikuwa na watu fulani, unajua watu siku hizi sawa sawa na watu wa siasa unaona huyu ni kiongozi halafu anatokea mwingine anasema mimi ndiyo kiongozi safi. Labda walikuwa wanataka kumbadilishie wamweke kiongozi mwingine. Sasa akahamie kule... Wazungu walipopata habari hizo wakampa Chifu wa Issenye ajumulishe Natta kama sehemu yake. Sasa akawajumilisha, lakini waliohara, aliwafanya kama watumwa wake. Mwisho Wanatta wakakaa wasikilizana tena, walisema tumrudishe mtemi. Ndiyo wakamwendea tena arudi aje kuongoza, mpaka kufa. Ile mabadilika wake alibadilika kwa sababu ya siasa tu wameondoa mtemi. Jan: Aliporudi alifanya vizuri zaidi? Romara: Alifanya vizuri zaidi. Jan: Alijifunza? Romara: (laughter) Jan: Kwa kifupi mawasiliano na makabili wa majirani. Ilikuwaje katika historia? Romara: Katika historia mimi ninavyoelewa.... uhusiano wa majirani ulikuwa mzuri sana... Eh... hapa jirani yetu magharibi alikuwa ni Ikizu, sisi ni marafiki mpaka sasa. Hawa Ngurimi kaskazini walikuwa marafiki mpaka sasa. Jan: Na wao walikuwa marafiki bila kufanya Ring'a wala... mlikaa kwa amani tu? Romara: Kwa amani tu. Halafu jirani yetu wa Kusini walikuwa ni Wasukuma. Hawa ni marafiki zetu mpaka sasa. Hapa mashariki ilikuwa ni hawa Waikoma, Waikoma nao ni kama wandugu. eh... Sisi adui yetu tu ni Wamaasai. Ndiyo walikuja kwa ajili ya kutunyang'anya ng'ombe. Jan: Na ushirikiano na hawa majirani ambayo ilikuwa nzuri, mlikuwa mnaoana bila tatizo au ni mara chache? Romara: Bila tatizo. Jan: Na ilitokea mara nyingi kuoana? Romara: Ilitokea mara nyingi isipokuwa wakati ule kitu kimoja tu ... ilikuwa shida kwa msichana kuvuka kwenda kuolewa katika kabila nyingine, ilikuwa ni vigumu. Jan: Kwa nini? Romara: Kwa sababu wasichana nao walikuwa wachache .... Jan: Kwa hiyio wazee hawakupenda waende? Romara: Ehh... Waolewe humohumo... maana wakienda huko vijana hawa watawakosa kuoa. Hilo jambo ilikuwa katika kila kabila, lakini kama si msichana, labda mwanamke amekosana na mume anatafuta mume anavuka anakwenda tu. Jan: Kwa hasa mlikuwa mnaoana humu ndani? Romara: Ehh. Jan: Kwa mfano katika vizazi vyako upande wa mama au baba, ni nani ambao walitoka kabila nyingine? Romara: Hapana, mimi kwangu wote ni Wanatta. Jan: Na unaweza kukuta wengi kama wewe ambao wote ni Wanatta? Romara: Sio wengi, wengine unakuta wanachanganya. Wengine Wasukuma, hilo hilo, hasa Wasukuma waliolewa humo kwa wingi sana. Jan: Na vijana wakiwa na michezo wanaweza wakaalika Waikoma, Waissenye, wengine wakaja kucheza pamoja? Romara: Sisi taratibu zetu za michezo wakati tunacheza tulikuwa na uhuru kijana kutoka Natta akaenda akacheza Ikoma... na bila wasi wasi. Ehh. Kama vile, kwa mfano, labda kwa sababu wakati imekuwa Waikoma wametengana kidogo, wa hapa porini wakitenga, lakini jirani zetu kama Waissenye tulikuwa tuna... tukuanzishe mchezo kwetu hapa wao wanavuka wanakuja tunacheza. Wakianzisha kwao na sisi tunavuka. Tena kwa wingi, sio mtu moja au wawili, hapana. Tunakwenda tunacheza. Jan: Na kwa nyangi wanakuja? Romara: Kwa nyangi hapana, kwa nyangi labda nyangi ya kumlaki, kama pombe, mtu anaweza anakuja anakula.... Lakini nyangi ni nyangi ya watu tu. Ya kabila wazi (?). Jan: Na tena mambo ya Saiga hawawezi kuingia? Romara: Hapana, hawawezi kuingia. Jan: Na kwa biashara unaweza kwenda huko kufanya biashara bila kuogopa ogopa? Romara: Unaweza kwenda tu ... Na biashara si imeanza juzijuzi tu... wakati ule ulikuwepo biashara zaidi... na Wasukuma... Jan: Biashara gani? Romara: Biashara... sisi tulikuwa tunawinda wanyama... na Sukuma walikuwa nanani... tabia kusokota udodi, wanavaa mkononi. Sasa walikuwa wanahitaji sana mkia ya nyumbu wakati ule. Sasa vijana wa kwetu walikuwa wanajitahidi sana wanakwenda wanafuata nyumbu wakati wanakuja wanapiga nyumbu kwa wingi wanakusenya ili mikia wanakwenda nayo. Sasa ni uchumi huo. Hata na nyama ukipeleka wakati huo Usukuma... Sukuma katikati hawana nyama... basi unauza... sasa unauza unabadilisha kwa mfano kondoo, ng'ombe, ndizo tunakuja kufuga hapa. Zaidi biashara tulikuwa tunafahamiana na Wasukuma, lakini hawa wengine Waikoma na Wanatta, karibu mazingira yetu inafanana tu. Jan: Usukuma unarudi na nini? Unapata nini? Romara: Mifugo. Jan: Na ninyi mlienda huko au wao walikuja hapa? Romara: Sisi tunapeleka. Jan: Wao hawafiki hapa? Romara: Wao wakifika wanafika kwa shughuli zingine. Jan: Si biashara. Romara: Si biashara hiyo... Au wanakuja wanakuja kununua hiyo mkia, anakuja ananunua tu. Jan: Na mnaweza mkafika mpaka ziwani kufanya biashara, au biashara haikuwa na watu wa ziwani. Romara: Walikuwa wanafika. Kulikuwa hakuna kizuizi. Jan: Wajita waliweza kufika hapa kununua mambo hayo? Romara: Ndiyo Jan: Wajaluo waliwahi kufika hapa? Romara: Kwetu hapa? Wajaluo hawakuwahi kufika.... Mosi: Bosongo... Sumu [Mayani's rough translation: Sumu haikuwa biashara?] Romara: Sumu walikuwa wanapeleka kubadilishana na wawindaji. Wasukuma. Hata upande wa ziwani waliwapelekea sumu. Maana Wajita walikuwa vilevile wawandaji. Walikuwa wanahitaji sumu, wao hawajui kupika sumu, wanaiona tu, "hii ndiyo sumu?" Na Wanatta walikuwa mafundi kupika sumu peke yao katika makabila hayo. Jan: Na ile biashara ya meno ya tembo, mlikuwa mnafanya? Romara: Ah, meno ya tembo hapa kwetu hayakuwa na thamani sana. Kwa sababu hawakuwa na wawindaji wa tembo kwa siraha zetu hizi. Wakati wa zamani babu zetu waliwinda lakini baba zetu hawakuwinda wakati huu sisi hatukuwinda. Jan: Kwa hiyo ni nani ambao waliendesha biashara kubwa ya meno ya tembo... kufika Bagamoyo? Wandorobo? Romara: Mimi sijui, kwa sababu hawa Waarabu walipofika hapa... sikusikia kwamba walikuwa wananunua meno ya tembo. Waarabu walifika walikuwa wanawaita Machumbi. Amachumbi. Wao walikuwa wanaleta ushanga pamoja na hizi nguo, nguo za kwanza hizi walianza kuleta ni wao. Jan: Na hii ilikuwa kabla ya Wajerumani kufika. Romara: Ehh. Kabla ya Wajerumani. Jan: Walikuja kama watu wa biashara? Romara: Ndiyo. Ni watu wachache tu, hapa hawakufika kwa uwingi. Jan: Na wao wanatembea, hawana makao? Romara: Hawana makao. Augustine: Ebu, Nkiuliza swali, labda litakuweza kusaidia. Katika uwindaji wa tembo, natamwuliza msimulizi wako, kwa sababu tuna wimbo huu, Wa Rarori, Wapigali hawa, wimbo nawasilia kabia kuonyesha wawindaji wetu kama ulivyosema mababu zetu walikuwa wawindaji wa tembo si Baba zetu. Walikuwa wakiua matembo. Tembo hatumli, hatukuli nyama, waacha kwa sasa, tembo hatuli nyama yake, lakini walikuwa wanawinda. Sasa wale walikuwa wanawinda kwa ajili gani? Bila shaka ni meno, pengine wanaweza pengine kujaribu jaribu ku... ingawaje hawana historia ya kupata ufunu kidogo. Kwa sababu walikuwa wanawawinda hawa tembo. Wanapeleka wapi? Romara: Waliwawinda hawa tembo kwa ajili ya utamaduni. Kwa sababu tembo, unajua wakati wa michezo tulikuwa tunavaa bangili zake hapa... chasabati. Hizo zilikuwa zinahitajiwa sana. Sasa kama umeua tembo ukija na jina hilo anakuja mtu unabadilishana naye anakupa ng'ombe unaenda kukata yale meno. Meno yale unaanza kuyauza. Bangili. Na wewe unapata faida ndani. Mimi nilivyoelewa wao waliuziana humu humu tu hawakuwa na watu wengine kwenye ukoo maarufu wanasafirisha meno kwenda mbali. Ehh. Augustine: Sasa ndiyo hivyo, maana hakupata jiwabu kwa nini walikuwa wanawinda tembo. Jan: Lakini Waikoma wana ile meno ya Tembo makubwa. ... Machaba Romara: Wanayo. Jan: Na ninyi mlikuwa na asili kama hii? Romara: Sisi hatukuwa na asili hiyio. Na kihistoria wanasema sisi tulikuwa na pembe hizi mbili pembe za ng'ombe. Lakini Wanatta kwa sababu ukovu wao wenyewe wamezipoteza. Zile zilikuwa sawasawa ni ile meno ya nanihi... Mayani: ................................................................. Romara: ................... Mayani: Mfafunilie... Ikoma kuna watu ambao ni Waring'a wa Wanatta. Na hawa watu, hizo ring'a zilipatikanaje? Romara: ...Ring'a ukisikia "baring'a yitu" ni kwa sababu ya bhatu............................... ............................................................................................................ [Mayani's rough translation: Ring'a na Waissenye baada ya kukorofishana -- kuondoa mambo hayo kutengana tuheshimiana. Usifanye na Ikoma tu, hata na Issenye. Wanapigana wanafanya Ring'a na Issenye. Waikoma -- tumejenga nao karibu, wanajenga ng'ambo na Waikoma. Ikoma wanavuka ng'ambo wanakuja hapa, Mongate kwa mfano ni Natta.] Kwa mfano Natta... Ikoma... Issenye.... Kuacha kubwitana......................................... ..................... Mayani: ....Hamatike na Hamatike na ring'a..... Romara: ............. [Mayani's rough translation: Sijui. Ababoriho -- Bahimorumbe wa Ikoma.] Jan: Sasa tumekuwa na maswali mengi kwa muda mrefu. Labda umechoka sana. Romara: Sijachoka. Tena nafurahi sana. (laugh) Hata mimi inanikumbusha sana nakumbuke mengine karibu nimesahau. Mayani: Kwa hiyo unataka siku nyingine tuje? Romara: Safi, tunawakaribisha. Jan: Vizuri. Mayani: Bataka Nageech. ... Unamfahamu Bataka... ndiyo huyu Megasa... Romara: Ila tunasema majina yale sasa jina Bataga ni ya ujana. La baba na mama Megassa. Kama mimi ukichukua majina... kila kipindi lazima uwe na jina lingine. Nilipokuwa kijana nikaitwa Karokandukwa. Jan: Maana yake? Romara: Maana yake ni jina tu la kujitapia. Mimi ............................... (laughter) ...............[Mayani's rough translation: Jina la ujana -- Kirekyandukwa, kinachoma tope, kinang'uta tembe, hata kinang'uta. Alipofika Kigori alijiita Nyamsiheri -- mtu wa dharau. Maraba kwenye Kigori. 5 names in all.] Kipindi kingine....... Matatu yaliyoyataja, na mawili, jumla yangu ni matano. .......... ......................................................................... Jan: Na ile jina la kijana rafiki zako wote walikuita? Romara: Ehh. Wakati mwingine inavunja ule ya nyumbani. Unabadilisha ile ya nyumbani hata kufa. Ni mama tu anakuita nyumbani. Lakini nje..... Jan: Unapoenda kwa michezo unatamka ile majina ya kujisifia. Mosi: Tena kwenye michezo unajitapa na kujisifu, unasikia anazumgumza mengi, ni ya kutjitapa... Jan: Na hiyo yote ni kwenye michezo? Romara: Ehh. Mosi: Unapanda mori kabisa... Kama ni kucheza unacheza mpaka vumbi inatoka... (laugh) .... Mayani: .................... Ebitana birenge... [Mayani's rough translation: Natta, ina ebitana ngapi?] Romara: Ebitana........... Mantarera........ Kundukora....... ............ [Mayani's rough translation: Vingi, Mantarera, Kundukora, halafu kuna egitana cha Saiga. Kitana cha Bungirate, Kitana cha Nyamobora, Ekewankunywa, Mantarera -- nyuki. Sang'anga -- walikuwa huko wakati ule. Mayani: .................................[Mayani's rough translation: Sang'anga karibu na Nyabuta kapori kahapo] Romara: ................................ Augustine: ......chasaiga ........ Romara: ......... Mayani: .............. Mosi: Unaelewa maana ya Ebitana? Jan: Ni ile ukienda kwenye vita unashika? Mosi: Eh... kusaidia mambo ya vita..... Romara: ........... Mayani: Romara: Mayani: ....Sang'ang'a......... Romara: .............................. Sang'ang'a ..................... Kitaara na Mochuri. ................. Mayani: ... Mongate...... Yasigeta..... Romara: Mayani: ....Ebimenyo.... Romara: Gitaraga na Mochuri...... Mayani: Amasambwa...... Romara: .................[Mayani's rough translation: Ebimenyo -- Sang'anga karibu na Mochuri, Mongate -- Karibu na Grumeti peke yake, Kyasigeta -- kusini Ft. Ikoma -- kuishi mwanzoni. Kitaraga na Mochuri kuna Emisambwa. Wakitaka kutafuta mvua wanaenda pale, pamoja na Ekiteko na Nyichoka. Nyichoka ni mto, nyoka. Abamoriho Abarumarancha wanafahamu risambwa wa Nyichoka. Ketiku ni Abamoriho Busaye.] Mayani: Jan: Emisambwa? .. Mayani: Ehh. Ndiyo Nyitaka na Mochuri, pamoja na Ekitiko, pamoja na Nyichoka, kwenye mto wa Nyichoka. ... Romara: Nyichoka........... Jan: Na nani anafanya? Ekihita au? Akina nani? Mayani: Nyichoka...... Romara: .... Abamoriho... [END OF TAPE #16, SIDE B, BEGIN TAPE #17, SIDE A] Romara: ....Gitiku..... Namoriho Busaye.......[Mayani's rough translation: 1) Kitaraga -- mlima, 2) Nyichoka -- maji, nyoka, 3) Rubana, Eketiko, mto dimbwi (Wasaye). Kitaraga na Mochui ni Rumarancha. Jan: Wanafanya nini kwenye ile mitambiko yao? Mosi: Kama hali ya hewa imekuwa mbaya, mvua imekosa, wanaenda kutambikia. Romara: Wakitambikia pale, jinsi tunavyoelezwa kihistoria, sijafika pale, lakini hata hivi sasa wanakwenda wakati mwingine wanapata mafanikio. Ikiwa kiangazi kabisa kabisa wakiamua wakwenda pale na kondoo mweusi wanachinja pale, wanafanya mitambiko yake pale wanacheza na ngoma pale, kutoka pale hawawezi kufika nyumbani ... watanyeshewa njiani. (laugh) Jan: Kwa hiyo ni Saiga wanaotawala wanaenda? Au ni nani? Romara: Hapana. Watakwenda watu wote, Wanatta wote wanaohusika pale, lakini wako wahusika wenye kwenda kufanya shughuli hii. Jan: Na wahusika ni akina nani? Romara: Sasa hapa sina historia. Kwa kuna Mzee Kabucho ndiyo anaelewa. Jan: Kwa hiyo ni kwamba kwenye ukoo wao wanahusika na ile... misambwa. Romara: Ehhh... Ukoo wanaohusika kufika pale wote tumekwenda lakini wanaokwenda kushika kutambikia ni wakina fulani. Ndiyo wanatambikia kwa niaba yetu. Sawa sawa kama tunavyokwenda kanisani, si wote tunakwenda kusali, lakini mwenye kutambikia si ni padre? (laugh) Jan: Na ni hasa kwenye milima? Au kuna sehemu nyingine? Romara: Hapo pote, kuna mitambiko ya mlima huko wanaita Kitaraga, huo wanatambikia vilevile ni mlimani. Halafu Nyichoka kuna bwawa la maji, dimbwi, humo wanasema kuna nyoka. Na ndimo wanamtambikia. Halafu pale Rubana kuna Getiko, ni dimbwi vilevile kubwa sana, haiishi maji, toka maji yamo tu. Lakini ukienda kwenye dimbwi. Sasa haya matambiko yetu ni mara hii... mara tatu. Jan: Tatu ni nini na nini? Romara: Kwenye mlima, kwenye mito, kwenye, Nyichoka. Jan: Kwa hiyo hakuna zaidi ya hizo? Romara: Hakuna... labda kama yapo nimesahau... lakini ... Jan: Na hizo ni kwa nchi zima, kwa hiyo kama nchi zima inakosa mvua, wanaweza wanakwenda wapi? Romara: Wanakwenda kuomba sasa pale mitambiko. Jan: Wanachagua ipi? Romara: Sasa ni kadri jinsi mnavyoishi kuna, unajua, wakati wowote, unaishi, tunaishi kama, tunasema Saiga, sasa Saiga nyingine wanaabudu mahali pengine na nyingine inaabudu mahali pengine. Ehh. Jan: Kwa ni, kwa mfano Warumarancha wanasehemu yao? Romara: Warumarancha wanaabudu Kitaraga na Mochuri. Halafu na hii Nyichoka ni Warumarancha. Na Getiku ni Abasaye. Romara: ..... Jan: Hakuna? Romara: Ibada wote ni kwa ajili ya Wanatta wote. Isipokuwa wanakwenda ni kama viongozi. Jan: Wanaamini kwamba kitu pale ambacho kitawasaidia au wanaona ni mahali pazuri pa kuomba. Romara: Kinacho saidia.... Mosi: Ah Ah wanaamini kwamba kuna kitu ambacho wanaamini kuna kitu fulani, kwa mfano hapo Nyichoka, tunasema kuna nyoka mle? Wanaenda wanaelewa kwamba kuna nyoka wanaenda kuomba. Sasa Geteko mle kuna nini ambacho wanaamini kuna kitu mle? Romara: Kuna mtu, kuna kiumbe kama binadamu. Tena wanasema ukienda kuomba kinatoka nchi, kinapiga aaah, kinatoka, kinaona hivi, ... Jan: Kama mtu? Romara: Kama mtu. Jan: Na nyingine? Romara: Hii ya mlimani sijui. Mosi: Wanasema kuna vitungi, kuna magiha, ............. Pale kwenye mlima mle huwa tunasikia kuna ... vile wanawake wanaweka mafiga matatu... sasa pale kuna mafiga aina mbili, kuna figa la mwanamke na figa la mwanaume, viungu viwili vidogo, kama vimechemsha kitu... sasa pale vitu hivi, wanapika na wanaabudu. Sasa wanawapa maombi yao. Jan: Unaweza kunionyesha kwenye ramani ziko wapi? ... [END OF INTERVIEW, SIDE A]

Show Full Transcript Download Transcript PDF

Field Notes

I11 Fieldnotes Mariko Romara Kisigiro Nata Origins Baba Nyamunywa was a hunter Nyasigonko was an Msonjo from Loliondo. They met where she lived at a rock, cave where there was water. Ekingita na lolende (?) to make fire. She had ulezi. Bwanda [ORIGINS/NATA; SONJO; HUNTERS; BWANDA] To the east were only the Maasai Ikoma over the Grumeti Issenye at Nyeberekera [BOUNDARIES] Issenye had an mganga leader that kept the Maasai back. But the Maasai took away the rain for many years and there was no food. They went to other waganga to ask what to do. They tied their mganga to a marangare tree snag and cut it down, he died. Thus the Maasai had a chance to come in and raid. The Issenye fled nearer to the Nata and were accepted. [PROPHETS/ISENYE] The settlements followed the Saiga. Nyagoti -- Abakihocha, all lived there. They were quiet and separted out among the Wanata Saiga -- Nagusi -- Wasaye Ngureti -- Sasakwa and Ngotera Rumarancha -- Mumaroga [SETTLEMENTS; SAIGA/TERRITORY] Fighting between Saiga and Saiga Abakinaho and Abasanduka Abasaye and Abangirate Fighting by fimbo for the utawala [SAIGA/RULE] Chasiriti 1. Amanyema 2. Abaganda 3. Abakira first two are Kigori Abateneku -- wanaondelewa wazee Rikora Mwanyachuma Mwanyasaye Sherehe ya kutembea -- kukerera [RIKORA] Four Hamati 1. Abamoriho -- Abairegi, oburwe, ang'ombe 2. Abagikwe 3. Abamwancha 4. [HAMATE] ihumbo, ekeburu. Ikelisho. Kutaacha Asaiga Sherere -- kill a cow Eight Abachama and Kang'ati Orutanya -- his fimbo, of the Mchama. Vita ya fimbo. Clothes black, not red or white. Abachama. Sifa of the Kang'atiā€¦ [SAIGA/RITUAL; SAIGA/LEADERS] Agecha ya Magoro -- 1882??? Before the Germans came. People went to Sukuma, Dutwa and Kanadi. His mother Mwinoki went as a young girl. Others stayed back in Sukuma. Others were sold there. Megassa became chief in 1885. [FAMINE] Agecha ya Riranga -- Jua Kali His mother was grown by then. But Romara was not yet born. Rihe rya Tabaka Muzecha. Hantachega. Were settled there after leaving Sukuma from the hunger. Wanata, Waikoma and Wasukuma were all settled there. They had built on the passage way to Buringa by the Maasai to raid. The Waikoma Saiga of Abakubura made a Ring'a with the Abikwabe. [NDABAKA; MAASAI; RAIDS; PEACEMAKING] Kyamunda -- disease of diorera, kipindu pindu. [DISEASE] Megasa He was of the top Nyangi rank and became the Chief. He had two sons -- Kisamo who was born of him and Rutigenga who was bought. They were sent to Shirati to school. [MEGASA] Trade Tails and Arrow poison to Sukuma Amachumbi -- strangers, Arabs, brought cloth Ivory for bracelets [TRADE; SUKUMA; STRANGERS] Ikoma -- Ring'a na Wanata [RELATIONS] Amagiha ? Ebitana 1. Manterera 2. Kundakura [KITANA]

Show Full Field Notes Download Field Notes PDF

Related Items (Vitu vinavyohusiana)